Nukuu ya Baba wa Taifa inayoishi

Aug 11, 2018
11
45
Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?

Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.

Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?

Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.

Wengi katika watu wa nchi zetu ni wajinga ndiyo maana hukubali kutawaliwa hivyo.

Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu.

Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira (idiots), kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe.

Ni ukweli usiopingika kuwa masuala ya maendeleo ni masuala halisi na hayawezi kuwa masuala ya ubabaishaji tu.

Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili.By Mwalimu J.K.Nyerere.
 
All TRUTH

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
4,842
2,000

Sawa muda ukifika tutaelewa

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom