ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Korea ya kaskazin imesema kwamba jaribio la hivi karibuni la udunguzi wa kombora la masafa marefu(ICBM) lililofanywa na Marekani ni hatua ya hatari ambayo inaleta chokochoko za kijeshi.
Pia imeeleza kwamba jaribio hilo linaonyesha kwamba matayarisho ya vita vya nuclear yapo kwenye hatua za mwisho kwa upande wa Marekani. Na kuendelea kwa kuionya Marekani kwamba isidhani inaweza kuhimili mashambulizi yao(Nkorea) na kwamba Marekani haiwez kushinda vita hivyo kwa kua itageuzwa kua majivu.
Kauli hiyo tata inafuatia baada ya marumbano na vitisho vya muda mrefu kati ya Marekani na korea kaskazini kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Korea kaskazini.
Hapo awali, Rais wa Marekani Donald Trump alituma meli kubwa ya kubeba ndege(aircraft carrier) 'armada' kwenye pwani ya Korea ambapo Jeshi la korea kaskazini lilitisha kuizamisha meli hiyo na pia kushambulia ngome za jeshi zilizopo Japan na Korea kusini.
Vyanzo mbalimbali vinaeleza kwamba mfumo huo uliotumiwa na Marekani (Ground Based MidCourse Defense System) kudungua kombora hilo ulianza kufanya kazi mwaka 2005.Ulibuniwa kwa ajili ya kudungua makombora ya masafa marefu(ICBM).Pia una uwezo wa kudungua kombora likiwa hata nje ya dunia (exosphere).
Kwa sasa mifumo hiyo kama 30 imefungwa Alaska na California kulinda Marekani dhidi ya shambulizi lolote huku mingine 15 ikitarajiwa kumalizika 2017.