zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,930
- 30,445
Habari za jioni wakuu, kuna mengi yameongelewa na Mheshimiwa Rais leo ila kuna moja limenishtua sana na hilo ni kuona Mhe Spika Job Ndugai alipokubali kupeleka sheria ya madini na gesi kufanyiwa marekebisho bungeni wakati yeye mwenyewe akiwa naibu spika alihusika kufanikisha muswada ule mbovu kupitishwa mwezi julai 2015 na kibaya zaidi ililetwa kwa hati ya dharura na hata wapinzani walipokosoa mtindo huo waliishia kuzomewa na kutolewa nje sasa kipi kimebadilika leo Ndugai anakubali muswada kwa sasa una makosa ila 2015 haukuwa na makosa?????
Pili nitashangaa sana wabunge wa CCM wataokubali kufanyia marekebisho muswada ule maana wao walipitisha kwa kura ya ndio na wakasema wapinzani wanapinga kila kitu sasa kipi kimebadilika ndani ya hii miaka miwili hadi wakubali kufanyia marekebisho muswada walioupitisha wenyewe kwa mbwembwe nyingi???
Tatu nachoshangaa ni kivipi Rais anampa order ndugai ashughulikie muswada huo wakati huyo huyo ndugai ndio alihusika kuupitisha???
Kwakweli nina maswali mengi sana ila kikubwa ni kwamba nasubiri kusikia mbunge wa kwanza wa ccm akiridhia muswada ule wa gesi kufanyiwa marekebisho wakati waliupitisha wao kwa mbwembwe nyingi na kejeli kwa upinzani
Ni hayo tu