NSSF... Sikujua kama Shirika hili lipo hivi!!!!!

cement

JF-Expert Member
May 5, 2012
581
218
Wakuu heshima mbele

Baada ya kufanya kazi za kwa miaka kumi ss nimeamua kuacha nataka nijiajiri mwenyewe!

Nimekuwa mwanachama NSSF toka 2002 mpaka leo michango yangu ipo vizuri barua ya kuacha kazi ya mwajiri nimeshapeleka muda mrefu ss mwezi wa saba,kinachonishangaza taratibu zote nimefata lkn naambiwa eti pasu kwa pasu ss pesa nikatwe me harafu kuzitoa naambiwa nusu kwa nusu hii imekaaje!maombi ya pesa yangu yapo Ubungo Kinondoni mbona Rushwa zingine hazifai jmn??pesa yangu waikate imefika muda naihitaji masharti yanakuwa mengi.

Wadau naombeni msaada wa mawazo nichukue hatua gani?makoa makuu nimeenda nikaambiwa file liko ubungo nikifika ubungo longo longo kibaooooo!!!!
 
Mkuu pole sana, wewe komaa nao utapata tu na wala usijaribiwe kutoa rushwa.

Ila swali jingine, je wewe hiyo miaka 10 ulifanya kazi wapi? na je uliwahudumia watu vizuri?
Kama ulikuwa jeuri na mkilitimba sasa ndo ujutie ulivyowafanyia wengine na ubadilike.
 
Wasikutishe, tena komaa na waambie unawashitaki. Kwa kawaida notisi huwa ni miezi sita tu na pesa yako inakuwa tayari, tena unapewa yote lump sum, ukilegea shauri yako utaingizwa mjini au kusumbuliwa sana. Kumbuka, hizo ni pesa zako ambazo umeziweka kwa miaka yote ulipokuwa kazini, wanatakiwa kukupa michango yako yote pamoja na interest. Huendi kuomba bali kuchukua hela zako na kuhudumiwa ni haki yako si fadhili.

Ukiwa mpole ndo shauri yako, itabidi umpoze mfanyakazi mmoja ili akushughulikie.
 
Hebu nenda takokuru! Angalia nao wanaweza kuomba pasu kwa pasu maana nchi hii naona tumejenga ka-utamaduni ka-rushwa kuanzia juuuu hadi chini kabisa!
 
Inasikitisha sana maana pesa yangu manyanyaso kibao!
 
Mimi pia mwaka 2002 yalinikuta mambo kama hayo, nikawa mbishi mpaka ofisi hiyo hiyo ya Ubungo wafanyakazi wote wa kaunta wakanifahamu.

Nilichoka na mara njoo baada ya wiki mbili mara wiki moja zao, siku moja nikalianzisha, mzee mmoja aliyeonekana kuwa mzoefu nao aliniita pembeni na kunishauri akaniambia, 'kijana wasikusumbue hao nenda chumba namba fulani kuna mwanasheria wao kajieleze utasaidiwa'.

Ukweli nakwambia baada ya kumuona yule dada Mwanasheria (Mungu ambariki sanaa-Ameen) aliinua mkono wa simu akaongea nao, hutaamimi nikikuambia ndani ya wiki nikakamata mzigo wangu wote na wala sio pasu kwa pasu.

Huna haja ya kwenda Takukuru anzia hapohapo kwanza. Pole sana Mtanzania mwenzangu, ndio baadhi ya watumishi wa serikali walivyo, ukiwa mpole jasho lazima likutoke.
 
Wewe kama wanakuomba rushwa waambie sawa, nenda Takukuru watakupa njia za kufanya kuwanasa hao waomba rushwa.
 
daah kilio cha mtz hiki..pole sana..hamna kitu kama hicho mkuu komaa nao jamaa wazushi sana.
 
Thubutu! hela yangu mwenyewe niambiwe mambo ya pasu kwa pasu haki ya nani namnyonya mtu ulimi.
 
Pole sana usijaribu wala kumpa mtu yoyote rushwa.kama bado wanakusumbua ingia katika ofisi ya chief manager hapo atakusaidia.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Jamaa watu wa ajabu sana hii kauli imenishtua sana!
kama viambatanisho vyote viko sahihi hakuna sababu ya kukuzungusha, mweleze meneja wao kama na yeye haeleweki nenda makao makuu ukawaripoti. Mimi utanisumbua sehemu nyingine lakini kwenye haki yangu huwa sina mzaha kabisa.
 
Mimi NSSF Walinilipa pesa yangu yote.ila nadhani kwasasa serikali imekopa sana fedha kutoka mashirika ya hifadhi za jamii ikiwemo NSSF nadhani ndilo tatizo.nchi hii tunataabu hakuna kwa kukimbilia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom