North Korea yarusha kombora

North Korea yarusha kombora

Kwanini inakimbiwa sasa?! Na kwann ukitaka kutoroka nchi adhabu yake ni kifo kama kweli Maisha ni mazuri huko
Mkuu mbona tunazunguka pale pale? shida ni uthibitisho unaleta habari za kuandikwa na adui yake. Yaani wewe mtu unayemshutumu kutembea na mke wako unaweza kuandika habari nzuri juu yake???
 
Duniani kote hamna data hata kuhusu north korea,sasa ww hizo data umezitoa wapi?? Kama sio umbea tu
Hali ya maisha ya watu wa North Korea ni Mbaya sana.
Sio nchi ya kutamani kuzaliwa pale.

Tangu mwaka 1995, CHINA NA USA
Zimepeleka msaada zaidi ya 75% wa Chakula.

Maafa ya njaa miaka ya 90s yaliua watu kuanzia laki 8 hadi milioni 2.4 kutokana na Ukame.

Hawa malofa wa North Korea wamekua wakikosolewa kwa kuwekeza Nguvu na rasilimali za nchi kwenye silaha za vita. Wakati mahitaji ya msingi ya watu wake ni hafifu.

Majuzi tu, waliagiza wananchi wakusanye Vinyesi yao ili kuweza kuhimili uhaba wa mbolea ya shambani. Mpaka mnaamrishwa kukusanya vinyesi vya binadamu, hii sio indicator ya nchi iliyopiga hatua.


Ni kweli kwamujibu wa tafiti ya Gallup, North Korea ndiye adui Mkubwa wa USA kwa sasa, ikifuatiwa na Russia, China na Iran ambayo inasemekana ni ya Mwisho.

Na watu wanaoichukia USA hujaribu kujipa matumaini kua North Korea iko vizuri, huku wakijua ni kujidanganya. Hata ukitumia common sense, taifa lenye kuwekewa vikwazo popote pale hali ya wananchi wake haiwezi kwenda vizuri.

China ndiye amekua msaada mkubwa kwa Taifa hili kwa muda mrefu sasa.
 
Wanapata msaada mkubwa Sana kutoka China.
40% ya wananchi Wa North Korea wanateseka kwa Njaa kali. Mwaka huu mwanzoni waliomba msaada wa chakula.
Wanahitaji misaada ya kiutu.

Atakuja Mjinga na kukuaminisha kua pamoja na vikwazo, North korea hawana shida wako, vizuri.

 
Back
Top Bottom