Nunda (17) Mungu anaishi chooni !!

Nunda (17) Mungu anaishi chooni !!

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Nunda alikuwa yupo darasani na siku hii mwalimu aliuliza darasa ,Je mnaweza kufikiria Mungu anaishi wapi ?Au Mungu yupo wapi ?

Akanyanyua mtoto mmoja wa kike akasema Mungu yupo Mbinguni kwa sababu huko ndiko iliko Pepo ,mwalimu akasema sawa jawabu zuri ,mwengine kama yupo akatokea mtoto mwengine yeye akasema Mungu yupo katika nyoyo zetu ,mwalimu akaonekana kufurahi na kutabasamu huku akisema nzuri sana .

Haya kama yupo mwengine ? Darasa zima ilionekana hakuna alienyoosha mkono isipokuwa Nunda peke yake ,dah mwalimu akaona huu sasa mtihani ,kwani alijitahidi kumkwepa na kumpotezea,ila hakuna budi :confused2:

Mwalimu ; Haya Nunda unafikiria Mungu yupo wapi ?

Nunda :Chooooni.

Mwalimu ; Chhooni ? ,huku mwalimu akiwa hajaamini jawabu alilopewah.

NUNDA;Ndio mwalimu kwani kila siku asubuhi baba honigongea mlango wa chooni marakwamara na kusema.."GOD, are you still there ?":becky:
 
Achen kufuru nyie watu

Hapa hakufuru mtu ,hiyo ni true story ,ni kawaida iliyo wazi kabisa watu kusema ,,Mungu wangu bado hujatoka chooni ?

Ila kwa Nunda tunaweza kusema ilikuwa tungo tata kwake na kwa vile bado ni mtoto inawezekana alifahamu hivyo ,ila kwa mwenye tumbo la kuhara akienda kugonga mlango wa chooni mala ya kwanza kisha ukakohoa ,akaondoka halafu akarudi tena na kukugongea ukakohoa kwa sauti ya kushinikiza kwamba bado upo ,basi lazima atasema Mungu wangu fanya utoke huko ,hivi wadau haya ni mambo ya kuzua !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom