Mwezi wa Oktoba 2025 unaweza usibadilike, lakini Tanzania inabadilika na hofu yenu ndiyo inafanya muwakamate viongozi wanaodai haki.
Kejeli zenu hazifuti ukweli kuwa bila tume huru, uchaguzi ni maigizo ya kuwahadaa waliolala na kujifariji kwa kukumbatia barafu kwenye hali joto ya nyuzijoto 40, furaha yenu itayeyuka punde!
CHADEMA si watu wachache, ni dhamira ya mamilioni ya Watanzania wanaotaka mabadiliko.
Mnaweza kudharau sauti zao leo, lakini hamtaizuia kesho yao.