Kwa wale waliowahi kushika aina yoyote ya uongozi wa,Jumuiya, vyama,mashirika n.k. wanaelewa vizuri jinsi tuhuma za kiajabu zinavyoundwa na kuwachafua watu bila ya kuwa ni wakosa au wahusika. Bahati mbaya tuhuma hizo huenea haraka mno na kuaminika kirahisi hadi huwa vigumu kufutika hata kama ukweli utadhihiri.
Katika kila jamii huwa kuna kundi lina uwezo wa hali ya juu kueneza habari za uzushi na zikaaminika.Ajabu ya mambo mara nyingi kundi hilo huwa ni lile “LISILOONEKANA” na hata wale wanaoshiriki huwa hawakubali kama wamo humo!!! UHATARI wa kundi hili umezidi katika ulimwengu wetu mpya wa mitandao ya kijamii.Ubaya wa kundi hili hautofautiani na ule wa waandishi wa habari ambao wengi wao hutumiwa na wamiliki wa vyombo hivyo wanaojali tu maslahi yao na kuyalinda wa udi na uvumba.
Uamuzi wa kuyaeleza haya niliupata nilipokuwa naperuzi gazeti la Dira ya Mtanzania toleo No 411 Apr 18-24/2016 lililokuwa likimzungumzia Dr.Dau kuwa anamiliki BILIONI 100 !!! pia ni mmoja wa wamiliki wa timu maarufu ya New Castle, UK!!!(Nikasoma mengi mtandaoni kuhusu Dr Dau na NSSF )
Ajabu ya mambo Dr.Dau siku ya ufunguzi wa daraja la Kigamboni, alipewa nafasi na mheshimiwa Rais JPM ambae hadi sasa amethibitisha wazi kuwa hana simile na wezi wa mali ya umma.
Ndipo hapa nilipoanza kujiuliza..ikiwa Rais kaweza kutumbua jipu la Mkurugenzi wa jiji la Dar ,Wilson Kabwe mbele ya umati wa watu na akamkaribisha Dr.Dau kuongea machache kwa kuutambua umuhimu wa Dr huyo ktk ujenzi wa daraja hilo, ina maana Rais ANAELEWA VIZURI KUWA Dr DAU SI JIPU!!!ANGEKUWA JIPU ASINGEMKARIBISHA NA WALA ASINGEMTEUA KUWA BALOZI.
Waandishi wa habari hawawezi kujua mengi kuliko Rais wetu ambaye alitoa somo zuri aliposema “MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI”
Kayu Ligopora
Athens Greece
kaygreko@yahoo.com