Nukuu Sita za Nyerere ambazo CCM hawana budi kuzitafakari kwa makini sana leo hii

  1. "Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?"
  2. "Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii."
  3. "Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?"
  4. "Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga."
  5. "Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili."
  6. "Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe...."
Na ya saba ambayo aliitoa siku nyingi sana;

7. "Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika" - Mwalimu Nyerere (Januari, 1966)

Na nyingine ya nane;

8. "Kwani fursa iko mbele yetu na inategemea kama tuna ujasiri wa kuichukua. Kwani uchaguzi uliopo siyo kati ya kubadilika au kutobadilika; uchaguzi kwa Afrika ni kati ya kujibadilisha au kubadilishwa &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; kubadilisha maisha yetu wenyewe kwa mwongozo wetu, au kubadilishwa na matokeo ya nguvu zilizo nje ya udhibiti wetu.. .Tunapendelea kushiriki katika kutengeneza hatima yetu sisi wenyewe" &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG];MwalimuNyerere (Januari, 1966)

Nukuu hizi zimo katika kitabu kinachoitwa : Reflections on leadership in Africa: forty years after independence : essays in honour of Mwalimu Julius K. Nyerere, on the occasion of his 75th birthday ' , by Haroub Othman, VUB University Press, 01 Jul 2000.
Tatizo viongozi walitegemea kutuburuza kwa sababu ya ujinga wetu sasa maelfu ya wasomi wanamwagwa mitaani kila mwaka bila ajira! Time will tell
 
Mnamlisha maneno Mwalimu iz not fare

Umeishia elimu ambayo hamkukufundishwa kitu kinaitwa references, kwa hiyo nakuelewa. Hata hivyo usikurupuke kujibu thread kama topic zinazoongelewa huzipendi au huzielewi. Hatupo kwenye ushabiki kama wa mpira hapa.
 
Kwa nukuu hizi utaambiwa Mwalimu aliwachukia matajiri. Mwalimu alitaka mtu atajirike KIHALALI. Alitaka pia matajiri wahangaike na utajiri. Wakae mbali na utajiri wao wakitaka kuwaongoza watu. Hatukumwelewa. Mwalimu alitaka akikuuliza utajiri umeupataje using'ate ulimi kutafuta maelezo. Alikuwa na sheria nzuri sana ya kupambana na kuzuia rushwa. Ikachakachuliwa mwaka 1997 na 2007. Sasa hauwezi kumsimamisha mtuhumiwa yeyote mahakamani akueleze vijisenti na mali nyingine alizonazo kazipataje. Sheria inakulazimisha wewe unayemtuhumu ndio utafute ushahidi!
Tunakoelekea kubaya.
This is very informative! Haya Magufuli anayejipambanua kupambana na rushwa, kesharekebisha hiki?
 
This is very informative! Haya Magufuli anayejipambanua kupambana na rushwa, kesharekebisha hiki?
Sidhani kama viongozi wetu wana tabia ya kusoma vitabu vya Nyerere au vinavyoongea juu ya Nyerere. Kila siku ni kusoma gazeti la Uhuru na kujipongeza jinsi wanavyofanya kazi nzuri, kwa sababu hizo ndizo habari zinazoandikwa kwenye Uhuru
 
Sidhani kama viongozi wetu wana tabia ya kusoma vitabu vya Nyerere au vinavyoongea juu ya Nyerere. Kila siku ni kusoma gazeti la Uhuru na kujipongeza jinsi wanavyofanya kazi nzuri, kwa sababu hizo ndizo habari zinazoandikwa kwenye Uhuru
Na kuangalia kipindi cha shilawadu!
 
Back
Top Bottom