NOTION: Bongo Muvi inafeli wapi?? Warekebishe nini?

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Assalam aleykum,
Nimeona thread moja ambayo imetoa utani nikashawishika kuandika hii in a serious manner kidogo.

Kabla ya kuendelea nianze kwa kutoa ONYO: Haya ni mawazo yangu binafsi kwa kadri ninavyoamini na kuelewa kwanini sekta ya filamu za kitanzania inayumba na wachukue hatua zipi.. Kwa maana hio hii sio taarifa ya tafiti bali ni maoni ya mtu binafsi, yanaweza kuwa na ukweli au la.

Kwanza ili tuweze kuelewana ni maombi yangu uweke pembeni kile unachokiamini mpaka utakapomaliza kusoma huu uzi ndio ulinganishe mizani... Nitajitahidi iwe fupi maana sisi wa-Tanzania ni wavivu wa kusoma hasa maneno yakiwa rundo bila ya picha!! 😂😂

Ni utani tu ndugu, embu tuwemo sasa;

Ni ukweli usiopingika sekta ya filamu nchini imeyumba ukilinganisha na miaka ya hapo nyuma kidogo, haswa kipindi cha uhai wa moja ya nguli kuwahi kutokea kwenye historia ya sekta hii nchini. You guessed it, hapa namuongelea Steven Charles Kanumba (Pumzika kwa amani.) Nyote ni mashahidi na haihitaji maelezo yeyote mtu kujua filamu zilikua katika ubora wake kwa kiasi gani enzi hizo.

Labda nikupe mfano mdogo, enzi hizo tuliona collabo na wasanii wakubwa wa nje ya nchi. Tuzo zikiletwa kutokea mataifa mengine kuja Bongo.. Vipaji vipya vikitambulishwa leo na kila siku na kadhalika.

Siku hizi haya mambo yote hayapo tena na jambo baya ni kwamba wasanii wanajifanya hawaoni hichi kitu - sheer self-deception. Mbaya sana, ni kama unajipeleka kwenye chaka la simba kwa kujua na unasema huyo ni mbuzi. Very dangerous!! Ndio kitu wanachofanya Bongo Muvi!! Wanaukataa ukweli na upo wazi!!

Mambo ni mengi muda ni mchache sana. Lawama hazijengi isipokuwa kurekebisha makosa na kurekebisa kosa inahitaji mmoja ayajue makosa yake. Basi nianze na hizi nadharia ambazo nahisi ni makosa kwa fasta fasta:

1.Nadharia namba moja ni Teknolojia. Pamoja na kuwa na faida kibao kwenye sekta pia imeleta madhara; Inasemekana miaka ya nyuma kidogo filamu za kibongo ziliuza kwa sababu watu hawakua na access ya muvi za nje kwa hivo kuburudika iliwalazimu wanunue za nyumbani tu ndio maana filamu zetu zikapata ukubwa. Msinielewe vibaya sina maana wafungie muvi za nje!

Kwa wanaokumbuka; Bongo muvi waliwahi kuandamana muvi za nje zipigwe marufuku. Haha.. Mawazo finyu sana!! Ina maana hawakujiweka nafasi ya kwamba siku moja muvi zao zitakuwa kubwa kiasi cha kutakiwa kufikia mataifa mengine?? Na njia walioitumia kufungia muvi za wenzao ingeweza kutokea kwao maana watu wanaona na wanakumbuka. Ni kweli hiki ni chanzo lakini teknolojia hupigwa na teknolojia sio maandamano! Ni kikwazo ila wakigeuze fursa.

2. Uandishi mbovu: Engo muhimu sana hii!! Filamu inaanzia kwenye utunzi/uandishi. Kama huku pakiwa pabovu ni kazi bure.. Kiufupi ukipanda mbengu nzuri itachipua mmea mzuri na mbengu mbaya haiwezi kuzalisha mmea mzuri na uandishi ndio mbegu ya muvi. Ikiwa nzuri muvi itakua nzuri na ikiwa mbaya muvi itakua mbaya.

In the most part, mbengu za Bongo Muvi zinajirudia. Shambani wakulima wote wakipanda mahindi wanunuzi watanunua na yakitosha yaliobaki yataachwa yaharibike.. Ndivo ilivyo huku kwenye Bongo muvi - Watu hawanunui kwa sababu content ni weak na zinajirudia..

Uandishi unaathiri pia Sekta ya filamu kwa kutokuwalaumu waigizaji. Nina maana ipi? Script inasema jini avuke bara bara hapa hakuna kitu msanii atafanya zaidi ya kuigiza kilichokandikwa kwa sababu mwishoni hawa wasanii ni watu pia. They are looking for money to live on, kupeleka watoto shule na kadhalika kwa hivo inamlazimu aigize ili aingize kitu mdomoni sio abishane maana kazi yake ni kuigiza sio utunzi na uhariri.

Kiufupi, sekta ya filamu boresheni uandishi. Kuna vijana wana talents sana huko nje. Badilisheni ladha! Na kama shida sio uandishi mbovu basi nadharia namba tatu ndio kosa kubwa lingine..

3. Uwekezaji kidogo: Kwa wenzetu bajeti za filamu ni kubwa sana ila kibongo bongo hakuna uthubutu kwenye hilo. Wanasahu principle ndogo sana: Wekeza ili upate!

Kuwekeza kunaanzia na elimu kwenye crew. Kila aliye kwenye crew aelewe majukumu yake kwa ufasaha.. Achana na hilo, hii sio promo, ila kwa wale wanaoifahamu Wanene Entertainment, kuna kila aina za vifaa pale. Kuanzia watu na kila kitu. Kwa filamu fupi ambazo hawa jamaa wametengeneza ni wazi wapo vizuri ila wasanii wetu hawataki kuwatumia.. Kwanini?? Ubahili.

Bongo muvi wekezeni. Cheap investments mtazidi kutupa matango pori tu. Kwa mfano mwandishi anaweza kuleta stori nzuri ila kutoa toa matukio kwa sababu bajeti itakua kubwa basi stori nayo inaharibika.. Very sad tunabaki na matukio ambayo karibia kila muvi yanakuwemo. Change!

4.Mashabiki nao ni tatizo kubwa. Sio Bongo tu hata nje! Wakati mwingine na sisi tusilaumu kwa sababu kwa namna moja au nyingine sisi nao ni chanzo cha uporomokaji wa sekta hii! Sisi tunakuaje chanzo?? Hatununui kazi za wasanii kwa njia halali. Kama ni mbaya na hutaki kuzitazama acha kuzipata in illegal ways.. Kama unaitaka support kazi zao! Itawapa moyo lakini pia hela ya kuleta kitu kizuri zaidi

Nihitimishe tu, Engo muhimu ni ya uandishi. Bongo muvi muache ku-deal na strategy za kuuza muvi baadala yake muimarishe utengenezaji muvi zitajiuza zenyewe. Angalia Malawi na muvi yao ya "The boy who harnessed the wind" mule hakuna mapigano wala ujambazi ila ni filamu ilifika mbali kwa kula dili na NetFlix. Nigeria pia ilipata deal na NetFlix zaidi ya muvi 5 ikiwemi Lion's heart na kuna taarifa za chini chini kuna muvi moja kenya inaeza kula dili la namna hio hio. Zote hizo ukizitazama hazina kung fu wala nini ila content za uandishi zina mashiko.

Niwape ka home work ebu igeni wasanii wa muziki.. Sasa hivi wanawekeza ndio maana mashabiki wanawapa sapoti!!

Mkiitumia teknolojia vizuri. Mkaandika stori zenye mashiko! Mkawekeza hela nzuri ya kutosha ili stori hizo ziwe visualized bila kukata kata mawazo ya mwandishi maana wenzetu wana msemo, chochote kilichoandikwa kinaweza kuwa katika hali ya picha inayotembea na nyinyi muige hio. I believe haya yakitimizwa flow itakua nzuri na mashabiki wakicheza nafasi yao vizuri tutavuka mipaka... Filamu zitasimama tena.

Sasa hivi sio muda wa ma nini niniFlix. Huko bado hatujafika.. Online streaming kibongo bongo inae safari ndefu ingawa sio mbaya kuthubutu lakini turekebishe kwanza halafu ndio tuendelee kujenga. Kama hard copies hatununui tukija online ambako kuna Instagram, youtube, hulu, Amazon, abc, HBO na NetFlix tutatulia kweli?? Tuanze na Branding tuje marketing sasa!

Yalikuwa mawazo yangu tu.

Ciao adiós
 
Very strong idealism Buddha, it s true kabisa katika soko la filamu tz uchawi ni hayo mambo uliyoyazungumzia Labda nyongeza kidogo kunatatizo Katika umoja wao kama wasanii sijui wanashida gani Kwasababu wamefanikiwa kujiwekea Matabaka wao wenyewe, kwamfano kuna incidence fulani ya uzinduzi wa Swahili flix kitu ambacho nilijifunza pale ni kuwa kunakundi fulani la wasanii ndio Husikilizwa kuliko WENGINE.
Pia hawapo tayariiii kupokea mabadiliko kwasababu kama ni Ushaurii zimekuwa zikitolewa mara kwa Mara lakini inaonekana kuwa hawafanyii kazi
NB. ILI TUWEZE KUINGIA KATIKA SOKO LA USHINDANI LAZIMA TUKUBALI KUBADILIKA KIFIKRA, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU KATIKA KAZI 🤔🤔
 
Wajaribu stories nyingine Kila siku mapenzi tu mara tajiri kampenda masikini mara masikini kampenda tajiri
Inasikitisha
 
Bongo movie wana matatizo yafuatayo ya kiteknikali:

1.Cinematography mbaya

Hakuna mafundi na vifaa vya kuchukua video kwa ufundi na kwa kitaalamu. Video za bongo movie ni za kishamba hazina manjonjo ya kiufundi. Kamera zinachukuliwa hovyo hovyo!

2.Facial and body expressions mbovu

Waigizaji hawajui namna ya kuonyesha vizuri hisia za usoni na mijongeo ya mwili. Wanaigiza kishamba mno bila uhalisia wa uso na mwili kama vile kuweka mikono vibaya au kusimama bila kujiamini!

3. Over-reacting

Waigizaji wanaigiza kupitiliza. Wengine wanapayuka sana au wanaonyesha hisia kali kupitiliza kama vile furaha sana au kuongea kwa madoido sana. Hii inakera na kuleta uncomfortability kwa watazamaji.

Wajirekebishe. Maana haya yote hayahitaji teknolojia kubwa wala fedha nyingi.

Directors ni washambaa!
 
😂😂 Hapo mwisho
 
Kipindi cha kanumba hata hivi bongo movie haikuwa kama watu wanavyotaka aminisha watu..movie zilikuwa mbovu tokea zamani..kanumba mwwnyewe alikuwa hajui kuigiza ..
Labda watu wwnye akili waje wawekeisingi ya movie hapa bongo..lakini tusidsnganyane eti imefia wapi ilhali haikuwahi zaliwa
 
Bongo movie wana matatizo yafuatayo ya kiteknikali:

1.Cinematography mbaya

Hakuna mafundi na vifaa vya kuchukua video kwa ufundi na kwa kitaalamu. Video za bongo movie ni za kishamba hazina manjonjo ya kiufundi. Kamera zinachukuliwa hovyo hovyo!

2.Facial and body expressions mbovu

Waigizaji hawajui namna ya kuonyesha vizuri hisia za usoni na mijongeo ya mwili. Wanaigiza kishamba mno bila uhalisia wa uso na mwili kama vile kuweka mikono vibaya au kusimama bila kujiamini!

3. Over-reacting

Waigizaji wanaigiza kupitiliza. Wengine wanapayuka sana au wanaonyesha hisia kali kupitiliza kama vile furaha sana au kuongea kwa madoido sana. Hii inakera na kuleta uncomfortability kwa watazamaji.

Wajirekebishe. Maana haya yote hayahitaji teknolojia kubwa wala fedha nyingi.

Directors ni washambaa!
Namba moja hapo ni tatizo kubwa
 
Jambo lakwanza wanatunga story ambazo azipo kwenye jamii yetu, alafu wanaigiza matukio ambayo muhusika aendani na mazingira ya eneo usika
 
Siku zote mtoto wa tajiri anataka kumuoa Mtoto wa Maskini..wazazi wanakataa
 
Wanaigiza maisha ambayo sio ya Kitanzania. Pia wahusika hawaendani na kile wanachokiigiza. Mtu anamiliki kampuni kama za MO anatembelea Passo. Mtu anaigiza kazi yake ni messenger lakini anamiliki jumba Masaki
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom