NURU YA ROHONI.
Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu.
Nakuomba sana niangazishe;
Ukanitazame kwa huruma tu,
/: Ukanitulize
Mimi maskini.:/
Futa dhambi zangu,
Kwa damu yako.
Hasira ya Mungu iniondoke.
Machubuko yako, hata mateso,
/: Niyawaze vema
Rohoni mwangu.:/
Nakutumaini peke yako tu,
Niwe mtumwa wako
Pote nilipo, utanikubali,
Sina mashaka!
/: Nitakushukuru
Pasipo mwisho.:/