Serendipity
JF-Expert Member
- Jan 24, 2009
- 486
- 43
Nilitembelea leo ofisi za NSSF Dar es salam zilizopo Ilala karibu na Amana hospital.
Wateja nilio wakuta hapo walikuwa na Khali ya Kukata Tamaa na maisha.
Malalamiko/Manung'uniko yao ni kuhusu mfuko wa NSSF kuwakatisha tamaa wanachama waliostaafu au walioacha kazi kwani Huduma zao Haziridhishi ukilinganisha na mifuko mingine.
Kero kubwa ni pale utakapoanza kufuatilia mafao yako, Madai yako hayatapokelewa mpaka usote mtaani kwa muda wa miezi sita(ni NSSF bylaw) ndipo watakukubalia ufungue madai ya mafao yako kwa mara ya kwanza.
Kero inazidi kukera maana baada ya hiyo miezi sita uliyosota mitaani bila kipato chochote, wakikubali kupokea madai yako wanakupangia tarehe ya mbali(inaweza kuzidi miezi saba) ndio waanze ku process mafao yako. Inasemekana Inaweza kuchukua zaidi ya mwaka mmoja au zaidi bila kulipwa mafao.
Kama Khali itaendelea kuwa hivi basi ni bora vijana wanaoanza ajira wajiunge na mifuko mingine ili kuepuka hii kero ya NSSF.
Mwenye uzoefu kama malalamiko hayo ni ya kweli atueleze kwa kutoa ushuhuda wake hapa jukwaani.