Kuna bro alioa demu,demu akawa na kazi ya utumishi,bro akapanda cheo,kufika sehemu mafuso yakanunuliwa,na demu akawa na uhakika wa jumba la kifahari na mafuso ya mchanga yanaleta laki tatu kwa siku,yule manzi si kamuwangia jamaa hainuki kwenye wheel chair mwaka wa kumi sasa na mbususu hawezi kula anakula kwa macho tuu.mwanamke amegeuka meneja wa familia. bro anabaki kuita tuu jina,na mwangalizi ni ndugu wa mwanaume,Hawa watu weka mbali na watotoInawezekana
1. Umeoa fukara na sasa kapata uhuru wa kifedha.
2. Umeoa mjinga na sasa kapata pesa ndio wauona ujinga wake.
3. Ulikuwa unamnyanyasa wakati hana pesa, na sasa kapata pesa ni muda wa kulipiza kisasi.
Hitimisho, katika yote hayo juu umeoa mwanamke asiyekuheshimu/asiyekutii...
Atalia vibaya huyoMwalimu wake kipofu tena alishakufa
na umesema hutaki kuvunja io ndoa,,mpeleke kwa huyo mama ake na dada zake basiNi kweli, ndg zake hasa mama na dada zake wanaamini Mimi ndiye mwenye matatizo ila kaka zake wanapingana naye vikali
Akikutangaza kuwa hutoi matumizi unakufa? Mpuuze tu. Dawa kiburi mpe jeuri. Tafuta vijana wa kazi ongea nao chemba, waibe duka zima, wasiache hata dekio. Akifungua tena, wanapita nalo again. Yani ni tukio juu ya tukio.
Ka ana bwana anaempa mtaji wachoke wao. Inaumiza sana kuwa na mwenza unaempambania kwa maendeleo ya familia alafu akuletee fistula ya moyo.
HAPA NDIO KOSA LAKO LILIPOIli kupunguza ukali wa maisha na kuondoa utegemezi kwa mambo madogo madogo, niliamua kufungua kibanda cha duka na kumkabidhi mke wangu ili kisaidie kwa baadhi ya mahitaji muhimu ya nyumbani
😌😌 tumshauri afuate nyayo zako. Anamdekeza sana my wife wake huyu.Nakubaliana naww
Sasa mbona ivo Tena. Wanaume ni WA yeyote according to Albert charamila😌😌 tumshauri afuate nyayo zako. Anamdekeza sana my wife wake huyu.
# na mi nikifa mume wangu asioe.
Acha kutetea ujingaMaduka yanafilisika hasa ukiwa na tabia ya kutoa mahitaji ya nyumbani.
Ukitaka biashara isiyumbe kila mwisho wa mwezi mwongezee mzigo dukani.
Sema na umemchoka tu, yaani hizi nguo za kike za elfu 25 na perfume ndo vivunje ndoa.
Hebu tuliza akili angalia familia yako.
binti kiziwi njoo usome comments.
Mwachie na usijihusishe na chochote kwenye hilo duka. Endelea kufungua miradi mingine kaa huko ukipiga kazi. Usisahau kuwa kwenye maisha kuna wewe mwenyewe bila ya mtu mwingine. Jijali brotherMimi ni muajiriwa katika sekta ya umma mke wangu sio mwajiriwa yaani ni mama wa nyumbani. Tuko kwenye ndoa ya kikristo kwa miaka 14 na tumejaaliwa watoto.
Ili kupunguza ukali wa maisha na kuondoa utegemezi kwa mambo madogo madogo, niliamua kufungua kibanda cha duka na kumkabidhi mke wangu ili kisaidie kwa baadhi ya mahitaji muhimu ya nyumbani huku Mimi nikitumia sehemu ya mshahara kuwekeza kwenye maeneo mengine ya maendeleo.
Ni mwaka mmoja na miezi kadhaa imepita tangu nimfungulie mke wangu biashara lakini jambo la kusikitisha ni kuwa sioni tena faida ya kibanda kile maana mke wangu anabadilisha aina za nguo na marashi huku nikimuuliza anadai kuwa ananiheshimisha kwa watu. Pia ananitangaza kwa ndg na jamaa zake kuwa sitoi matumizi yeye ndiye anayetoa matumizi.
Tumekaa vikao kadha wa kadha tukihusisha ndg zetu lakini haonekani kubadilika na kikao cha mwisho alitamka kuwa mtaji wangu umeishahivyo uliomo ni wa kwake.
Hali hii imesababisha migogoro ya mara kwa mara na sioni tena raha ya ndoa.
Pia hali hii imenijengea tabia ya kumchukia mke wangu mara kwa mara ninashikwa na hasira hata bila sababu ya msingi japo kiukweli Sina nia ya kuvunja ndoa yangu bali ninahitaji mke abadili tabia.
Ninaomba ushauri ili kunusuru ndoa yangu.
Ahsanteni.