NSSF-ARUSHA...Sitanyamazia Hili...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF-ARUSHA...Sitanyamazia Hili...!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PakaJimmy, Nov 18, 2009.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ndugu Wana-JF,

  Huenda nikaenda kwenye lugha yenye extremes kwenye hii thread, maana tayari adrenalin level yangu ishapandishwa na watu wa Ofisi tajwa hapo juu.

  Ofisi ya NSSF hapa Arusha ina matatizo yaliyobobea.

  Kwanza unapoingia tu hapa ENISISIEFU utadhani umefika msibani, maana kwa kawaida watu waliofiwa utawajua tu kwa sura zao!..Ni nyuso za huzuni tupu. Nilifanikiwa kuwepo katika Ofisi hiyo kwa Lisaa limoja, lakini sikufanikiwa kuona CHEKO la mteja yeyote...ni kila mtu anaeleza anavyoteseka!

  Baada ya kujiunga kwenye foleni nilisikia mama mmoja akiongea kwa hasira.."Basi mtupe kazi za kufanya hapa, maana tunashinda hapa miezi, toka asubuhi mpaka jioni na hakuna kinachoendelea"!

  Ukianzia counter ya mapokezi unakutana na mama mmoja ambaye nadhani ni kutokana na kauli zake ndo aliwekwa pale...Amevaa sura ya Mbuzi, na anaongea kwa kero ajabu.


  Ukutani wamebandika makaratasi yanayoeleza uzuri wa huduma zao, ambapo when you go to reality, all the shit is a white elephant, Kimaasai tunasema "Meti-Onyo!

  Ukitoka hapo unakutana na vibao vyenye vyeo vizuri ajabu..eti "SENIOR BENEFITS OFFICERS"...sijui "TECHNICAL naninani huko"...etc.
  Lakini jaribu kuwafuata hao Oficcers, unakumbana na kero za kutisha huko.

  Mafaili yametupwa chini ovyo na mengine yamefungwa kamba za kudu utasema mitumba!..sijui ni utaratibu gani wa filing wanaoutumia pale, maana hata mtoto wa miaka 17 aliyesoma Office Practise pale KIMAHAMA Centre hatakuwa careless vile!

  Mbaya zaidi ulizia faili lako, watahangaika kulitafuta hadi unasahau shida iliyokupeleka, na unaanza kuwaonea huruma tena!...In short there is not a single filing system or order in use there.

  Kila ukienda wanakuwa hawajui kabisa faili liko wapi.Wanaishia kulikosa kabisa, na kukuandikia tarehe ya kurudi tena kwenye kikaratasi, ambapo hawarekodi popote hiyo tarehe, na utakaporudi unaanza na square-one!..too boring!

  Unakuta wanazunguka tuu, toka mlango huu kwenda mwingine, wanagongana tu makoridoni, wanaangalia saa na muda, na kubip watu kwa simu...kweli mwenye hasira asisogee zile ofisi, atapata kesi buure!

  Meneja wa Tawi hili bwana Mwakatobe nadhani hajachukua initiative yoyote kuangalia dhiki wanayopata wateja pale. Anawasikiliza wale wanaopata access ya kuingia Ofisini kwake tu!

  Suggestion box lililopo hapo ofisini limepigwa vumbi ajabu, nadhani lina miaka kadha halijafunguliwa na mtu!

  Inasikitisha sana kwa watu wasomi kama hawa kufanya huduma za stone-age-era kwa wateja miaka hii ya competition, wakati wamekaa na makompyuta makubwa mezani, na nje kwenye yadi wamepaki magari ya hela mingi ajabu!

  Kama wakubwa wenu watapita hapa JF, nawaomba wagharamie kidogo tu kuleta mkufunzi wa Mada rahisi ya Customer Care hapo ofisini, huenda hawa watu watabadilika, japo kwa kiasi cha chini kabisa...huh!

  Nawasilisha, at least hasira zimenishuka baada ya kuweka hazarani...!
   
 2. M

  Matumaini Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Nilikuwepo hapo juzi juzi tu kwa shida fulani...yote uliyosema ni KWELI TUPU....Its like visiting an old abandoned store where old files are kept...
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bora kama umeona...Hawa wafanyakazi wanasahau kabisa kwamba wanahudumua watu wa kila aina pale!..

  Wanadhani wote ni wastaafu, hawajui kwamba wengine tumetoka fasta maofisini na kwenda kufuatilia mambo pale, wanabaki kuuza sura tu... Hivi lidandansi ziliendaga wapi?
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160

  PJ, hoja nzuri sana na for sure itamsaidia Mwkaobe kifungua macho!!! Lakini huoni hilo la cheni limekaa kaudaku?
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima Kwako PJ

  Jumatatu nilikuwa NSSF kwaajili ya kufuatilia vitambulisho vya wafanyakazi baada ya NSSF kulazimisha wafanyakazi wote kujiunga tangu mwezi february 2009.Kila nikifuatilia napewa sababu za hovyo mara ohoo cards zinatengenezwa Afrika kusini njoo mwezi ujao,wafanyakazi wameshakatwa michango yao kwa miezi kumi bila kupewa vitambulisho ambavyo ni muhimu kwao kwaajili ya huduma mbali mbali wanazotoa NSSF.

  NSSF Arusha wamekithiri kwa uzembe uliopitiliza.
   
