Chabruma, NRM katika maana ya vyama vya siasa, ni chama cha siasa. Pengine kwa muundo haitafanana na CCM lakini bado haiiondolei sifa ya kuwa chama cha siasa. Hata CCM haifanani ki muundo na Democrat au Republican vya Marekani; na labour au conservative vya Uingereza, lakini hauwezi kusema hivi ni vyama vya siasa zaidi ya vingine.Kwani NRM ni chama cha siasa? Acha upunguani wewe. Unakumbuka mara ya mwisho wamefanya uchaguzi lini? Unajua pia ni tangu lini Museveni amekuwa kiongozi wa NRM
Tatizo la vyama vyetu vya siasa Afrika, ni uongozi kung'ang'ania madarakani na kudhani kuwa bila wao hakuna chama au Serikali. Mh. Kaguta Mseveni ni muumini wa hili. Mbabazi alikuwa mtu wake wa karibu sana, na sasa kwa hisia tu (na hata kama ni ukweli) kwamba anataka kumuondoa kwenye urais ambao ameufanya kama ufalme. Akisikia tetesi tu wewe ni adui.
Tofauti njema iliyopo katika hili kwa CCM na Serikali ya Tanzania kwa ujumla inalala hapa kwenye kubadilisha uongozi. Baada ya uongozi wa kwanza wa mwalimu Nyerere, tuliweka utaratibu mzuri tunaouheshimu na kuufuata, wa kubadilisha viongozi. Huko kwingine sivyo ilivyo na inaonekana huko Uganda na hata Zimbabwe.