Ntagazwa ataka mawaziri wasiwe wabunge

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Ramadhan Semtawa

WAZIRI mwandamizi katika serikali ya awamu ya pili na tatu, Arcado Ntagazwa, ameshauri mawaziri wasiwe wabunge ili kutenganisha nguvu za bunge na serikali.

Kauli ya Ntagazwa inakuja kipindi ambacho mjadala huo, umeanza kutawala ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baada ya Kenya kutangaza mabadiliko makubwa ya katiba kuzuia mawaziri wasiwe wabunge.


Ntagazwa akizungumza jana kwa njia ya simu, alisema hatua ya waziri kuwa mbunge inanyima fursa ya uwakilishi mzuri jimboni.


"Unajua kuna jambo la Collective Responsibility (uwajibikaji wa pamoja), mbunge akiwa waziri hawezi kuwakilisha vema matatizo ya jimbo kwa sababu hawezi kuikosoa serikali," alifafanua Ntagazwa wakati akichangia maoni kupitia safu ya Gumzo la Wiki inayochapishwa katika gazeti la Mwananchi Jumapili.


Makala hayo ya Gumzo la Wiki, yalibeba kichwa cha Habari: "Wakati ni huu, mawaziri wasiwe wabunge."


Akitoa maoni yake, alisema kwamba, nchi kama Cameroon, mbunge akishateuliwa kuwa waziri, nafasi take inachukuliwa na mtu wa pili katika matokeo ya uchaguzi.



"Mimi kusema ukweli, ningependa na sisi sasa tuangalie mfumo wetu wa uongozi wa dola, ili tuweze kufumua pale ambapo tunaona kuna mapungufu," alisema Ntangazwa.


Alisema wananchi wanapaswa kuwasilishwa vema majimboni kwao, lakini fursa hiyo, haiwezi kutimia vema kama mbunge atakuwa ni sehemu ya serikali kwa maana ya waziri.


Ntagazwa alisema
mfumo wa waziri kutokuwa mbunge umekuwa ukitumika pia katika katiba ya Rwanda, ambayo waziri anapoitwa bungeni hujikuta katika wakati mgumu kama atakuwa haifahamu vema wizara yake.

Tayari mawaziri wawili wamepoteza kazi zao nchini Rwanda baada ya kushindwa kujibu vema maswali ya wabunge bungeni, licha ya kuitwa zaidi ya mara tatu.
 
Serikali ya CCM inaweza kutoa maamuzi kama haya kweli?!
Kwamba mawaziri wasiwe wabunge?

I doubt!
 
Atawaudhi wengi ambao wanachukulia ubunge kama tiketi ya kupatia uwaziri. Anachosema Ntagazwa ni sahihi kabisa, rejea hata ile tafiti ya kitengo cha Uwazi pale Twaweza iliyowaumbua mawaziri katika capacity yao kama wabunge kuwa ni mabubu.

Kingine pia unajua talent pool itakuwa kubwa sana kama wakiitikia wito huu maana kuna wataalamu wengi tu wasiotaka siasa ila wangeweza kuendesha wizara kwa uhakika.
 
Hawa jamaa wamezidi unafiki, hata kama anachokisema ni kweli, hivi kwanini hakusema wakti ule yeye akiwa waziri? au sasa ndio ameona ni wakati muafaka kwa vile yeye sio waziri tena?
Ntagazwa aache unafiki!
 
Tena itasaidia sana kwa sababu wapo Wabunge ambao hawathubutu kuikosia Serikali ama huifagilia Serikali hata pasipohusika wakiwa na 'agenda' ya kudhani kwamba kwa kufanya hivyo hawataonekana wanaipinga Serikali. Wanadhani kwa kufanya hivyo wanaweza kuonekana ni watetezi wa Serikali na hatimaye kuteuliwa kuwa mawaziri, manaibu, etc.!
 
Hawa jamaa wamezidi unafiki, hata kama anachokisema ni kweli, hivi kwanini hakusema wakti ule yeye akiwa waziri? au sasa ndio ameona ni wakati muafaka kwa vile yeye sio waziri tena?
Ntagazwa aache unafiki!
Ntagazwa is a free citizen of a democratic country of Tanzania where freedom of speech is permissive. Yaelekea una chuki binafsi ambayo ni hatari kwa demokrasia!
 
Vema kujadili uzuri wa hoja yenyewe. Kama mzee wetu amefunuliwa kwa wakati huu mambo mazuri, tuyaache kwa sababu tu hayakujitokeza wakati akiwa kwenye nafasi ya kufanya hivyo? Kama ni unafifiki au vyovyote iwavyo, hapa hoja ni je maoni yake yana mashiko? Binafsi naona kwa maana ya kutenganisha utendaji wa mihimili mitatu ya serikali, basi utaratibu wa kuwa na mawaziri ambao kwa upande mwingine ni wabunge ubadilishwe. Mawaziri wasitoke miongoni mwa wabunge. Sambamba na hilo, kwa maoni yangu naona nafasi kama za wakuu wa mikoa na wilaya, kama kweli wanachofanya ndichio wanachotakiwa kufanya hazina maana wala tija kwa wavuja jasho wa nchi hii.
 
Hawa jamaa wamezidi unafiki, hata kama anachokisema ni kweli, hivi kwanini hakusema wakti ule yeye akiwa waziri? au sasa ndio ameona ni wakati muafaka kwa vile yeye sio waziri tena?
Ntagazwa aache unafiki!
Baelelze baeleze watu wazima wanapokuwa wanafiki wakiwa ndani mmm wakitoka mijikelele ndio hao hao akina Qaresi
 
Boramaisha nafurahi kwa kutambua kuwa Mzee wa mtemba, Arcado Ntagazwa kama raia wengine wote wa TZ ana uhuru wa kusema has akwenye nchi hii ya "kidemokrasia". Na pia nataka kukuhakikishia kuwa mimi sina chuki binafsi na Arcado! in contrary namuheshimu kwa sababu aliwahi kuwa waziri wangu, tatizo langu ni kwa nini sasa! kama alivyowahi kuuliza mbunge mmoja "alikwina" yaani alikuwa wapi?
Anyway, nafikiri ni vyema kumuunga mkono FM, tuachane na Arcado ( yeye ni mnafiki basi), tujadili uzuri wa hoja hii kwa maslahi yetu. Mimi nafikiri katika haya mabadiliko ya sheria hasa ile ya kutenganisha biashara na siasa waweke kipengere hiki pia!
 
...
Akitoa maoni yake, alisema kwamba, nchi kama Cameroon, mbunge akishateuliwa kuwa waziri, nafasi take inachukuliwa na mtu wa pili katika matokeo ya uchaguzi.
Sipati picha mfumo huu ukija Bongo, kwani kuna watu wataukataa uwaziri. Ukiteuliwa kuwa waziri, unakuwa si mbunge tena. Baraza la Mawaziri likivunjwa na ukapigwa chini, huwezi kurudi bungeni tena kwani nafasi yako inakuwa ilishachukuliwa na mtu mwingine, kwa hiyo unapoteza vyote :D
 
Back
Top Bottom