 6. A

  AM_07 Member

  #6
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  yes, NSSF arusha wanasikitisha, kila mfanyakazi unaekutana nae utadhani mligombana jana jioni, real wanakuona kama kero wakati mchango wangu ndio mshahara wao,ila kwa ujumla hospitality watanzania wengi inatupiga chenga, iwill put it as a fresh tipoc ila kwa lkweli tutanyanganywa kazi zetu hata za uhausgell
   
 7. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Kuna baadhi ya wafanyakazi wanashirikiana na waajiri kuwibia wafanyakazi. Utakuta mwajiri wako hapeleki michango kila mwezi, anaweza kukaa hata mwaka mzima, na anapopeleka halipi faini inayopaswa kulipwa. Ukiwafuata hao wafanyakazi kuwauliza kwanini mmajiri haleti michango, wanakujibu kijeuri, "Ulikuwa wapi siku zote usifuatilie" "Tutawasiliana naye" na mengine mengi.
  Mbaya zaidi ni pale muda wao wa lunch unapofika, wanachukua zaidi ya masaa matatu na wanaporudi ofisini wanajivuta sana na mwisho wanakupa tarehee ya kurudi
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  This is a very serious allegation kwa ndugu yangu Mwakatobe... sijui ndio kummaliza kabisa au vipi!!?
   
 9. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Haya yasemwayo hapa kama ni kweli, ndugu yangu Mwakatobe ofisi hana.
  Na kama anafahamu haya na ameshindwa kuongoza njia ipasayo, naamini huu utakuwa wakati sahihi wa kutafuta ofisi nyingine kwani hali ni mbaya!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuna watu wananiambia ni mpaka uwakatie kitu kidogo ndo wanakushughulikia fasta, but i dont want to believe it fast, coz i want to prove it for myself. Sitatoa hata mia, na naandika kila nikipewa tarehe ya kurudi.

  Mwishoni nitakuja kuwaeleza kuwa inagharimu miezi mingapi kwa mtu ambaye amefanyia kazi hapahapa Arusha(yaani faili lake halihitaji transffering yoyote ya Dar au wapiwapi), na michango yake yote iko sahihi!

  Inaboa but i think iam learning a very new xperience with these Alien-workers here!..Nitakuja kutoa kwenu dossier ya kutosha mwisho wa project yangu.

  Tuombe Mungu!
   
 11. s

  sombyo Member

  #11
  Nov 19, 2009
  Joined: Nov 19, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili tatizo lipo na uongozi wa juu unalifanyia kazi. Tumuache Mwakatobe na chain yake kwani haina uhusiano na utendji mbovu wa staff wa benefit section. Vinginevyo ujumbe umefika
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nashukuru sana Mkuu Sombyo.

  For the sake of that (red), mi na`edit mahala hapo nilipoenda extremes, maana kweli umeonyesha ustaarabu sana, nimekuwa convinced kwamba yamefika, na kwamba something is going to be done soon.

  Big-up Mkuu, na tafadhali sana tusaidiane kukemea hii hali, maana tunateseka sana, kiasi kwamba wastaafu wanajuta kuwa watumishi siku zao.

  Mshaurini Meneja ajaribu kuvaa viatu vyetu, au la atumie njia ya kumtuma ghost client aone huyo mtu atakavyotendewa...atashangaa na roho yake Mkuu!

  We remain anxious and time will tell.
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Mkuu Sombyo Heshima kwako.

  Kwanza karibu jamvini.

  Nashukuru kama uongozi wa juu unalifanyia kazi kwasababu NSSF Arusha si kwamba imekuwa ni kero ya miaka mingi lakini imewafanya hata baadhi ya wanachama kufikiria njia mbadala.

  Mwakatobe ana miaka mingi pale NSSF sijui ni kwanini amekubali kuacha mambo yaaribike kiasi kwamba mfanyakazi akikwambia anakwenda pale inabidi apatiwe ruksa ya siku nzima.Nadhani ni vyema ikiwa Bwana Mwakatobe atapangiwa kituo kingine cha kazi hasa wilayani kituo cha Arusha ni kikubwa sana kwake.

  Unaweza kushangaa sana muda wa mchana wafanyakazi wa NSSF wanakwenda kula Picnic bar ambayo iko mbali sana na kituo cha kazi,ni kwanini hawaendi kula Green hut au hotel nyingine yoyote iliyo karibu na ofisi yao ?.
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Poleni sana wanachama wa NSSF. meneja na wafanyakazi wote wa tawi hilo wawajibike kimajukumu.
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu hakuna aliyepoa kati ya wateja wote, maana tunaendelea kunyanyasika.

  Kuhusu kuwajibika, wao wenyewe ni watu wazima, na nadhani waliapa kuwatumikia wateja ipasavyo, hivyo watajihukumu wenyewe!

  Halafu kuna hii hali ya kuwaambia wateja..."tungekuandikia cheki...lakini kwasasa hakuna hela kabisa benki, kwahiyo nenda endelea kusubiri, labda jaribu wiki ijayo..."

  Mi sielewi inamaanisha nini! Yani vituko ni vingi hapa nyie...!
   
 16. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  KERO KERO KERO, PJ you have said it all, hapo kwenye red utawaamini vipi na kila mwezi wanachama karibia how many thousands wanachangia, wangekuja na gia nyingine sio hiyo.
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  But this time something must be done to sieve out these mediocres.
   
 18. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  wanahitaji mafunzo ya jinsi ya kuwajali wateja wao
   
 19. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  wanahitaji mafunzo ya jinsi ya kuwajali wateja wao
   
 20. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Duuuuu kweli ni sooo au jamaa anafukuzia chapaa tu anasahau kibarua chake na kuwa serious kazi???
   
Loading...