NSSF yashinda tena 77

Unajua ile ripoti ya rushwa Tanzania iliyotolewa na PCCB inasema kuwa NSSF na hao PCCB wenyewe ndio least corrupt

inamaana Ikulu, CHADEMA, jesho la polisi, PPF, TRA, BIMA CCM na hata JF kuna rusha KASORO nssf na PCCB

Kwa hiyo NSSF inazizdi taasisi nyingine kwa kutokuwa na rushwa au tuseme kiwangao cha Rushwa NSFF ni cha kiwango cha chini kabisa tofauti na tasisi nyingine? haya tuendeleee kuwapongeza kwa kweli lakiniiiiiii................

Ni rushwa aina gani hiyo unayoshindanisha Polisi na NSSF. Core services business bjectives zikiwa tofauti ina maana hata rushwa inatakiwa ipimwe kwa vigezo, vyanzo na viashiria tofauti tofauti...... Au sio

Huwezi kupima rushwa ya hospitali ukalinganisha kwa vigezo hivyo hivyo na Rushwa ya Benki. Kwa haraka hara mtu unaweza kusema Hospitali ya mwananyamala ni more crrupt kuliko Benki ya NMB. lakini......

So Bora walinganishe mashirika yanaytoa huduma sawa la sivyo tutapenda kuona uchambuzi unachambua detail zaidi wich may prove otherwise
 
inamaana kulikuwa na ulazima wa kuvaa kiswahili namna hii?<BR><BR><IMG border=0 alt="" src="http://3.bp.blogspot.com/-ikOcJYGQQYY/Tg4AmxrjymI/AAAAAAABBAQ/lTF2SsDiwFw/s1600/8.JPG">
<BR><BR>

Sijui Dr Ramadhani Kitwana Dau angevaaje ili aonekane kavaa sawasawa. Labda ningeuliza inakatazwa kuvaa Kiswahili?
Picha nikiiangalia sioni kasoro yoyote. Dr Dau kavaa kofia ya mkono, juu katia koti chini ya koti kavaa kanzu ya dariz.
Kwa hakika kabisa hayo ni mavazi yetu watu wa pwani na kama ukipenda ni mavazi yanayomnasibisha mvaaji na Uislam.

Sasa sijui kiinachokera ni nini Uswahili au ni Uislam katika vazi alilovaa Dr Dau?

Mie sipati tabu kumuona mtu kavaa suti ya vipande vitatu na tai. Kama ilivyo kanzu, koti na kofia na suti ya vipande vitatu zote
hizo ni lebasi zinazokubalika kisheria kuvaliwa kama nguo za heshima ambazo mtu anaweza kuvaa katika shughuli yoyote ya kiserikali.

Hivi kweli inashangaza nini mtu kama Dau, Mswahili wa Kidaresalaam na Mafia kuvaa vile?

Labda ndugu yangu kwao anakotoka hawana utamaduni wa kivazi kwa hiyo kwake yeye kivazi anachokijua ni hizo suti.

Sie watu wa pwani tuna utamaduni wetu.

Zamani sisi tulipokuwa tunainukia katika miji ya pwani tukitiwa suna siku ya wali kutoka wazee wetu walikuwa wakitushonea suti na
suti hiyo ikivaliwa na kanzu na juu kichwani unapiga kilemba.

Mohamed Said
 
Back
Top Bottom