Hiyo ripoti ya shirika la NSSF ikijibu gazeti la Mwanahalisi nafikiri inapotosha. "Unqualified Report" haina uhusiano na kufilisika au kutokufilisika bali kama mahesabu yanatoa picha halisi ya shirika. Hata hivyo, naamini Mkaguzi inabidi aandike ripoti ingine kuhusu "Going Concern" (i.e uwezekano wa kufilisika au kutofilisika) ya shirika analolikagua ambayo nafikiri hiyo ripoti ni sehemu ya ripoti ya Manajementi na haihusu jinsi uwekaji wa mahesabu ulivyokuwa. Ni tofauti na "Auditor's Opinion". Sasa NSSF wanapotumia ripoti inayohusu jinsi mahesabu yao yanavyowekwa kama sababu ya kujenga hoja kuwa shirika halifilisiki, ni kupotosha umma. Watupe Management Report ya Wakaguzi.
Kama huoni kwa macho basi walau papasa! yaani hii hukuiona!
NSSF hatarini kufilisika
Kuhusu dai kuwa NSSF ipo hatarini kufilisika, hii pia si kweli. Kipimo kizuri cha uwezo wa kifedha wa mfuko (financial soundness) ni Tathmini ya Mfuko yaani Actuarial Valuation ambayo inafanywa kila baada ya miaka 3. Kwa upande wa NSSF, Actuarial Valuation ya mwisho ni ya mwaka 2010.
Zoezi hili lilifanywa na Kampuni ya xxxxxxx kutoka Canada ambayo mwaka xxxxx iliteuliwa na Shirika la Kazi Duniani yaani International Labour Organisation (ILO) kufanya Tathmini ya Shirika la NSSF. Matokeo ya Actuarial Valuation inayoishia mwaka 2010, yanaonyesha kuwa Reserve Ratio ya NSSF ni 6.8. Tafsiri ya matokeo haya ni kuwa NSSF inaweza kumudu kulipa mafao YOTE kwa wanachama na kulipa gharama ZOTE za uendeshaji kwa miaka 6.8 bila kuingiza hata senti moja kwa maana ya ukusanyaji wa michango au mapato kutokana na vitega uchumi.