NSSF & daraja la Kigamboni: Q&A

Mtoa mada anatafuta majibu kama haya yafuatayo kutoka makao makuu yake. "Mchakato unaendelea, zabuni zitatangazwa hivi karibuni, upembuzi yakinifu utafanyika baada ya hapo. Kisha mtaalamu mwelekezi atatafutwa, zabuni zitafunguliwa hivi karibuni, kutakuwa na "short list", tutakaribisha wabia wa maendeleo watuunge mkono, tuombe "no objection Benki ya Dunia etc. Zoezi zima linaweza kuchukuwa karne moja mpaka daraja likamilike! Nakumbuka daraja la Mkapa na hivi sasa Malagarasi!
 
Join Date : 17th March 2011

Posts : 21
Rep Power : 0
Katumwa aje afanye research maana humu kuna vichwa, naona maswali yamemshinda na msiingwizwe mkenge na huyo Mr. NSSF hana lolote.
 
Mr NSSF (Nina Sepa Sisemei kwenye Forum yenu) hata kuuliza sitaki jibu kwanza hayo kama utazaliwa upya maana inonekana umekata kamba
 
naomba hii irudishwe siasa kisha iwe merged na ile za video za Dr Dau TBC
 
Mengi yanasemwa na inavyoonekana ni kuwa wengi pia wana maswali zaidi sasa naomba mlio na maswali yenu (Kuhusu Daraja la kigamboni tuu) leteni nami nitajitahidi kuwajibu na kuwaweka sawa kwa kadri ya uwezo wangu. Pale ambapo nitakuwa sina data za papo kwa hapo basi nitaomba muda ili nizilete.

Natumai tutakuwa na mjadala wenye mtiriko mzuri na wa heshma.

Akhasanteni.
Hizo ajira vipi? Tupeleke wapi 'cv' zetu? Au ndio zinagaiwa kiukoo kichinachina?
 
Mengi yanasemwa na inavyoonekana ni kuwa wengi pia wana maswali zaidi sasa naomba mlio na maswali yenu (Kuhusu Daraja la kigamboni tuu) leteni nami nitajitahidi kuwajibu na kuwaweka sawa kwa kadri ya uwezo wangu. Pale ambapo nitakuwa sina data za papo kwa hapo basi nitaomba muda ili nizilete.

Natumai tutakuwa na mjadala wenye mtiriko mzuri na wa heshma.

Akhasanteni.
Baada ya daraja kinachofuata nini watu kutathminiwa nyumba zao wapewe chao wasepe au? hichi kidaraja ni kwa ajili ya kile kimradi cha new city?
 
Nimefurahishwa sana na mradi huu, lakini serikali pia ingejali marekebisho ya reli zetu kwani beneficiaries ni wengi sana wa reli, ukilinganisha na vipaumbele kama hilo daraja ambalo limepewa kipau mbele wakati wakazi wa kigamboni huwezi kulinganisha na wahitaji wa reli ambao wanatoka Moro, Dom, Tabora, Kigoma, Mpanda Shinyanga na Mwanza. Bado jambo hili linaniumiza kichwa
 
Sasa daraja linajengwa JF? Badala ya kuhangaika na kujenga daraja unakuja kutafuta maswali humu, ili iweje?

Kajenge kwanza, ondoa huu uharo!
 
nipeni tenda ya kusambaza cement hapo, japo kwa nguzo moja tu basi.
 
Back
Top Bottom