Mkuu ebu nieleweshe ni kwanini intel amefail kwenye simu wakati ni mkali wa processor za pc
architechture tofauti mkuu
processor za pc ni x86
processor za simu ni arm
hii ni mifumo miwili tofauti, x86 zina nguvu kushinda arm lakini zinatumia sana umeme hivyo vifaa vyake havikai sana na charge.
pia unatakiwa ufahamu kwenye simu sio processor tu, inaitwa soc yaani ina mambo kibao zaidi ya processor. soc ina vitu kama
-processor
-gpu
-modem
-wifi
-blueotooth etc
hivyo qualcomm au mediatek anapowauzia watengeneza simu soc anakuwa hauzi tu processor bali complete package, intel hana hayo mambo mengine hivyo mtu akitumia cpu za intel inabidi mambo kama gpu modem na vitu vyengine akanunue mahala pengine hii inaweza sababisha vifaa kuongezeka bei. zamani intel alikuwa anawalipa watengenezaji vifaa hizo gharama zinazoongezeka ila siku hizi ameacha. unaweza google neno "contra revenue" kufahamu zaidi.
ila naona sasa hivi intel anatengeneza modem kwa ajili ya iphone mpya kama vile iphone 8 na x, na pia cpu zake zinaanza kuja na gpu za amd, hivyo pengine huko baadae na wao wakaja kuwa na soc nzuri.
sema intel si designer tu wa processor bali pia ana viwanda vya kutengenezea processor. na viwanda vyake vinatumia technology za hali ya juu ambazo viwanda vya samsung, global foundries na TSMC bado hawajaweza ifikia. sema viwanda vyake alikuwa anatumia tu yeye mwenyewe bila kuwatengenezea wenzake.
kuna mkataba mpya wa Arm na Intel, kwamba intel atakuwa ana manufacture processor za kampuni nyengine kama mediatek, qualcomm etc. bado hazijatoka ila tusubirie pengine zikawa nzuri kuliko zinazotengenezwa na kina samsung.