Noah inataka kunipa pressure.

King_Villa

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
575
379
Wakuu habar zenu.
Nina kigar changu nimekinunua juzi nilikuwa safi kabisa
Juzi nilikua naelekea moshi nilipofika umbali kiasi na kuingia segera nikaanza kisikia midundo isiyoyakawaida katika gari .(yaani mi midundo mithili Gari inaruka bumzi lakini ni upande Mmoja na bila kukoma)

Nikajipa moyo ngoja nitembee kidogo nikifika segera ntaenda kuicheki .
Hali ilizidi ikabidi nishuke kuangalia, nikakuta tairi zote ziko safi .
Nikahisi labda ni bush zimekufa kutokana na kuingia Kwenye mashimo mitaa ya chalinze kutokana na mvua iliokuwa inaendelea.
nikajipa moyo nikaendelea na safari huku nikitembea taratibu.

Nikiwa karibu kufika segera nikasikia tairi la upande wangu mbele limepasuka afu Gari ikanihamisha upande lakini haikupinduka .
Nikarudisha upande wangu nikabadili tairi na kuendelea na safar.
Nikaona nihairishe zoezi la kupitia segera nikaenda mpaka mitaa ya hedaru ile hali ikarudi tena ..
Lakini nikaona tairi la nyuma upande usio wa dereva limeweka crake afu limevimba .nikanunua tairi jipya na kuliweka

Nikarudi salama hadi dar lakini Leo hali imejirudia tena ila tairi la nyuma lingine nalo limevimba .

Afu Gari imekuwa inayumba sana hasa nikiwa na overtake na speed.

Sasa naombeni ushauri wenu kwa wadau mliokuwa Kwenye tasnia ya magar kwa muda mrefu .

Na kuna tofauti ya .
Wheel alignment na wheel balance.?
IMG_20170309_165422.jpg
 
Pole sana, ngoja wataalamu zaidi waje, ila inaonekana tyres zako zime expires, hizo ambazo kabla hujabaidili. Hiyo ni hatari na pengine ni zile zilikuja na gari, pengine ni kwa mazingira yale ya huko Japan na si kwa matumizi ya bongo land.
 
Tairi hizo ni zilizo kuja na gari? Kama ndio je muda wake wa matumizi umeuangalia? Inaweza kuwa tairi zimechoka ndio maana zinavimba au ni tairi za kutumia kwenye baridi sasa huku kuna joto.
 
Alignment na balance ni vitu viwili tofauti, waweza Google hapa kwa maelezo mazuri zaidi
 
iyo ni wheel balancing tie rod end au bush so matairi yanakua yanalika upande moja
 
Boss tairi hakuna hapo weka kiatu cha ukweli hizo Muda wake umekwisha na shukuru Mungu uwa zinapasuka kwa mpigo. Hizo ni tairi za waya, waya zimeshakatika..... Nunua toyo, brgstone au yokohama na Yana matairi mazuri Sana utayatumia hadi uchoke.... Usihangaike na Kitu kingine badili tairi zote ukitumia gari kwa mwez ukiona inakula upande peleka wakakupimie wheel alignment..... Oil com tazara na kipawa wapo vizuri DSM
 
Tairi hizo ni zilizo kuja na gari? Kama ndio je muda wake wa matumizi umeuangalia? Inaweza kuwa tairi zimechoka ndio maana zinavimba au ni tairi za kutumia kwenye baridi sasa huku kuna joto.
Nimeangalia muda zinaonesha zimetengenezwa 2012
 
Boss tairi hakuna hapo weka kiatu cha ukweli hizo Muda wake umekwisha na shukuru Mungu uwa zinapasuka kwa mpigo. Hizo ni tairi za waya, waya zimeshakatika..... Nunua toyo, brgstone au yokohama na Yana matairi mazuri Sana utayatumia hadi uchoke.... Usihangaike na Kitu kingine badili tairi zote ukitumia gari kwa mwez ukiona inakula upande peleka wakakupimie wheel alignment..... Oil com tazara na kipawa wapo vizuri DSM
OK asante mkuu
 
Mkuu kwa standard ya yaisha yetu jitafutie linglong au champiro tyre tairi nzuri kwa izi za China tatizo litaisha,hapo shida hukubadili tyre zilizokuja na gari zinaonekana mpya lkn zimeexpire na kama umebadili umefunga zile za kichina mf. Good ride zina hilo tatizo la kuvimba na hayo mengine waweza kuta umepanda shm yenye ncha ya kawaida au kijiwe tyre inachanika,badili tyre kwanza.
 
Back
Top Bottom