Nukuu Sita za Nyerere ambazo CCM hawana budi kuzitafakari kwa makini sana leo hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nukuu Sita za Nyerere ambazo CCM hawana budi kuzitafakari kwa makini sana leo hii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Aug 28, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  1. "Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?"
  2. "Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii."
  3. "Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?"
  4. "Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga."
  5. "Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili."
  6. "Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe...."

  Na ya saba ambayo aliitoa siku nyingi sana;

  7. "Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika" - Mwalimu Nyerere (Januari, 1966)


  Na nyingine ya nane;

  8. "Kwani fursa iko mbele yetu na inategemea kama tuna ujasiri wa kuichukua. Kwani uchaguzi uliopo siyo kati ya kubadilika au kutobadilika; uchaguzi kwa Afrika ni kati ya kujibadilisha au kubadilishwa; kubadilisha maisha yetu wenyewe kwa mwongozo wetu, au kubadilishwa na matokeo ya nguvu zilizo nje ya udhibiti wetu.. .Tunapendelea kushiriki katika kutengeneza hatima yetu sisi wenyewe";MwalimuNyerere (Januari, 1966)

  Nukuu hizi zimo katika kitabu kinachoitwa : Reflections on leadership in Africa: forty years after independence : essays in honour of Mwalimu Julius K. Nyerere, on the occasion of his 75th birthday ' , by Haroub Othman, VUB University Press, 01 Jul 2000.
   
 2. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...da...kweli. Ogopa sana mtu akishakata tamaa. Ana uwezo wa kuamua lolote lile!
   
 3. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Sisiem wana macho lakini hawaoni,wana masikio lakini hawasikii.
   
 4. Root

  Root JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,307
  Likes Received: 13,015
  Trophy Points: 280
  Dah hii kweli na ipo siku patanuka tena itaanza kama matani
   
 5. srinavas

  srinavas JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 2,729
  Likes Received: 1,231
  Trophy Points: 280
  ongera kamanda endelea kuwakilisha chamma
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  nimependa sana sana nukuu hizi maana nimeamua kuzi print na kuziweka kwa ajili ya kuzirejea mara kwa mara
   
 7. egbert44

  egbert44 JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 17, 2006
  Messages: 361
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimekubali kuwa amani ni zao la matumaini ........ kuwa aliye juu mngoje chini usimpandie, akupigae shavu la kulia mpe na la kushoto, mla mla leo mla jana kala nn?, ukitaka cha uvunguni usibinue kitanda na mengine mengi hahahahahahahahaha!
   
 8. Kiumbemzito

  Kiumbemzito Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Kaka hapo nimeiona ya saba ndio ya kweli, na karibia itatokea.
   
 9. a

  andrews JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nikiwa kama mtanzania ninayeishi uk naanzisha harambee ya kununua mask na na miwani ya kuzuia macho yasidhurike na mabomu ya askari wa ccm ffu chadema inapofanya mikutano,maana sasa lazima tujitolee kwa hali na mali kuikomboa nchi yetu kaburu aliwauwa akina solomoni mahlangu akina steve biko lakini mauwaji na mabomu na mbwa kuuma watu na kumuweka mandela ndani kwa miaka 27 haikurudisha nyuma mapambano ya kuwaondoa makaburu na leo afrika kusini ni nchi huru na ccm ifahamu vijana wananguvu kuliko ffu na polisi wao iko siku tutasema sasa basi na hapo kikwete na maswahiba zake watakumbukwa kwa uandaaji wao wa umwagaji wa damu is amatter of time bomu la tz likilipuka hakuna atakayesalimika ndani ya ccm maana lazima kuwashugulikia kwa njia hiyo hyo wanayoitumia.nitajitolea mask 1000 na miwani yake kwa kuanzia hili
   
 10. Malcom Lumumba

  Malcom Lumumba JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 4,843
  Likes Received: 8,197
  Trophy Points: 280
  ndugu zangu yule mzee alikuwa chosen by God na pia humo humo ndani ya CCM watu ambao Nyerere aliwapenda na kuwaamini ndiyo walikuja kumgeuka na hiyo laana itawatafuna vizazi vyao vyote,.......mkubwa hiyo ndo gospel tunataka kuisikia watu waone wanakoenda
   
 11. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ukweli utabaki kuwa ukweli hata upotoshwe namna gani Sita na Nyerere waliyoyasema ni ukweli wala haupigiki ccm wanajipa matumani huku wakijua hakuna mamlaka iliyokaa milele madarakani dunia. siku yaja ccm watalia na wengine kuikimbia nchi na wengine kujiua ili kukwepa mkono wa sheria
   
 12. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Namfananisha nape na ally makemiko huko iraq
   
 13. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Mtu akipiga uluzi sana mwisho wake ni kuimba!
   
 14. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #14
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  hata mimi naamini muda si mrefu kila mtu atanena kwa lugha yake.
   
 15. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,142
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  Nukuu # 7 ndiyo nimeipenda,r.i.p mwl...tutakukumbuka milele
   
 16. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Ungeziboresha kidogo kwa kuweka semi za kufunga na kufungua. Pia ungeweka tarehe/mwaka na ikiwezekana mahali alikotoa hizo semi. Asante
   
 17. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,371
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  MWL(R.I.P.) ALIKUWA KAMA NABII NDIO MAANA NAPENDA KUSIKIZA NUKUU ZAKE SANA. (sina uhakika na nukuu alizotoa mleta mada hapo juu kama ni genuine) MWL ALIKUWA HASOMI POPOTE HOTUBA ZAKE NA MOSTLY ALIWAFANYA WASIKILIZAJI WAKE WACHEKE THEN ANATOA POINTS.
   
 18. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mkuu zinapatikana wapi? Kitabu au tape?
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa nukuu hizi utaambiwa Mwalimu aliwachukia matajiri. Mwalimu alitaka mtu atajirike KIHALALI. Alitaka pia matajiri wahangaike na utajiri. Wakae mbali na utajiri wao wakitaka kuwaongoza watu. Hatukumwelewa. Mwalimu alitaka akikuuliza utajiri umeupataje using'ate ulimi kutafuta maelezo. Alikuwa na sheria nzuri sana ya kupambana na kuzuia rushwa. Ikachakachuliwa mwaka 1997 na 2007. Sasa hauwezi kumsimamisha mtuhumiwa yeyote mahakamani akueleze vijisenti na mali nyingine alizonazo kazipataje. Sheria inakulazimisha wewe unayemtuhumu ndio utafute ushahidi!
  Tunakoelekea kubaya.
   
 20. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280

  Nahisi ulikuwa unataka kumfananisha Nape na aliyekuwa waziri wa habari nchini Iraq Al-Saaf...
  Lakini ishu ni kuwa ukamchanganya na Ally Majid Al-tikrit almaaruf kama Chemical Ally.
   
Loading...