Nukta Nyeusi

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Siku moja professor wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi wake wajiandae na Test anayowapa muda huo huo.

Wanafunzi walisubiri kwa uoga mno hasa ukizingatia aliwaambia ghafla mno. Professor aliwagawia karatasi za maswali huku upande wa maandishi akiufunika chini na kuwatamkia kwamba yeyote asifunue karatasi mpaka atakapowaruhusu.

Baada ya kumaliza kuwagawia karatasi ya maswali kwa wote, professor akawaambia wafunue karatasi na kuanza kufanya mtihani.

Kwa mshangao, kila mtu akaona ya kwamba hakuna maswali yoyote katika ile karatasi, isipokuwa nukta kubwa nyeusi katikati ya karatasi.

Professor baada ya kuona mshangao kwa kila mwanafunzi, akawaambia hivi, "nataka kila mtu aandike kuhusu anachokiaona kwenye karatasi"

Wanafunzi wakachanganyikiwa, na kuanza kuandika vitu ambavyo hawajazoea.

Baada ya muda kwisha, Professor alichukua karatasi zote na akaanza kusoma majibu ya kila mmoja mbele ya darasa.

Wanafunzi wote walikuwa wameelezea ile nukta kubwa nyeusi, wakaelezea 'position' yake katikati ya karatasi, rangi ya ile nukta n.k.

Baada ya professor kumaliza kusoma majibu ya wanafunzi wote, darasa lilikaa kimya na Professor akaanza kuelezea.

"Sitaenda kuwapa marks kwenye hii Test, nilitaka niwape tu kitu cha kuwafikirisha. Hakuna hata mmoja aliyeandika na kuelezea kuhusu sehemu nyeupe ya karatasi. Kila mmoja wenu amelenga kwenye nukta kubwa nyeusi iliyokuwa katikati ya karatasi.

Hakuna hata mmoja kati yetu anayeangalia sehemu nyeupe ya karatasi iliyopo katika maisha ya wengine. Utasikia huyo mzinzi, huyo mlevi, huyo mgomvi, huyo fisadi, huyo muongo , ana makalio makubwa... !!!

Nukta nyeusi ni ndogo sana ukifananisha na kila kitu ambacho tumejaliwa nacho na Mwenyezi Mungu. Ila ndicho kitu kinachochafua akili zetu.

Ondoa macho na masikio kutoka nukta nyeusi katika maisha yako, anza kuangalia weupe wa karatasi.
 
idea ya Dot jeus na karatas nimeshaisoma katika kitabu cha LENGO LA MPINGA KRISTO!!!! mwandish wake WILLIAM L. BHOKE! sehemu hyo inafafanua sawia na wewe,,, ila inahusu juu ya waumin walivo na mtazamo hasi kwa viongoz wao w dini muda wote wana wawazia hilo doa jeusi kumbe hawajijui kama wanazidi kuua imani yao na kumpanulia tabasamu kubwa shetani,,,,,, asante kwakuileta idea hii hapa jf,,, maana ni wachache wao hupenda kusoma vijitabu vya dini ila mitandaon ni active member full time,.
 
Bwana asigwa naomba nikutaarifu kuwa hii nimeisave kwa ajili ya matumizi yangu ya binafsi. BIG UP
Hi itakuwa chakula yangu ya akili kwa leo, nitapata muda nikae alone to digest and put in my life. Thanks again and again
 
I never thought of the white space myself. Thanks Mkuu. Imefungua chapter mpya kwa maisha yangu.
 
Apo kwa mfano,unawaongelea ma professors wa nchi gani labda?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom