Jackal
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 9,556
- 12,675
Kweli mkuu umechambua vizuri.Hayo mambo ni ya inner circle. Ni wale wabobezi ndio wanaelewa haya!Kwa bahati mbaya Bashiru hajui kuwa ndani ya ccm kuna ccm mbili. Ccm dola na ccm chama cha siasa. Ccm dola ndio inaamua nchi iendeshwe vipi na hiyo ndio inayoratibu nani awe kiongozi. Ccm dola ndio inayopora kura na kutoheshimu box la kura. Ccm dola inaundwa na viongozi wote wastaafu hasa wenye kumiliki mali walizochukua kwa wizi. Kundi hili la ccm dola linashirikisha viongozi wote wastaafu wa serikali na wa vyombo vya dola na taasisi nyingine. Hawa wanatumia ccm chama cha siasa kuhadaa umma kwamba ccm ni chama cha siasa. Ccm dola ndio yenye wazee wanaoamini kwenye mambo ya matambiko ya nchi hii kama mwenge wa uhuru na muungano. Kundi hili linaamini kwenye ushirikina sana, kulinda mali zao na madaraka. Wako radhi damu imwagike lakini ccm isitokee madarakani
Kuna ccm chama cha siasa chini ya Bashiru, hawa ni wale wanaomini kwenye kufanya siasa za ushindani lakini wana uwezo mdogo kwenye siasa za hoja. Hawana maamuzi yoyote ndani ya chama kwani hawajui chama na nchi inaendeshwaje. Kwenye kundi hili ndio kulipojaa watu wanaojipendekeza, wanafiki, wafanya fitina, wasaka tonge, wazinzi nk. Hawa ndio huvalishwa nguo za chama kwenye kila jambo kutokana na kuwa na viherehere ili wapate mlo wa siku. Hawa ndio hutumika kuiba kura, kuratibu vikundi vya kihalafu kufanya ukatili wakati wa uchaguzi na hushirikiana kwa karibu na vyombo vya dola baada ya kuchukua maagizo toka ndani ya ccm dola. Huyu Bashiri anajitahidi kuifanya ccm ikubalike lakini inakuwa ngumu ndio maana unaona anakuwa mkweli japo anahofia usalama wake, huku akiona ccm ikishinda kwa mbinu ovu ambazo yeye hashirikishwi. Isipokiwa anajua dhahiri ccm haiko madarakani kwa ridhaa ya wananchi bali kwa utashi wa kundi la ccm dola.