Hii habari pamoja na kwamba mimi ni mshabiki wa Simba naona itakuwa na ukweli, na kama ina ukweli wowote inabidi wahusika wawe responsible na Takukuru wafanye kazi yao, wote anayetoa na anayepokea rushwa wote wametenda makosa na lazima washitakiwe kwa mujibu wa sheria.
Kuna siku niliwahi kusema humu kwamba Kaburu ni tatizo pale Simba na ninahisi hata huu mgogoro itakuwa kazidiwa kete kwenye kumuuza Okwi na ashaona dalili sasa kwamba wanachama wamemshitukia ndo maana ameamua kujiuzulu, yule jamaa ndo anayekuza mgogoro Simba, ndo aliyekorofishana na Matola mpaka Matola kaiacha timu B. Kuna watu hawamtaki Rage lakini Rage ni nafuu mara mia kuliko huyu jamaa. Kaburu nenda kabisa na usirudi tena kuja kuwa kiongozi wa Simba.