Nomben ushauri tumsaidie huyu dada. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nomben ushauri tumsaidie huyu dada.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Cantalisia, Oct 18, 2011.

 1. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Habari zenu wapendwa,kuna met wangu hapa oficn ana tatizo ambalo hata yeye mwenyewe haelewi ni tatizo gani,ni mtu ambaye relation zinamsumbua sana,amekuwa akitendwa mara kwa mara kwa ni mtu mwenye hasira na wivu sn,japo huwa akipenda anapenda kweli na wala huwa hatoki nje ya uhusiano anapokuwa mtu,relation yake ya mwisho ilikuwa na maumivu makali sana kwake kwan alimpata mtu aliyeza kumtuliza hasira na wivu wake na wakawa wameshatambulishana,wakiwa wanaendelea na relation met wangu akagundua jamaa ana mke wa ndoa na mtoto kupitia simu yake ila mke wake yuko mkoa mbeya ni mwalimu,alipomuuliza jamaa kutokana na ushahidi ikabidi akiri na kuomba msamaha ila ndio met wangu akakasirika na kuachana naye.

  Sasa ni miezi minne tangu yuko single amekuwa ni mtu wa mawazo sn amepungua na ameshindwa hata kujipendezesha km awali,anasema upweke ndio tatizo anataman kuwa na mpnz na anahic hawezi kuwa peke yake, anataman apate mtu wa kumwonyesha mapnz yake na watu wanaomtokea wapo ila anashindwa kuwaamin na hata kuwa nao,nimejitahidi kumshauri nahata kumwonyesha sred za humu za kufanana na matatizo yake lkn tatizo haliishi na ameendelea kuwa hivyo,saa nyingine unakuta analia tu,nikimuuliza anasema anataman angekuwa na mpenz akamweleza anavyojisikia,kwakweli ni hali ambayo mie km binadamu mwenzia inanihuzunisha na nimeshindwa namna ya kumsaidia na kuamua nilete kwenu wadau tuone tumsahuri nn japo kumsaidia,nawakilisha.
   
 2. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kwana kabisa mpe pole besty wako....

  jambo la kwanza kabisa naona ni bora yeye aendelee kutulia...hamna shida ya kuwa na papara ya kuingia kwenye uhusiano mwengine kwa kuwa kwa sasa yupo emotional na hivyo judgement yanke itakuwa sio sahii.

  pili ni wakati wa yeye kukaa chini na kujichambua kwa undani kwa nini mahusiano yake yeye yanaishia pabaya....hapa sasa inabidi awe kweli kabisa maana ndio atapata kujua tatizo lipo wapi na hivyo kujirekebisha. kwa mtazao wangu naonakuwa uchaguzi wake unaweza kuwa mbovu....na hii inaweza kuwa inatokana na yeye kuwa mtu wa hisia kali alizonazo na hivyo zina cloud judgement zake na kushindwa kuona the real person ambaye anataka kuingia nae kwenye mahusiano....wanaume wasanii bwana...maneno matamu mpaka unalegea lol!

  mwisho kabisa attitude yake inabidi ibadilike....na inatakiwa aanze na fikra zake kubadilika kuhusiana na mtazao wake wa hali aliyokuwepo sasa. ni vyea kwanza ajue mapungufu yake yaliyochangai kwa yeye kupatwa na mikasa hiyo hivyo kubadilisha jinsi anavyojiendesha wakati anaanzisha mahusiano. pia she must think positive....kwa kuwa bado wapo wanaume wanamtaka aichukulie hiyo kama kuwa yeye bado ni mrebo na with careful selction atapata tuu mwanaume ambaye atamfaa yeye.

  ila mwambie kabisa kwa sasa asiingie kwenye uhusiano wowote ule....tulizana na afanye self evaluation!!!!
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mpe pole shostito,mwambie asijali yote yatakwisha na atamsahau huyo bwana lakini na yeye pia asi pende kupita kiyasi,na asiwe mwenye wivu sana amuamini mpenzi wake na asiweanamshuku unajua wivu mwingi kwa mwanamme pia n kero,ajaribu kujishughulisha na kazi zake kwani akiwashiriki sana wanaume watampeleka pabaya,avute subra ajirekebishe na yeye mapungufu yake,na amuombe Mungu atampa mwenye kheir na yeye...
   
 4. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Sawa mkuu kwa amesoma majibu yako na ushauri wako anakushukuru sana na ameahidi kuufanyia kazi.
   
 5. bulldoza

  bulldoza Senior Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpe pole na hongera kwa kuachana na huyo mwizi (mume wa mtu)ni wachache sana ambao wana busara kama zake kiuiumiza kwa muda akiamini atapata mwanaume wake mwenyewe....
  Pili mweleze haitaji kulia na kujichoka na kujichukia ila anahitaji muda ajipe muda wa kukaa mwenyewe bila kuchokorwachokorwa ..atoke na nyie marafiki zake...nendeni cinema hata baada ya kazi ...wkend pls m-kip busy nenda naye swimming places....mpe raha rafikiyo ajione nayy ana marafiki...yes we need to be loved sumtymes but some ppl they dont deserve to be given our loves....aone hao wote was one of them...she needs time to heal her souls...
   
 6. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hilo la wivu ndio tatizo kubwa huwa anamwamini ila anapenda kila wakati wawe wanaongea kuchati muda wote ajue yuko wapi na mambo km hayo ambapo kwa sasa ameazimia kudeal na hali hiyo,amesoma ushauri wako na anakushukuru sana.
   
 7. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Amesoma na amekuelewa mkuu nami nitajitahidi kumkip busy angalau asifikirie haya mambo tena!
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mwambie aende kwenye thread ya Russian Roulette asome huo mpambano atacheka na ku relax kidogo! On a serious note mwambie rafiki yako kwamba sasa anakaribisha ulcers tena kwa ari na kasi. Hakuna kitu kibaya kwa afya kama worries. Mwambie aanze kwenda gym,a join kwaya kama ni mkristo,ajiunge na music school kama anapenda muziki,aanze kozi mpya ya evening class,the point is mwambie atafute kitu cha kumshughulisha baada ya kazi,haya mambo ya wanaume na malavidavi asiyaweke mbele sana bana yatakuja yenyewe,afterall wanaume kibao town hapa.
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Binandamu yoyote yule mwenye wivu wa kupindukia hawezi kufanikiwa katika jambo lolote lile maishani!
   
 10. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante bishanga,at least ametoa tabasamu baada ya kusoma coment yako,jana nilimwonyesha ila sred ya RR kwa alivyokuwa wala hakuisoma ndio anaisoma sasa,asante kwa ushauri mkuu.
   
 11. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Amekiri na kukubaliana na wewe na analifanyia kazi tatizo hilo ili aondokane nalo!
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,026
  Trophy Points: 280
  Cantalasia rafiki na mjukuu mwema,

  Unavyosema "amekiri, amekusoma na amekuelewa" unataka kutuambia huyo mtu uko naye hapo?

  Kama uko naye mwambie anipungie mkono nione............
   
 13. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Niko naye hapa babu, anapunga huuoni babu?
   
 14. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  cantalasia!! ni aje umetoa siri zangu JF!! na nilikwambia iwe siri yako!!
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,026
  Trophy Points: 280
  Kwakuwa ana matatizo, nimekubali kupungiwa na mkono wa kushoto, azawaiz ningemtukania kikojoleo chake......

  Beki tu ze topic.............mwambie Mie Babu ODM a.k.a bigi braza Asprin babu wa wajukuu wa kike namwambia hivi:

  1. Ajiunge na JF awe anauliza maswali mwenyewe ili akitongozwa na masharobaro ya huku ajue namna ya kupambana nayo, siyo kulialia hivyo.

  2. Mapenzi hayatafutwi bali yanakuja nachurale..... Saa nyingine anapaswa amshukuru Mungu kwa kutendwa labda yawezekana ameepushwa na mazahma makubwa zaidi

  3. Maisha haya ni mafupi sana, aachane na biashara ya kujuta na kuvililia vibaiolojia vya kiume. kwani bila vikojoleo maisha hayaendi?

  4. Kwa kuwa wanaume ni wakarimu sana, fuatilia sredi ya RR, asijibane sana. Akipata mpango wa nje ajirushe kwa raha zake. Angalizo: Asivunje ndoa za watu

  5. Kwa ushauri zaidi anitafute PM

  Wewe sema Amina mwambie yeye anipigie makofi kwa ushauri huu.

  NB: Mara ya mwisho nilimshauri Graca Marchel, akautumia ushauri huu akazidisha viwango akampindua Winnie Mandella......... Dont practice this at home.
   
 16. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Umetisha Aspirin..
  BUT umejipigia sana promo..
   
 17. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ni pouwa kbs my dia,nisamehe tu coz nia yangu ni njema ni ili tupate msaada coz napenda kukuona mwenye furaha wakati wote feis!
   
 18. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  sure Baba_Enock,...anything than enough is harmfull,..imeandikwa tuwe na kiasi mkuu
   
 19. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  na huu wivu wa kupita kiasi sijui wanajifunzia wapi,...mimi mbona sinaga
   
 20. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Babu ujumbe umefika tena kausoma mwenyewe,na ameahidi kujiunga very soon,akijiunga cha kwanza ni kuku pm then mambo mengine yaendelee.
  Amesoma ile sred ya RRila anasema anaogopa waume za watu anataka wake peke yake.
  Anashukuru kwa ushauri na ameahidi kuufanyia kazi.Amekupa saluti ya kutosha babu, namimi mjukuuu wako nimeitikia amina na amekupigia makofi ya kutosha babu.
   
Loading...