Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Ni Septemba mosi ya mwaka 2000 mara baada ya mchakato mkubwa wa kurudi tena jikoni na kuipika na kufanyia kazi mapendekezo, na madhaifu ya Nokia 3210, siku hiyo ya Ijumaa ikawa ni siku bora kuwahi kutokea katika uwanja wa teknolojia ya mawasiliano, kwani ndio siku ambayo dunia kwa mara ya kwanza ilipata kupewa zawadi ya simu bora kutoka kwa Nokia. Simu ambayo inaaminika kuwa ndio simu bora kuwahi kutokea katika historia za utengenezaji wa simu duniani.
Ni Nokia 3310 ilizinduliwa rasmi katika kipindi ambacho kampuni ya Nokia ilikuwa ikiongozwa na Mika Anttonen (Mika Anttonen alikuwa CEO wa Nokia katika miaka ya mapema ya 2000). Mkuu wa Uendeshaji wa Nokia aliyeongoza kipindi hicho cha mafanikio makubwa alikuwa Jorma Ollila, ambaye aliongoza kampuni hiyo kuanzia 1992 hadi 2006.
Jorma Ollila anahesabiwa kuwa mmoja wa viongozi muhimu wa Nokia ambao walifanya kampuni hiyo kuwa tajiri na maarufu duniani kama kiongozi wa simu za mkononi.
Kwa mujibu wa wataalamu wa usimamizi wa makampuni, Jorma Ollila alikuwa mstari wa mbele na alichangia msukumo mkubwa kwa Nokia kuwekeza katika teknolojia ya GSM na kuimarisha utafiti na maendeleo ama R&D, jambo ambalo lilisababisha kuzalishwa kwa bidhaa bora kama Nokia 3310.
Katika kitabu cha The Nokia Revolution: The Story of an Extraordinary Company That Transformed an Industry cha mwaka 2011, mwandishi Dan Steinbock anaelezea kuwa “Jorma Ollila alikuwa mhimili mkuu katika mabadiliko makubwa ya Nokia, akielekeza kampuni kuwa kiongozi wa soko la simu za mkononi duniani.”
Kazi bora sana ilikuwa iliwezekana kwa sababu ya timu ambayo ilikuwa imepokea maono baada ya wadau kuonesha kuwa kuna mapungufu kwenye Nokia 3210, moja ya mtu wa muhimu sana ambaye aliweka msingi wa utengenezaji alikuwa ni Pekka Ala-Pietila ambaye alishirikiana na timu ya uzalishaji yenye watu wenye akili kubwa sana, watu kama Frank Nuovo ambaye alikuwa ni Chief Designer, Timo Ali-Vehmas, Pertti Korhonen na wengine wengi.
Simu hii ilijulikana sana na kuwa maarufu kutokana na ubora wa betri yake kukaa na moto kwa muda mrefu wakati wa matumizi; mtu angeweza kuitumia kwa siku kadhaa bila kuichaji tena.
Kwa mujibu wa mchambuzi wa teknolojia kama Andy Walker kutoka TechRadar, Nokia 3310 “ilikuwa simu imara sana katika kutunza moto, ikishinda hata simu za kisasa zinazojulikana kwa teknolojia zao za hali ya juu.” Walker anaongeza kuwa “ubora wa vifaa ulifanya simu hii kuwa ngumu kuvunjika kirahisi hata baada ya kuanguka kutoka kwa urefu .” huku Andy Walker akiipatia jina la Indestructible Maniac
Mitandaoni kumejaa meme na video zikionesha namna ambavyo hii simu ilikuwa ni imara sana, kiasi kwamba baadhi walifananisha na namna wafua vyuma kuwa ndio waliohusika kutengeneza body ya simu hii. Kuna maelfu ya meme zinazoonesha namna simu hii ilivyokuwa bora.
Katika utafiti wa mwaka 2019 uliofanywa na Chuo Kikuu cha Helsinki, Nokia 3310 ilichukuliwa kama mfano bora wa vifaa vya mtandao vilivyo na muundo unaodumu na kuhimili hali mbalimbali za mazingira, jambo ambalo limekuwa changamoto kwa watengenezaji wa simu za kisasa zinazojikita zaidi katika muundo wa kioo na wembamba wa chini zaidi.
Wakati Nokia 3310 ilipopata umaarufu wake, pia kulikuwa na washindani wakubwa waliokuwa wakipambana kupata sehemu ya soko la simu za mkononi. Miongoni mwa washindani wakuu walikuwa:
Motorola: Kampuni ya Marekani haikuwa nyuma kwani ilikuwa na simu maarufu kama Motorola StarTAC, ambayo ilijulikana kwa muundo wake wa kifahari na uzito mwepesi, ingawa kwa upande wa uimara na maisha ya betri, Nokia ilishika nambari moja.
