NSN sasa kuendesha shughuli za Vodacom

PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
57
NSN sasa kuendesha shughuli za Vodacom Send to a friend
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imekubaliana na kampuni ya Nokia Siemens Networks (NSN) ili NSN itoe huduma za mtandao kwa niaba ya Vodacom Tanzania.

Chini ya makubaliano hayo, kampuni ya NSN itaendelea kuboresha na kuuendesha mtandao wa Vodacom kwa miaka mitano ijayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare, aliwaambia waandishi wa Habari Jijini Jana kwamba wafanyakazi wa Vodacom watahamishiwa kampuni ya NSN.

Mkurugenzi huyo alisema wafanyakazi hao watakao hamishwa watapata fursa ya kuongeza utaalamu zaidi ndani ya NSN.

Alisema njia hiyo ya uendeshaji si mpya na kwamba Vodacom Tanzania itandelea kutafuta njia bora zaidi za uendeshaji ili kuboresha huduma kwa wateja.

“Uwezo wa kampuni ya NSN wa kuendesha huduma za ki-mtandao ni mkubwa na utaiwezesha Vodacom Tanzania kuboresha huduma zake za mtandao na hatimaye kuboresha huduma zetu kwa wateja,” alisema.

Kutokana na makubaliano hayo NSN itachukua majukumu yote ya mawasiliano ya mtandao pamoja na yale ya mtandao katika kanda za mbalimbali nchini.

Uzoefu wa Nokia Siemens Networks kimataifa utaiwezesha Vodacom Tanzania kufikia malengo yake ya ubora wa mitandao ubora wa huduma kwa mteja na unafuu wa gharama.

NSN ni waendeshaji wakubwa wa huduma za mitandao Duniani ikiwa na inaendesha vituo vya mitandao 830,000 Duniani kote ikiwa na mikataba 222 ya uendeshaji. Vodacom ina vituo 1,000 vya mawasiliano nchi nzima.
 
Hivi hii ndiyo inaitwa "Outsourcing"?

Nadhani tafsiri ya Kiswahili si sahihi

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare, aliwaambia waandishi wa Habari Jijini Jana kwamba wafanyakazi wa Vodacom watahamishiwa kampuni ya NSN.

Mkurugenzi huyo alisema wafanyakazi hao watakao hamishwa watapata fursa ya kuongeza utaalamu zaidi ndani ya NSN.

Nadhani hapa ni baadhi ya "vitengo" ndivyo vitavyokuwa chni ya NSN!

NSN si wataalamu wa HUDUMA KWA WATEJA including KUUZA VOCHA!
 
Nafikiri ni wahandisi tu ndio wanahamia NSN....kuna rafiki zetu kule ngoja tuwaulize watujuze...nasikia airtel walishajiunga NSN siku nyingi...
 
ni wahandisi tu wamehamishiwa NSN, customer care EUROLINK, sales AFRIKINGS + more to come
 
hii habari sio nzuri when it comes to "competitive labor market" kwani kumbuka pia kitengo cha operations cha Zain (Airtel) pia kilichukuliwa na NSN mwanzoni mwa mwaka jana na hii iwanafanya telecom engineers wengi ambao wapo Vodacom na Airtel kuwa na options chache za kukimbilia yaani Tigo na Zantel tu.

Hivi kuna sheria yoyote ambayo TCRA wanayo kuhusiana na kuregulate these "outsourcing" deals?
 
Sidhani kama TCRA wanaweza kuyapangia makampuni ya simu whether to outsource or not to....
 
Unajua kila mfanyabiashara anatafuta namna ya ku operate competitively, na ni haki yake kufanya hivyo hata akiamua kuuza kampuni yote.

Mi naona this move is just ok, labour market itazidi kuwa competitive na as a result more opportunities will be created. Kumbuka its during the hard times ndipo ambapo ubunifu unatamalaki! Though I understand in the short run, watu wata suffer kiaina!!

All the best all the affected people!!
 
Sidhani kama TCRA wanaweza kuyapangia makampuni ya simu whether to outsource or not to....

Penye mkondo wa hela unafikiri kuna sheria inaapply hapa tanzania? hakuna cha TCRA, wala cha DOWANS, nchi ipo utumwani!
kuna fununu kuwa hawa NSN wamewagomewa na vodacom south africa, lakini hapa bongo wamepamia, shamba la bibi! kwani sheria zipo au urojo kama kawa!
 
erolink waliochukua customer care ni bure mtu aliyekuwa analipwa laki saba na nusu na voda kwa kazi hiyohiyo wao wanamlipa laki tatu na ishirini no airtime kwa mwezi no matibabu kila kitu wameua. wana applications kibao za watu mpaka ukitaka kupta nafasi wanakukamua kilo mbili kwanza.
 
Good move. As a telecommunications Engineer and a veteran (Yes, a real sense veteran) and a retiree with 16 Years of telecommunications experience in Canada and over 18 Years in different countries of the world, without forgetting, as a prestigious former student of Bell Northern Research, Bellevue. (Toronto) (where digital began) and former employee of Northern Telecom, Middle East and Africa based in Maidenhead UK. Its a great move.

That is Zomba!
 
hii habari sio nzuri when it comes to "competitive labor market" kwani kumbuka pia kitengo cha operations cha Zain (Airtel) pia kilichukuliwa na NSN mwanzoni mwa mwaka jana na hii iwanafanya telecom engineers wengi ambao wapo Vodacom na Airtel kuwa na options chache za kukimbilia yaani Tigo na Zantel tu.

Hivi kuna sheria yoyote ambayo TCRA wanayo kuhusiana na kuregulate these "outsourcing" deals?

TIGO same thing Customer Care imekuwa outsourced kwa jamaa waliopiga hela EPA(Johnson Lukaza) pia wahandisi nao kuna kampuni ambayo imekuwa outsourced kwa ajili yao ila sio NSN kwa Zantel kitengo cha Customer Care kilikuwa njia kuwa outsourced kwa hao jamaa wa EPA pia sijui wamefikia wapi sina uhakika
 
good move. As a telecommunications engineer and a veteran (yes, a real sense veteran) and a retiree with 16 years of telecommunications experience in canada and over 18 years in different countries of the world, without forgetting, as a prestigious former student of bell northern research, bellevue. (toronto) (where digital began) and former employee of northern telecom, middle east and africa based in maidenhead uk. Its a great move.

That is zomba!

mmmhhh!? hapa kwenye bold ndipo panaponipa shida mimi!
 
Back
Top Bottom