NUVUS ORDO SECLORUM... Msaada. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NUVUS ORDO SECLORUM... Msaada.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiby, Mar 12, 2010.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Katika dola moja ya kimarekani pana picha ya piramidi ambayo kifuniko chake cha juu ni jicho. Pia kwa juu pana maandishi haya ANNUIT SEPTIS na kwa chini yake pana maandishi haya NUVOS ORDO SECLORUM na chini yake THE GREAT SEAL. Hii nuvos ordo seclorum inasemekana ina maanisha secular order ikiwa na maana non-religious(yaani wasio na dini) cha kukanganya pembeni mwa piramidi pana maandishi IN GOD WE TRUST. Sasa naomba msaada kwa wana JF anaefahamu:-
  -Nini maana ya hili neno ANNUIT SEPTIS?
  -Kama serikali haina dini kwa maana ya secular order hii tena IN GOD WE TRUST Yaamaanisha kwamba wasio na dini bado hata hivyo wana mungu?
  -.Na hii GREAT SEAL huu ni mhuri mkuu wa nini na hii alama ya piramidi asili yake ni nini?
  Tafadhalini naomba msaada wenu wachambuzi wa mambo.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Unge google tu mazee

  In GOD we trust maana yake ni G = Gold, O= Oil , na D= Diamond
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280

  Ahsante mkuu. Something is better than nothing. Hapa nipata kianzio na bado natumaini kupata zaidi.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  MZEE HUKO UNAKOKWENDA NI MBALI, NI BORA UNGEANZIA NYUMBANI KWANZA; KATIBA YAKO YA TANZANIA INAKWAMBIA SERIKALI HAINA DINI, LAKINI UKIJA KWENYE WIMBO WA TAIFA TUNAIMBA MUNGU IBARIKI TANZANIA,
  SWALI LINARUDI PALEPALE NI MUNGU GANI HUYO WAKATI KATIBA INASEMA SERIKALI HAINA DINI, NA WASIO ABUDU MUNGU (KINGUNGE), WANA HAKI GANI YA KUIMBA HUU WIMBO WA TAIFA?

  mzee toa kwanza kibanzi ndio utaluiona boroti
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  an•nu•it coep•tis

  Pronunciation: (än'nOO-it koip'tis; Eng. an'yOO-it sep'tis), [key] Latin.
  He (God) has favored our undertakings: a motto on the reverse of the great seal of the U.S. (adapted from Vergil's Aeneid IX:625).

  Source: http://dictionary.infoplease.com/annuit-coeptis
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa ufupi Marekani ni dola iliyoamua kutengeanisha Kanisa na Serikali (Church and State) kutokana na zahama walizozipata huko Ulaya wakati wa zama za giza (Dark Age). Ila hiyo haimaanisha waliacha Msingi wao wa Ukristo wa Kiprotestanti (Protestant Ethic). Pia ukumbuke kuwa zama hizo Ukristo (Christianity) ulikuwa umekumbatiana sana na dhana ya Ustaarabu (Civilization) ambao ulikuwa ukisambazwa duniani na Ubeberu (Imperialism). Ndio maana walichinja Watu wa Asili ya Marekani wakati wanaingia Marekani. Kisha wakachukua mabibi na mababu zetu utumwani huko Amerika. Hivyo usishangae kuona hizi alama za ajabu kwenye Dola ya Kimarekani, zote zinaashiria kuwa hilo ni taifa lilolijikita katika Udini, Usiri na Ubeberu wa kujaribu kuleta mfumo mmoja wa utawala duniani - A New World Order. Itazame tena hiyo dola utaona neno E pluribus unum, yaani, 'Out of many One'/'Umoja utakanao na Wengi'. Na ile alama ya piramidi lenye jicho ni alama ya Freemasons.
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280

  Hashima yako mkuu. Sasa hilo jicho lililo alama ya freemasons linamaanisha kuwa taifa la Marekani limejengwa juu ya misingi ya doctrine ya freemasons?
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280

  Hapa ndio patam mkuu. Hili boriti tulilo nalo hufikiri kwamba ni athari za matokeo ya kujisalimisha chini ya mfumo mmoja wa kuiongoza dunia yaani world order? Sidhani kama tuna hiari yetu wenyewe kuwa na mfumo wa kiutawala nje ya huu.
   
Loading...