Ntafikaje chuo cha mipango Dodoma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ntafikaje chuo cha mipango Dodoma?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by salosalo, Aug 8, 2012.

 1. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Nataka kwenda chuo cha mipango Dodoma nikitokea Arusha kwa magari ya abilia.
  1. Nitatakiwa nishukie kituo gani?
  2. Baada ya kushuka kuna umbali gani mpaka hapo chuoni ?
  3. kama safari itaenda vizuri, je ntafika mida gani kama nikiondoka Arusha saa 12 asubuhi?
  4. Je nitapata gari ya abiria ya kuelekea chuoni?
  5. Vipi kuhusu maeneo chuo kilipo, ntapata nyumba za kulala wageni?
  Naombeni mwongozo tafadhali maana naenda kwenye interview ambayo itafanyika tarehe 13/08/2012. Hivyo nataka kujua ili nijipange siku ya kusafiri.
  Je kama nikiondoka huku Arusha tar 12 ntaweza kuwahi usaili bila kulazimisha ?
   
 2. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ukifika stand dodoma, uliza stend kuu ya daladala ya Jamatini. Hapo utapata daladala za kwenda chuo cha mipango. Pia hata ukipanda daladala za msalato au veyula utashukia kituo cha mipango. Chuo kipo barabarani kabisa. Nauli ya daladala ni tsh 300 na tax ni sh 6000. Ni bora uondoke ar trh 11, maana safar ni safar, hujui ya njiani. Guest jiran na mipango zipo ndio.
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuna mabasi ya Arusha -Dodoma direct kama Abood, Hood na mengine ni safari ya siku moja ukiondoka AR saa 12 mkienda vizuri bila tatizo unawez kufika Dodoma same Day saa 3 au 4 usiku. Dodoma mjini guest kibao usihofu. Alternatively, kuna mabasi ya Arusha -Dodoma kupitia Babati na Kondoa nayo huondoka AR muda huo lakini yenyewe hufika mapema zaidi maana njia ni fupi zaidi. Ukipanda haya huna haja ya kufika Dodoma mjini maana basi linapita hapo hapo nje ya chuo ni suala tu la kuwaeleza wahusika wa basi wakuteremshe hapo. Ukiongeza na maelekezo ya Kaumza hapo juu utafika Chuo cha Mipango. Bon Voyage!
   
 4. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Hongereni sana kwa maelezo mazuri mliyompa Huyo jamaa, kwa kuongezea tu Kama yeye ni mvulana na usiku baada ya usaili akipenda kupumzika na kupata mrembo aende maeneo ya Chako ni Chako atapata mrembo
   
 5. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Nasikitika sana kuchelewa kujiunga na Jamvi yaani najuta kuchelewa kulijua. Nashukuru sana bwana mkubwa, sasa najisikia nimekuwa mwenyeji wa Dom
   
 6. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Sajenti, hiyo salute hapo kwenye picha ni yako mkuu. Nashukuru sana. Kiukweli ushauri wenu umenifaa sana. Nimeelewa maana ya Bon Voyage.... so nashukuru sana. Nimeshindwa kukujibu kwa lugha hiyohiyo
   
 7. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  :busu:busu:busu Tehe teheeeee! Nafurahi kweli, mimi ni kidume kweli na nadhani kwa namna hiyo ntapunguza stress za usaili au ntajipongeza kwa kufanya vizuri. Mimi ndo ntaamua kusuka au kunyoa. Hata kama kuna msichana ataenda naye apeleke bidhaa hapo chako ni chako(ni ushauri tu)
   
 8. Mimley Mahela

  Mimley Mahela Member

  #8
  Mar 19, 2016
  Joined: Mar 16, 2016
  Messages: 16
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Jamani samahanini me ni mwanafunzi nimemaliza kidato cha nne na nimepata dvtin three ya 25 na sihitaji kwenda advance n napenda kwenda chuo lakini vyo vyenyewe napendelea kiwe udom au mipango naomba ushauri nikasomee couz gani ila nilisoma biadhara so nina d ya bkepng na comerce pamoja na c ya history, language na kiswahili pleas naombeni ushauri wenu
   
 9. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2016
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Mbona unaandika mwandiko mbaya,wewe umemaliza form four kweli????
   
 10. Mimley Mahela

  Mimley Mahela Member

  #10
  Mar 21, 2016
  Joined: Mar 16, 2016
  Messages: 16
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  kaka angu huo si ushaury mbona waanza leta majungu
   
 11. Hamiyungu

  Hamiyungu JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2016
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 342
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 60
  Ndio maana umefeli,kwa huo mwandiko walimu walipata shida sana.jaribu wewe kusoma ulichokiandika hapo juu.
   
 12. Mimley Mahela

  Mimley Mahela Member

  #12
  Jun 11, 2016
  Joined: Mar 16, 2016
  Messages: 16
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Hayo so maisha KAKA usidharau usiyemjua
   
 13. f

  fokonola bokoyoka JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2016
  Joined: Feb 13, 2015
  Messages: 571
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 80
  Sasa usipande abood au hood hizi zinapita morogoro na ni mbali, kata tiketi ya arusha express yanafika Dodona SAA 9 alasiri au saa nane mchana, inapita bahati, singida then Dodoma, stendi ya mkoa Dodoma na ya vifodi zipo umbali wa mita chache sana, panda vifodi vya st gema utashukia kituo cha mipango. By saa 10 jioni utakuwa mipango. Vyumba vipo vingi pale maeneo ya kanisani.
   
Loading...