Nukuu toka tamko la waislaamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nukuu toka tamko la waislaamu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by emalau, Jan 22, 2011.

 1. e

  emalau JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]Wadau kuna mwana JF alituwekea hapa janvini tamko la waislamu, nililazimika kuprint tamko lenyewe nikalisome kama kuna la maana la kujifunza. Nimejaribu kunukuu sehemu chache na kuzitupa hapa janvini ili ikiwezekana tujadili kidogo ingawa mengi yamesemwa, na tuangalie kama maneno waliyotamka na kuandika yalistahili kutamkwa na viongozi wa dini au la. Nukuu zenyewe ni kama ifuatavyo:[/FONT]


  1) maaskofu walithubutu hata kuweka kando mafundisho ya Biblia yao juu ya masuala ya uzinzi wakawahimiza waumini kumpigia kura mtu wanayemtaka bila kujali kwamba anakabiliwa na kashfa ya kupora mke wa mtu. Waliwaambia wasihangaike na maisha binafsi ya ndoa ya mgombea.  2) Waislamu tumelazimika kukutana na kutoa tamko hili kwa sababu matukio yanayotokea hivi sasa yanaonesha kuwa wale ambao Watanzania walikataa kuwapa uongozi na Ilani yao iliyoandaliwa na maaskofu, ndio sasa wanaielekeza nchi pa kwenda huku viongozi wa CCM na serikali wakijitahidi kadiri ya uwezo wao kunyenyekea kwa maaskofu hao.

  3) Ndio maana tangu wakati wa Nyerere hadi leo, uchaguzi wa viongozi wa Waislamu husimamiwa na vyombo vya dola. Nia ikiwa ni kutokuwapa Waislamu uhuru wa kuwachagua viongozi wao.

  4) mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanadhoofishwa katika kila hali, na ni makosa makubwa kuwaimarisha kiuchumi au kielimu

  5) 5) Kwa kushinikizwa na Maaskofu serikali iliwauwa Waislamu watatu Mwembechai pasi na hatia yoyote


  6) 6) Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa fidia.

  7) Umefika sasa wakati wa kugawana nchi ili Waislamu wanaochukiwa na kunyimwa fursa sawa na Wakristo waishi katika maeneo yenye Waislamu wengi na Wakristo waishi katika maeneo yenye Wakristo wengi.

  8) Kugawana nchi kutawawezesha Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC bila ya kuwakera Maaskofu.

  9) Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.


  [FONT=&quot]My take: Pamoja na mambo mengine waliyosema, nukuu No. 7 na 8 zimenitisha zaidi na wameweka historia mbaya katika nchi yetu, itabaki katika kumbukumbu kwamba waislaamu wan chi hii walishakusudia kuigawa nchi kwa misingi ya dini.

  [/FONT]   
 2. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh!!!!
   
 3. V

  Vumbi Senior Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hili ndilo tatizo la kwenda madrasa badala ya shule. Unategemea maisha mazuri bila kuwa na elimu utayapata wapi? nani atakuajiri na elimu ya madrasa? nani atakuajiri elimu ya Form (IV) au (VI) ambayo umefeli?. Kama kuwa na maisha mazuri ni kuishi waislamu peke yao mbona Pakistan, Algeria, Misri, Tunisia, Gambia, Yemen, etc hawana maisha mazuri?. Mataifa mengi ya kiislamu yaliendekeza udini badala ya tafiti za Kisayansi na technologia pamoja na uwekezaji kwenye elimu hivyo mataifa mengi yanamaisha magumu sana. Mataifa ya kiislamu yenyemaisha mazuri ni yale yenye mafuta na hayo mafuta yakiisha haya mataifa yatakuwa na shida sana. Waislamu wa Tanzani pelekeni watoto shule vinginevyo mtabaki mnalalamika huku hamna solution ya matatizo yanayowakabili.
   
 4. c

  chama JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Msiandike kwa ushabiki ambao hauna maana yoyote, waislamu wa Tanzania hawajatoa tamko lolote usichukulie kauli za mtu mmoja ukaigeuza ni kauli ya watanzania, waislamu wengi tu wanaathirika na utawala huu hali zao zimekuwa duni, hao wanaojitia ni viongozi wa waislamu walichaguliwa na nani? Wapo waislamu wengi tu walinufaika na mfumo wa elimu wakati wa Mwl. Nyerere hii dhana ya kuwa hatukupewa elimu ni upuuzi na imepitwa na wakati. Mwl. Nyerere kwa kutaka kusaidia waislamu alianzisha Bakwata ili tuwe na taasisi ambao itasaidia msukumo wa kielimu kwa waislamu, Bakwata imetuangusha waislamu kwa kukosa dira, leo hii tutalaumu wakristo kuwa wanapata nafasi za upendeleo kielimu? Karibu kila dhehebu la kikristo lina shule na vyuo vyenye kueleweka, Bakwata wanachojua ni kuomba tende tu hata Hijja wameshindwa kuisismamia. Waislamu tunatakiwa kufanya mabadiliko ya kweli ili tuwe na chombo madhubuti chenye kusimamia elimu ya vijana wetu, tuache kumlaumu Nyerere, tukumbuke Nyerere alitaifisha mashule ya kidini ili kuhakikisha kila mtanzania anapata nafasi sawa.
   
 5. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Kila jambo linao wakati wake! Ni rahisi sana kuufunika moto lakini moshi unaweza kupenya! Ukisikia manung'uniko na kisha huyafanyii kazi unatarajia nini? kama ilivokuwa Sudani ya Kusini si ajabu na Tanzania ikawa! sishangai kwa sababu hatuishi dunia tofauti na hii tuliyomo. Tunapaswa kujifunza na kutazama baadhi za mantiki za maneno. Na tusimame katika ukweli badala yake tutazidi kuharibu badala ya kutengeneza tukifanya ushabiki na unafiki!
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280

  Hapa umenifurahisha, kwa hiyo maana yake ni kuwa CCM licha ya kutupuuza lakini lazima ing'oke. kura tano.
   
 7. B

  Bull JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii mbona tulmesha ijibu??? au mnaanzisha topic mkipata majibu mnafunga na kuanzisha ingine ????

  kwa sababu siyaoni majibu kibao niliyochangia na nilivyomfaamisha mtoa mada
   
 8. c

  chama JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nadhani hujui nini unachokisema, matatizo ya waislamu Tanzania ni tofauti na hizo nchi ulizozitaja, zipo nchi nyingi za kiislamu zinaheshimika kielimu, mfano umeitaja Misri, Misri ni nchi ya kwanza duniani kuanzisha mfumo wa elimu ya university, Al Azhar university ndio chuo kikuu cha kwanza duniani kilianzishwa 969 AD ni chuo kinachoheshimika duniani, umaskini hautokani itikadi za kidini wala sayansi na teknologia haziongozi nchi, wanaongoza nchi ni wanasiasa mfano India na China zote zimepiga hatua kubwa kwenye sayansi na teknologia lakini India wananchi wake ni masikini sana sasa na hao pia ni waislamu?
   
 9. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi CCM hawajatoa jibu lolote kwa kero hizi za waislamu? Wao wamekuwa madarakani miaka hii yote. Kumbe kwa siri walikuwa wanatekeleza mkakati wa kukandamiza waislamu. Basi udhalimu wao utakuwa umepita kiasi!!! Makamba atoe majibu ya kero hizi hadharani. Chadema ni chama cha jana na wala hakijawahi kukamata dola. Hii ni kesi ya CCM
   
Loading...