NRM yataka Museveni aongoze miaka saba

NRM yataka Museveni aongoze miaka saba

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Shinikizo hilo la kutaka rais awe akiongoza kwa vipindi viwili vya miaka saba badala ya miaka mitano limepingwa na viongozi wa upinzani ambao wamesema ni njama ya Yoweri Museveni kuongoza hadi kifo.

pic+Museveni.jpg


Kampala. Chama tawala nchini Uganda, National Resistance Movement (NRM) kinashinikiza kuwe na kura ya uamuzi ambayo itaongeza kipindi cha utawala wa Rais Yoweri Museveni hadi mwaka 2035.

Shinikizo hili la kutaka rais awe akiongoza kwa vipindi viwili vya miaka saba badala ya miaka mitano limepingwa na viongozi wa upinzani ambao wamesema ni njama ya kufanya rais huyo aongoze hadi kifo.

Msemaji wa NRM, Rogers Mulindwa amesema lazima kura ya uamuzi ifanywe mwaka 2018. Desemba 2017, Bunge liliondoa sehemu ya sheria iliyozuia watu wenye umri wa miaka 75 na zaidi kugombea urais.

Rais Museveni mwenye miaka 73 ameongoza taifa hilo tangu mwaka 1986 na sasa amekubaliwa kugombea tena wadhifa huo mara mbili baada ya kipindi chake kukamilika mwaka 2021.

Museveni, miongoni mwa viongozi Afrika ambao wametawala kwa muda mrefu zaidi, pia ni mmoja wa viongozi wa mataifa ya Afrika ambao wamekuwa wakijitahidi kubakia madarakani kwa kubadilisha Katiba.

Kutokana na wabunge wa Uganda kubadili sheria ili wawe wakiongoza kwa miaka saba badala ya mitano, chama tawala kinasema kipindi cha uongozi wa rais pia kinafaa kuongezwa hadi miaka saba ili kuwe na uwiano katika chaguzi zote.

Shinikizo la kuandaa kura ya uamuzi linakabiliwa na pingamizi la kisheria kutoka kwa wanaharakati na baadhi ya viongozi wa upinzani ambao wanasema linakiuka Katiba.

Ingawa Rais Museveni amewahi kukaririwa akieleza anavyochukizwa na viongozi wa Afrika wanaotaka kubaki madarakani kwa muda mrefu kupita kiasi, amekuwa akijitetea kwamba alimaanisha wale wanaotawala bila kuchaguliwa na wananchi.
 
Namheshimu na kumkubali sana Rais Mzee Museveni hasa nikikumbuka jinsi Yeye na wale Wapiganaji wenzake 26 waliopambana na Uongozi mbovu uliokuwepo Uganda kipindi hiko hadi hatimaye mwaka 1986 akachukuwa Uongozi mpaka leo na kuweza kuifanyia mengi mazuri Uganda. Ila nadhani sasa imetosha Kwake kuendelea Kuwaongoza Uganda na badala yake awaachie wengine waongoze ili Uganda iendelee kuwa ' Pearl of Africa ' kweli.
 
"Uongozi mbovu uliyokuwepo wakati huo", japo kwa sasa na wa kwake ni mbovu labda zaidi ya ilivyokuwa kipindi ananyakua madaraka.

Ni wazi ktk mikutano yao hawa watu hawanaga agenda yoyote ya maendeleo wanayoongea tofauti na hayo ya kujiongezea mihula.

These people are really bogus and are the main reason behind African countries being referred to as Shithole Countries. They're liabilities to this impoverished continent.
 
Back
Top Bottom