NSSF kumwaga mikopo Saccos kuanzia Julai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF kumwaga mikopo Saccos kuanzia Julai

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BabuK, Jun 29, 2012.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) nchini kupitia vyama vya Akiba na Mikopo (Saccos) wataanza kupata mikopo ya nyumba na masuala mengine ya maendeleo kuanzia Julai mwaka huu, ilifahamika jana.

  Ofisa Mipango Mkuu wa NSSF , Gerald Sondo alisema hayo jana alipoeleza mikakati mbalimbali ya mfuko huo katika kuboresha maisha ya wanachama.

  Sondo alisema NSSF imejipanga kuwakopesha wanachama fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zao, elimu na hata biashara na kwamba mkopo huo utapitia Saccos za wanachama mahali pa kazi.

  "Kima cha chini kuikopesha Saccos kitakuwa Sh 50 milioni, lakini cha juu kinafikia hadi Sh 1 bilioni'' alisema opfisa huyo akiwa kwenye Viwanja vya Maonyesho vya Mwalimu Nyerere maarufu kwa jina la Sabasaba mtaa wa Barabara ya Kilwa.

  Alisema maandalizi ya kuanza kutoa mikopo imekamilika na kwamba NSSF inatarajia kuanza kutoa fedha kuanzia Julai Mosi na kwamba taarifa kuhusu mpango huo zilishatyolewa kwa wadau wakati wa mkutano uliofanyika Arusha mapema mwaka huu.

  Kuhusu masuala ya riba, Sondo alisema NSSF itahakikisha inatoa riba ndogo kwa Saccos na kwamba ni martarajio yake kwamba wanachama nao watapata fedha hizo bila ya kuwa na riba kubwa kama za vyombo vingine vya fedha.

  Alitoa wito kwa wanachama NSSF kuunza Saccos mahali pa kazi na kujiwekea akiba nyingi ili waweze kukopa fedha hizo ambazo malengo ni kuwasaidia wanachama ili kuboresha maisha yao.
  Chanzo: Mwananchi
   
 2. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Nauliza ivi hiyo mikopo itakuwa na riba? Na kama ndio kwanini wanitoze riba kwenye pesa niliyovujia jasho?
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  itabidi JE SACCOS nao wapeleke maombi kama kuna memba wenu ambaye ni memba NSSF..
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni mpango mzuri kwa kuanzia kwni hizo fedha zetu tumekuwa tukizililia siku nyingi ili ziweze kutunufaisha.
  Ningewashauri wafikirie na kuweka utaratibu wa kuwakopesha wanachama mmoja mmoja (individually) kwakuwa si maeneo yote ya kazi yana saccos na mahali pengine zipo lakini si endelevu.
   
 5. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kama nimisoma vizuri wanalenga SACCOS za mahala a kazi.. JE ni muunganiko wa watu wenye fani mbalimbali na inasimama yenyewe.... welwdi watusaidie katika hili..
   
 6. F

  FemaraFe Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  buy famvir uk is an anti-viral medication which after transformation in human organism turns into penciclovir which is active against such viruses as Herpes simplex (types I and II), Varicella zoster, and the Epstein-Barr virus (EBV). Penciclovir penetrates into the cells infected by virus where being subjected to treatment by viral ferments it turns into penciclovir-triphosphate which inhibits replication of viral DNA. The medication has not effect on the non-infected cells. buy famciclovir no prescription is active against certain strains of Herpes simplex with changed DNA polymerase which are resistant to Acyclovir (Zovirax). [​IMG]
   
Loading...