- Ericsson: Kampuni ya Uswisi, iliyokuwa na simu za aina ya Ericsson T28 na T39, ambazo zilikuwa maarufu kwa teknolojia zao za Bluetooth na mtindo wa kisasa, lakini zilikosa upinzani wa uimara wa Nokia 3310.
- Siemens: Kampuni ya Ujerumani pia ilikuwa ikizalisha simu za mkononi zenye muundo wa kipekee na ubora wa ujenzi, lakini bei zao zilikuwa juu ikilinganishwa na Nokia. Wao Siemens walikuwa na simu bora sana kama vile, Siemens A60 pamoja na Siemens SL45.
- Samsung: Ingawa bado haikuonekana kuwa na nguvu kama leo, Samsung ilikuwa ikianza kujijengea soko kwa simu za mkononi katika miaka ya mapema 2000, lakini bado haikufikia umaarufu wa Nokia 3310 katika sekta ya simu za msingi. Simu kama vile, Samsung SGH-600 pamoja na **Samsung SGH-2100 ambayo ilikuwa ni moja ya simu za mwanzo zilizokuwa na uwezo wa 3G ndani ya Korea Kusini.
Kulingana na ripoti ya Gartner ya mwaka 2001, Nokia ilishikilia zaidi ya 30% ya soko la simu za mkononi duniani, ikiifuata Motorola na Ericsson kwa sehemu ndogo zaidi.
Nokia 3310 haikuja na matumizi mengi ya kisasa ya simu za smart, ama vishikwambi vya sasa ama simu janja lakini kwa uhalisia Nokia 3310 ubora wake ndiyo nguvu yake.
Ilitoa huduma ya msingi na rahisi: kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi (SMS), na michezo kama Snake, Space Impact, pamoja na Bantumi. Kwa watu waliotumia simu hii, ilijenga urahisi mkubwa wa mawasiliano bila taabu za teknolojia ngumu.
Profesa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dr. James Kuria, anasema katika jarida la African Journal of Communication Technology la mwaka 2021 kuwa:
“Nokia 3310 ni mfano wa kifaa kilichofanikisha mawasiliano kwa urahisi mkubwa bila kupoteza ubora wa mawasiliano, na hivyo kuwafanya watumiaji kujifunza na kutumia simu bila shida.”
Mbali na kuwa kifaa cha teknolojia, Nokia 3310 pia ilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya watumiaji, hasa katika nchi za Afrika ambapo huduma za simu za mkononi zilianza kupanuka kwa kasi.
Ndani ya kitabu cha The Social Impact of Mobile Phones cha mwaka 2010, Profesa Mark Graham anaelezea kuwa “simu kama Nokia 3310 ziliwezesha watu wa maeneo mbalimbali kuunganishwa kiurahisi, hasa watu waliokuwa mbali na miji mikubwa, na hivyo kuleta mageuzi ya kijamii na kiuchumi.”
Athari hizi zilionekana wazi katika mabadiliko ya maisha ya watu, kuanzishwa kwa biashara ndogo ndogo, na mawasiliano ya haraka ya habari muhimu. Kuna maeneo enzi hizo ilikuwa ni mbali na minara ya simu lakini ukiwa na bar moja ya mtandao basi una uhakika wa mawasiliano.
Ingawa simu za kisasa za smart zimechukua nafasi kubwa sokoni, Nokia 3310 bado ina hadhi ya kipekee katika mioyo ya wengi. Hii imefanya kampuni ya Nokia kuanzisha tena toleo la kisasa la Nokia 3310 mwaka 2017, ikiwa ni ishara ya kuthamini urithi wa simu hii.
Katika mahojiano na The Verge, aliyekuwa mkurugenzi wa Ubunifu wa Nokia, Juho Sarvikas, alisema: “Nokia 3310 ni mfano wa simu ambayo watu waliipenda kwa sababu ya urahisi wake, uimara na maisha marefu ya betri. Tunajivunia kuifanya ionekane tena kwa njia ya kisasa lakini tukihifadhi roho yake.”
Nokia 3310 haikuwa tu simu ya mkononi; bali ilikuwa ni sehemu ya familia zetu haswa ndani ya Afrika, ilikuwa ni alama ya historia ya teknolojia ya mawasiliano, mfano wa ubora, uimara, na urahisi wa matumizi. Kwa mujibu wa wataalamu na wachambuzi wa teknolojia, Nokia 3310 itabaki kuwa mfano wa kifaa kilichofanikisha malengo makubwa kwa wakati wake, na kuachia urithi mzito wa uvumilivu na ubunifu katika tasnia ya simu za mkononi.
Kwa wapenzi wa simu za mkononi, Nokia 3310 inabakia kuwa “simu bora kabisa iliyowahi kutengenezwa,” ni kizazi cha dhahabu cha teknolojia.