Nunua Vitu kwa masikini kwa bei ya Haki

200K

Member
Apr 2, 2020
44
34
Barabarani unakutana na mwanamke mchuuzi maskini mwenye mtoto mgongoni,Unashusha kioo cha gari lako na kumuuuliza kwa sauti ya kijeshi

"UNAUZA BEI GANI HIVYO VITUNGUU NA HIZO NDIZI"?

Muuzaji maskini kwa upole anakujibu "shilingi elfu moja kwa kichane cha ndizi na shilingi elfu moja kwa fungu la vitunguu"

Kwa kiburi unamwambia unahitaji kichane cha ndizi kwa shilingi "mia tano" na fungu la vitunguu kwa shilingi "mia tano" au vinginevyo haununui

Muuzaji maskini anakubaliana na hali na kukujibu
"CHUKUA TU KWA BEI UNAYOTAKA,SIJAUZA CHOCHOTE TANGU ASUBUHI WALAU SASA NIPATE CHA KUNUNULIA WATOTO CHAKULA CHA USIKU"

Amepata hasara lakini Zaidi anaenda kukununulia mfuko wa kuweka bidhaa ulizo nunua

Unamwagiza afanye haraka vinginevyo utabadili mawazo

Anaomba msamaha na kwa tabasamu anakukabidhi bidhaa zako,anakubariki pia kwa kumuungisha.

Unamrushia hela na kuchomoka kwa kasi na kumwachia wingu la "vumbi" na moshi linalomfunika yeye na mtoto

Anakohoa wakati anaweka vizuri fedha kidogo alizopata.
#UMASKINI

unafika sasa kwenye Hotel ya nyota 5,ambapo unakutana na rafiki zako
Unawaambia waagize chakula na vinywaji kadiri wanavyotaka

Wanaagiza vyakula vya gharama kubwa na mabaki ya chakula ni mengi kuliko chakula walichokula

Gharama nzima inakua laki tano
Unalipa bila kuomba kupunguziwa,unampa muhudumu "tip" ya shilingi elfu kumi kama shukrani kwa chakula ambacho hamkula hata nusu yake.

"TUKIO HILI LINAWEZA KUONEKANA LA KAWAIDA KABISA KWAKO LAKINI SIO LA KIBINADAMU"

POINT NI KWAMBA

Kwanini kila mara tunaonesha tuna nguvu kubishania bei Wakati tunaponunua kutoka kwa maskini ?

Kwanini tunakua wakorofi tunaponunua kwa wahitaji ?

Kwanini tunaonesha ukarimu kwa wale ambao wala hawahitaji ukarimu wetu ?

kwanini tunaonesha "upole na utu" tunaponunua kwa watu matajiri ambao wanaona hela yetu Kama chenji ndogo tu ?

Kwanini tunaelekeza fedha zetu kwenye bahari ya fedha ?

TAFADHARI
nunua vitu rahisi kwa maskini kwa bei ya haki,wakati mwingine lipa na ziada unaponunua kutoka kwa mwanamke maskini.

TAFAKARI
 
Ushauri mzuri sana. Hasa maskini akipata fedha ndiyo ananunua kwa manyanyaso sana. Mimi siyo tajiri lakini hakuna kitu nachojali kama kununua vitu vinavyouzwa na watu kama kina mama na wachuuzi wa ''jua kali'' kwa bei nzuri kwao. Nikiwa na uwezo sijadiliani nao bei mara mbili kuomba punguzo kubwa. Kuna watu wenye hulka ya kunyanyasa wachuuzi wadogo wadogo. Kuna jamaa mmoja alikuwa ananunua mayai mpaka aje ayachukuwe alikuwa amemhenyesha yule mchuuzi mpaka nikaona huruma. Mara anauliza una uhakika siyo mayai ya kenge haya? Mara anamtuma kakamuwashia sigara.
 
sio ustaarabu kbx ani
 
Hili liwe fundisho kwetu ni zaidi ya somo. Tabia za kujiona miungu watu tuachane nazo.
 
Huwa nanunua hata nikiwa sina uitaji sana nanulilia hata wengine, sababu nilijifunza kununua walau hata kumsaidia huyo kuuza kwa njia hiyo.
 
Kuna jirani yangu mmoja alikuwa na shida, akawa anauza kiwanja chenye msingi kwa nusu ya bei aliyonunulia kiwanja.
Nikamkatalia, nikamwambia asiuze ila asubiri wiki mbili nimrudishie hela kamili aliyotumia kununua kile kiwanja...
Ukarimu ni muhimu. Ni muhimu sana kujali shida za wengine na kuto take advantage!
 
Ushauri mzuri sana. Hasa maskini akipata fedha ndiyo ananunua kwa manyanyaso sana. Mimi siyo tajiri lakini hakuna kitu nachojali kama kununua vitu vinavyouzwa na watu kama kina mama na wachuuzi wa ''jua kali'' kwa bei nzuri kwao. Nikiwa na uwezo sijadiliani nao bei mara mbili kuomba punguzo kubwa. Kuna watu wenye hulka ya kunyanyasa wachuuzi wadogo wadogo. Kuna jamaa mmoja alikuwa ananunua mayai mpaka aje ayachukuwe alikuwa amemhenyesha yule mchuuzi mpaka nikaona huruma. Mara anauliza una uhakika siyo mayai ya kenge haya? Mara anamtuma kakamuwashia sigara.
Limbukeni huyo hii dunia inahitaji uwe na adabu na unyenyekevu mkubwa hujui kesho nin kitatokea.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom