Noti mpya bandia sasa zapitia benki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Noti mpya bandia sasa zapitia benki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Feb 16, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Shadrack Sagati;
  Tarehe: 15th February 2011


  KASHFA ya kukithiri kwa noti mpya bandia inazidi kuongezeka na sasa imebainika kuwa hata baadhi ya benki nchini zinashindwa kuzibaini na hivyo kujikuta zinaziingiza kwenye mzunguko.

  Hali hiyo inatokana na Karani wa Fedha wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Februari 14 kuchukua fedha benki ya CRDB tawi la Lumumba na bila kutambua hatimaye akagundua amepewa noti nyingi za Sh 10,000 zikiwa bandia.


  Hata pale mmoja wa wafanyakazi wa TSN aliyepewa noti hizo alipokwenda kuweka baadhi ya noti hizo kwenye moja ya benki bila kujua kuwa ni bandia, karani wa benki hiyo alizipokea na kuzipitisha kwenye mashine na kuridhika kuwa ni halali.


  Kitendo hicho kinaonesha kuwa mashine za benki hazizitambui noti hizo na hata wafanyakazi wenyewe wa benki yawezekana hawana utaalamu wa kutosha wa kutofautisha noti bandia na halali hasa za Sh 10,000.


  Noti hizo ziligunduliwa na wafanyakazi waliopewa fedha hizo baada ya kuanza kuzitumia na kukataliwa mitaani ambapo jana baadhi yao walijikuta wakiwa na noti hizo.


  Meneja wa Fedha wa TSN, Diana Lyatuu, alithibitisha kuchukuliwa fedha hizo kutoka benki ya CRDB tawi la Lumumba kwa kubadilishwa na hundi.


  Noti nyingi ambazo zimezagaa ni zinazoishia na namba 366 na 362 ambazo ndizo wafanyakazi wengi wa TSN walikabidhiwa.


  Mmoja wa wafanyakazi wa TSN, Nelly Mtema, alikamatwa na Polisi baada ya kuzitumia fedha hizo alizopewa ofisini kwa ajili ya kwenda kulipia bili ya maji katika ofisi za Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO).


  Akielezea tukio hilo, Mtema alisema Februari 15 asubuhi alikwenda Dawasco kulipia maji lakini akashangaa kuwekwa chini ya ulinzi kwa maelezo kuwa ana fedha bandia.


  "Niliwakatalia kuwa si bandia kwani nililipwa ofisini, lakini nikapelekwa Polisi kituo cha Kimara," alisema Mtema ambaye baada ya kuzichunguza noti hizo aligundua bandia zikiwa tatu za Sh 10,000.


  Aliongeza kuwa baada ya sakata hilo, alilazimika kupiga simu ofisini, kufahamisha kuwa fedha alizopewa ni bandia na amekamatwa na polisi baada ya kuzitumia kulipia huduma ya maji.


  "Ofisini walizungumza na polisi juu ya kuwapo tatizo hilo ndipo nikaachiwa," alisema Mtema.


  Mkurugenzi wa Masoko wa CRDB, Tully Mwambapa, alipoulizwa juu ya tatizo hilo, alisema ana uhakika asilimia 100 ya fedha hizo hazikutolewa na benki yake.


  "Sisi tuna sheria inayomtaka mteja ahesabu na ahakiki fedha zake kabla ya kuondoka dirishani, itakuwaje keshia aondoke ndipo tupokee malalamiko ya kuwapo fedha bandia?" Alihoji Mwambapa.


  Keshia wa TSN alipoulizwa alisema hakuona haja ya kuhakiki fedha hizo kwa vile anaiamini benki hiyo kwani amefanya nayo kazi kwa siku nyingi. Hata hivyo, Mwambapa alisema: "Benki yangu ina sera ya kutoaminiana katika mambo ya fedha."


  Alijitetea kuwa kila dirisha lina kamera inayochukua mwenendo wa matukio ya kuanzia asubuhi hadi jioni yanayofanywa na karani aliyepo kwenye dirisha husika. "Ndiyo maana nasema fedha hizo hazikutoka kwetu," alisema


  Gazeti hili lilitaka kujua ukweli kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na kukithiri kwa noti hizo bandia, lakini simu ya Gavana Benno Ndulu ilikuwa inaita bila majibu.


  Baadaye Katibu Muhtasi wa Gavana alisema bosi wake alikuwa kwenye kikao muhimu na akashauri mwandishi kama ni suala hilo la noti bandia uulizwe uongozi wa benki husika kwani utakuwa na majibu ya tatizo hilo.


  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mji Mkongwe, Ibrahim Muhamad Sanya (CUF) ametoa hadhari kwa BoT na Hazina juu ya kuzagaa kwa noti mpya bandia na kuvitaka vyombo hivyo kuchukua hatua za haraka kwa kuwa kuna hatari ya uchumi kuathirika.


  Sanya alitoa hadhari hiyo na kuwasilisha noti bandia ya Sh 10,000 juzi bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoiwasilisha wakati akifungua Bunge la 10, mwaka jana.


  Kwa hadhari hiyo, Spika wa Bunge Anne Makinda, aliitaka Wizara ya Fedha kuwasilisha taarifa juu ya suala hilo bungeni. Akiwasilisha noti hiyo, Sanya alisema iligundulika kuwa bandia baada ya kukaguliwa na kubainika haina picha ya Baba wa Taifa upande wa kushoto.


  Alipoulizwa na Spika Makinda alikoipata noti hiyo, alisema alikabidhiwa na mfanyabiashara ndogo mjini Dodoma ambaye alidai kuipata kwa mteja aliyemwuzia bidhaa, hali ambayo ilimtia hasara kwa kuwa kiasi hicho cha fedha ni sawa na mtaji wake.


  "Kijana huyo aliponiona alinikabidhi noti hii na kudai kuwa kwa sasa zimezagaa mjini hapa na kunitaka niiwasilishe bungeni ili vyombo husika vichukue hatua, kwa kuwa hali mtaani ni mbaya," alisema Sanya.


  Akipokea taarifa na noti hiyo, Makinda alimshukuru Sanya kwa kutoa taarifa hiyo, na kuitaka serikali ichukue hatua za haraka na kulitolea maelezo suala hilo bungeni.


  Chanzo: HabariLeo
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu gavana Beno Ndulu ashinikizwe kujiuzulu...................
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hii nchi haiaminiki tena inabidi Tanzania iwe katika black list!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahahahahah,BLAKLIST DUH!mi nimechoka sasa,hata benki?tuamini wapi sasa?
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Hii Avatar yako nimeipenda.............
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Kweli Tz inabd iwe blacklisted: maana kila kona wmejaa vilaza na majambazi tu! Inakuwaje meneja wa benki unajibu tuhuma kimkatomkato tu!

  Huwezi kusema una uhakika wa asilimia 100! na kuwa mteja kuhesabu noti dirishani na akitoka nje ya hapo na kugundua kuwa amepewa noti feki inakuwa haiwahusu! Na yule mjingamjinga wenu akawa anajinadi kuwa wametengeneza noti zenye viwango vya hali ya juu..., hii noti ikizunguka kwenye mikono ya watu watatu tu imepauka na kuchakaa vibaya!

  Hii nchi inaendeshwa kijingajinga sana.
   
 7. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Temea mate chini mkuu!
   
 8. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Asante swetie naomba biblia
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Sina hamu tena na habari za bongo kila kukicha kuna balaa jingine. tutaishia wapi?
   
 10. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kuna haja ya wanaohusika kutokulala wakiutafuta mtandao wa kughushi noti hizo ili wausambaratishe. Na wakati huohuo watangaze namna ya kuzitambua noti feki kila siku katika vyombo vingi vya habari.
   
 11. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Avatar yako pia ipo kwenye black list! Kwanini usiibadilishe mpendwa?
   
 12. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Nikubadilisha mfumo wa usalama wa taifa tatizo wamerelux sana hii kashfa ni yakwao nazaidi wamekuwa ba mahusiano zaidi na raia tofauti na ilani za kazi zao kwakisingizio cha utandawazi na kufanya kazi zao kiteknolojia wakati wao wanatakiwa kufanya kazi kivitendo zaidi japo pale panapohitajika teknolojia itumike teknolojia.
   
 13. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Haa nabadilisha si wajua nina Damu ya ki tz lazima niwepo kwenye list :coffee::coffee:
   
 14. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huwezi kusema una uhakika wa asilimia 100! na kuwa mteja kuhesabu noti dirishani na akitoka nje ya hapo na kugundua kuwa amepewa noti feki inakuwa haiwahusu! Na yule mjingamjinga wenu akawa anajinadi kuwa wametengeneza noti zenye viwango vya hali ya juu..., hii noti ikizunguka kwenye mikono ya watu watatu tu imepauka na kuchakaa vibaya!

  Nilisikia kwamba mtalaam aliletwa kuja kuwahakikishia watanzania kuwa fedha mpya ina kiwango cha hali ya juu! sasa sijui kama walimlipia kuja au alikuja kwa gharama zake mwenyewe? Inanikumbusha mbali sana wakati bajeti ya mama zakia, mawaziri walikwenda mikoani ili kuwahakishia watanzania kuwa ni nzuri sana baada ya malalamiko lukuki.
   
 15. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Badilisha basi kwani unanisababishia matatizo yasiyo ya lazima!
   
 16. Profesy

  Profesy Verified User

  #16
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  du,kuna faulu hapo benki.
   
 17. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is very serious issue economically. Hii ni zaidi ya kuhujumu uchumi. Yaani watu wanaweza tu kutengeneza pesa bandia kirahisi tu. Gavana wa benki kuu ajiuzulu haraka iwezekanavyo.

  Nashauri hatua za dhararu kama ifuatavyo.

  1) Gavana wa benki kuu na wale wote waliohusika kutengeneza hizo noti wajiuzulu mara moja kwani wameshindwa kazi
  .
  2) Benki kuu au serikali itangaze kuziondoa hizo noti kwenye mzunguko wa fedha mara moja. Watu wasiruhusiwe kufanya biashara kwa hizo noti. Watu ambao wanazo hizo noti wazirejeshe kwenye mabenki na kuwe na watu maalum wa kuzipokea hizo noti zinaporejeshwa ili kudhibiti noti bandia.

  3) Noti za zamani ziendelee kutumika.
   
 18. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tulipo...sipajui.
  Tuendapo...sipajui.
  uchumi wetu...siujui.
  Uchumi unakua au la...Sijui.
  Currecny yetu inathamani...sijui.
  Sababu ya kutoa pesa mpya...sijui.
  Wananchi wanaathirika nazo mtaani...sijui.
  Lakini zipo noti feki mtaani...sijui kama zipo...hebu tuletee uthibitisho nimuagize XYZ afanye uchunguzi.
   
Loading...