Noti mpya kuchapishwa Tanzania

Ilumine

Senior Member
Dec 27, 2008
196
4
Leo, jioni hii katika runinga, nimesikia ya kuwa makampuni mawili ya huko ulaya yameshinda zabuni ya kuchapisha fesha/noti mpya za Tanzania. Hawakusema lini utekelezaji utaanza, na lini tutaanza kubadilisha noti tulizonazo nk.
Hoja yangu: Ninajua fika ya kuwa zoezi hili hutumia gharama kubwa sana. Mimi sijui, labda ni kwa sababu ya uelewa wangu mdogo, sijui sababu za msingi hasa zinazotufanya watanzania tuingie katika matumizi makubwa kama hayo. Ninajua, wataalamu wetu wanaweza kutoa maelezo mazuri ya kutujulisha uzuri au faida au lengo zima la zoezi, ambalo kwa vyovyote watasema litasaidia kuuinua uchumi wetu unaochechemea. Yapo mambo makubwa yanayotukaba watanzania kwa sasa, mfano tatizo la mgawo wa Umeme. Mambo kama haya, tunabaki kuyajadili tu bila kuchukua hatua zozote za haraka, tunaendelea namambo mengine ambayo hata yakicheleweshwa hatutaonja utofauti wowote. Noti zetu zina kasoro? au ndio tunauboresha uchumi wetu? Pengine hii ni njia ya kutaka kufanya kamchezo fulani, huku sisi raia tunapigwa changa la macho.
 
gharama nyingi ? umesahau kwamba uchaguzi mwakani! tegemea kuona mambo kama haya ya kuiingizia serikali gharama kubwa kuongezeka hasa katika kipindi hiki. Je unataka kujua baadhi ya hizo pesa zinapoenda ? nikikwambia utalia
 
Habari hii ipo pia mwananchi. Lakini swali linakuja: Hawa jamaa wanataka kwenda kwenye federation ambapo tutatumia pesa moja na wamekuwa wakisema 2012 tutakuwa tumefika huko. Sasa sijui tunachapa pesa mara ngapi? Yaani tuchape pesa tutumie mwaka then tunabadilisha????
 
Hivi wameshaanza kudai wasafiri airport elfu kumi ya kuchaniga uchaguzi???
hawa jamaa huwa hawapigi dili za kitoto!! wakiamua 'KULA" wanakula kweli kweli. si umesikia lakini sijui lini mabilioni yamepotea hivi hivi kupitia trl, uchaguzi huo upo karibuni!
 
hawa jamaa huwa hawapigi dili za kitoto!! wakiamua 'KULA" wanakula kweli kweli. si umesikia lakini sijui lini mabilioni yamepotea hivi hivi kupitia trl, uchaguzi huo upo karibuni!

Si mchezo nawaaminia ila nakumbuka kipindi kile miaka ya 2000 nilikuwa natoka nje ya Tz na nikaambiwa nilipe buku kumi ya kuchaniga Uchaguzi ukute safari hii watafanya buku 30 lol!:confused::confused::confused::confused:
 
tena wamesema zitaanza kutumika mwakani na hapa tusipokua makini tutakua tunanunua soda kwa noti moja sh. 10,000 maana kila siku pesa yetu inazidi kuporomoka
 
Si mchezo nawaaminia ila nakumbuka kipindi kile miaka ya 2000 nilikuwa natoka nje ya Tz na nikaambiwa nilipe buku kumi ya kuchaniga Uchaguzi ukute safari hii watafanya buku 30 lol!:confused::confused::confused::confused:

Dada Maria nani huyo anayekusanya hizo pesa hapo airport? Na ukikataa kutoa inakuwaje? Na nani huwa anazitumia, vyama vyote au CCM tu?
 
Si mchezo nawaaminia ila nakumbuka kipindi kile miaka ya 2000 nilikuwa natoka nje ya Tz na nikaambiwa nilipe buku kumi ya kuchaniga Uchaguzi ukute safari hii watafanya buku 30 lol!:confused::confused::confused::confused:
duh, yaani uliichangia ccm bila mwenyewe kujua, aisee hii kali! kweli walikupata!
 
Ukiona hivyo kuna mawili yanayoweza kuwa factor.

1.Noti bandia zimezagaa.

2.Wanataka kupiga panga la uchaguzi.
 
Ukiona hivyo kuna mawili yanayoweza kuwa factor.

1.Noti bandia zimezagaa.

2.Wanataka kupiga panga la uchaguzi.
in red - hii imekuwa sababu ikitumika over and over, yaani ina maana zikizagaa feki, kazi yao ni kuchapisha mpya bila kuweka any security features, kwa hiyo kinachobadirika ni upya wa noti tu na si kingine, weweeee kweli tznia tambarare.....uchaguzi huo mzazi mwezi huu na mwakani mwezi kama huu
 
hawa jamaa huwa hawapigi dili za kitoto!! wakiamua 'KULA" wanakula kweli kweli. si umesikia lakini sijui lini mabilioni yamepotea hivi hivi kupitia trl, uchaguzi huo upo karibuni!

Tanzania yetu hii, nchi inaenda kisiasa zaidi.
 
Du! hii ni guarantee kua hakutakua na tatizo la fedha za ku spend wakati wa uchaguzi mwakani. halafu uzuri ni kwamba hata E&Y au PWC wakiitwa kukagua hawataweza kuona kitu maana hawawezi jua zili printiwa ngapi. Kweli nchi hii kuna watu very creative. I do not know who is the brain behind this new scheme.

Lakini tusije kuelekea zimbabwe, maana kwa mtindo huu sijui itakuaje. Itabidi nifungue account ya Dollar, Oh no Dollar sio safe sana kwa sasa afadhali ya Euro.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom