Halafu nimekuuliza kuna tofauti gani kati ya huyo alligator na mamba?Hujaona juu?
Hahaha this's interesting now...sikuwa nimeona kipenzi
Binomial Nomenclature:
Alligators na Crocodile wote ni reptilia wanatokea kwenye order ya
Crocodylia lakini wanatofautiana familia zao Alligators (Alligatoridae) na Crocodiles (Crocodylidae).
Kitu ambacho kipo so interesting ni kuwa Alligators wote ni Crocodiles lakini Crocodiles wote si Alligators...funny uunh!!!
Crocodiles (Mamba):
Kwa kawaida mamba huwa ana kichwa kirefu zaidi ya alligators na kina shepu ya V.
Mamba akifunga mdomo wake, basi jino moja la nne huwa linaonekana kwa nje.
Mamba anaweza kuishi kwenye maji chumvi na maji baridi...ana uwezo wa kuchuja chumvichumvi iliyopo kwa maji hayo
Mamba wapo aggressive zaidi ya alligators...yaani ukifanya masikhara anakufanya kitoweo haraka mno.
Mamba hupatika karibia mabara yote ulimwenguni, wakati alligators hupatikana Amerika, Bara Hindi na Uchina.
Alligators:
Hawa huwa na kichwa kifupi halafu kipana na huwa na shepu mithili ya U
Alligators huishi kwenye maji baridi tu na mara nyingi huwa zile sehemu za vina vifupi.
Hawapo aggressive kama walivyo mamba.
Mara nyingi huwa wana ngozi yenye weusi mwingi kulinganisha na mamba.
Alligators hupatikana Amerika, Bara Hindi na Uchina.