Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,829
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni). Mradi huo uliopo Kigamboni, Dar unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba leo Septemba 25, 2023 amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.
Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.