NO AGENDA: Tumsaidie Diamond kuzifikiria vizuri kodi zake za nyumba

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
14,969
2,000
MAPEMA Machi, mwaka huu, mkurungenzi mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi alitoa makisio yafuatayo kuhusu kuingia kwa ugonjwa covid-19 nchini. Mosi, asilimia 80 ya wagonjwa wataumwa na kupona bila kuhitaji matibabu au watameza dawa nyumbani na kupona.

Pili, Profesa Janabi alisema asilimia 15 watalazimika kwenda hospitali, watatibiwa na kupona bila kuhitaji uangalizi wa hali ya juu. Tatu, alitaja ni asilimia 5, ambao wataugua sana, hivyo kulazimik kufungiwa mashine za kupumulia, yaani ventilator machines ili kunusuru maisha yao.

Profesa Janabi alisema ventilators zipo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) na JKCI. Hata hivyo, mashine hizo ni chache mno. Hazitatosha asilimia tano ya watakaoumwa covid-19 nchini na kuhitaji msaada wa kupumua.

Na uchache wa ventilator machines ni tatizo la dunia nzima. Italia ilibidi baadhi ya wagonjwa waliotumia mashine siku mbili wandolewe ili kupisha wapya. Matokeo yake watu wengi walipoteza maisha kwa kukosa msaada wa mashine za kupumulia.

Ilikuwa hivi; mashine zote za msaada wa kupumulia zilikuwa na watu waliozihitaji. Wakati huohuo wagonjwa wengine wenye kuhitaji msaada wa ventilator waliongezeka. Ikabidi waliopo kwenye machine waondolewe kwa mtazamo kuwa angalau walikuwa wameshaambulia. Wawapishe ambao hawajapata kabisa.

Profesa Janabi alitoa takwimu kuwa katika kila Waitaliano 100,000, ni watu 20 tu wakiugua ndio wanaweza kupata ventilators. Alisema na Marekani katika kila watu 100,000 ni watu 34 tu wanaoweza kupata ventilators. Ni kwamba katika watu 100,000, endapo kutakuwa na watu 35 wenye kuhitaji ventilators, mmoja atakosa.
Na atakufa.

Ni kwa takwimu hizo imekuwa ni rahisi ‘kubet’ kuwa maelfu ya watu wanaokufa kwa covid-19 Marekani, sababu ni upungufu wa mashine za kupumulia. Wingi wa wagonjwa ni mkubwa. Hakuna ventilator machine inayobaki tupu. Wagonjwa wapya wanawekwa wapi?

Ni kwa sababu hiyo, Marekani, wadau mbalimbali wamekuwa wakinyooshea mkono kuelekea sekta ya afya, maana mapambano dhidi ya covid-19 yanawategemea madaktari, wauguzi na watumishi wengine wa afya. Hao ndio makamanda walio mstari wa mbele.

Aprili 12, mwaka huu, saa 4 usiku, saa za Afrika Mashariki, saa 9 alasiri saa za Ukanda wa Pacific (PST) au saa 6 mchana kwa Ukanda wa Mashariki (EST), Rapa P Diddy na familia yake walikuwa wanatoa shoo ya kudensi live kupitia Instagram. Shoo iliitwa “Dance A-thon”.

Awali, Diddy na wanaye walitoa matangazo ya shoo ili kila mmoja, panapo wakati akaribie. Lengo la shoo hiyo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwaongezea nguvu wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Marekani.

Ni kampeni inaendelea Marekani kwa sasa. Taifa linashambuliwa kwa kasi kubwa na virusi vya Sars Corona 2, ambavyo vinasababisha ugonjwa wa covid-19. Jana saa 8:15 mchana (saa za Afrika Mashariki), Marekani ilifikisha rekodi ya waathirika 1,131,856.

Idadi hiyo ya wagonjwa wa covid-19 Marekani ni sawa na asilimia 29 ya waathirika wote waliorekodiwa ulimwenguni mpaka sasa. Dunia nzima, hadi jana mchana saa 8:15, wagonjwa wa covid-19 waliorekodiwa ni 3,417,609. Vifo duniani ni 239,900, Marekani ni 65,782.

Kutokana na hali hiyo, ni dhahiri kwa sasa wafanyakazi wa sekta ya afya wanafanya kazi kubwa sana. Ndio maana P Diddy aliona ana wajibu wa kuchangisha fedha kusaidia kuwapa motisha wafanyakazi wa sekta hiyo. Na si yeye tu, ni kampeni yenye nguvu kwa sasa Marekani.

Kipindi hiki watu wengi wanajifungia nyumbani, wanaishi kwa tahadhari kubwa kusudi wasipate maambukizi, kuna watu wanawapokea au kuwafuata wagonjwa, wanawahudumia ili kuokoa maisha yao.

Watumishi wa afya, madaktari na wauguzi, ndio ambao wapo mstari wa mbele kupambana ili kuhakikisha wagonjwa wanapona na hata kama wanakufa, basi maambukizi yasiendelee. Lazima kuwaonyesha kuwa jamii inawathamini kwa kazi kubwa wanayofanya. P Diddy akaenda ‘live’ Aprili 12.

Hiyo ndio hamasa kila mtu anapaswa kuwa nayo. Hata Tanzania, wafanyakazi wa sekta ya afya wanajituma sana kwa sasa. Inatakiwa waungwe mkono. Wanamuziki na watu maarufu mbalimbali, kila mmoja kwa nafasi yake anaweza kufanya jambo kuwapa nguvu wafanyakazi wa sekta ya afya ili wajione wanathaminiwa kwa kujitoa kwao.

Mastaa wakubwa walikwenda sawa na Diddy; LeBron James mpaka Kelly Rowland, Drake hadi Oprah Winfrey, Demi Lovato, Justin Beiber, DJ Khaled na asisahaulike Jennifer Lopez ‘J Lo’, ex-girlfriend wa Diddy.

Wakati Diddy na J Lo wakicheza, J Lo alimtania “nilikufundisha kucheza hivyo?” Nyuma ya J Lo alikuwepo mpenzi wake wa sasa, Alex Rodriguez. J Lo alisema kuwa Alex ni shabiki mkubwa wa Diddy na Mase. Jumla ya Dola 4 milioni (Sh10 bilioni) zilikusanywa.

KWA DIAMOND

Diddy anachangia sekta ya afya kwa sababu ndiko kuliko na changamoto kubwa. Ndio maana mastaa wakubwa duniani waliamua kuungana naye.

Diamond Platnumz, ametangaza msaada wake wa kulipa kodi za nyumba kwa familia 500 katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya COVID-19.

Msaada ni msaada. Yeye ameona hilo ndilo eneo la kusaidia, kwani kuna watu wanakosa kabisa vipato kipindi hiki. Tujiulize, huo ni msaada mwafaka kwa wakati mwafaka?

Yupo mtu atauliza, kipindi cha mlipuko wa COVID-19 na upungufu wa vifaa tiba unawezaje kumlipia mtu kodi ya nyumba badala ya kumnunulia barakoa na vitakasa mikono ili ajilinde na COVID-19?

Unamlipiaje mtu kodi ya nyumba wakati akiugua hatapata mashine ya kumuwezesha kupumua?
Kwa nini Diamond asingenunua ventilators hata mbili angalau zitaokoa maisha ya watu?

Bei ya ventilator moja ni Dola 25,000 (Sh58 milioni) mpaka Dola 50,000 (Sh116 milioni). Ventilators zitaokoa maisha ya watu, kodi za nyumba zitaokoa watu wasikose makazi. Tofauti haionekani?

Chukua maelezo ya Prof Janabi kuhusu uchache wa ventilators nchini. Unganisha harambee ya P Diddy. Jawabu unalo kuwa kipindi hiki misaada ipelekwe sekta ya afya. Kama ambavyo mfanyabiashara Rostam Aziz alivyowezesha kupatikana kwa mashine ya kupumia COVID-19 Zanzibar.

Uganda, Serikali ilizuia wenye nyumba kutoza kodi za pango kipindi hiki. Hata bila tamko la serikali, suala la kodi za nyumba ni la mazungumzo zaidi kati ya wenye nyumba na wapangaji. Wanaweza kuzungumza na kuelewana kwa kuitazama hali halisi. Ventilators, barakoa na vitakasa mikono si vya maridhiano. Lazima viwepo ili kuokoa maisha ya watu.

Credit: LUQMAN MALOTO

Sent using Jamii Forums mobile app
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
14,678
2,000
Ikiwa watu wanawekewa Ventilators hadi siku mbili na wanakufa, Je huu ugonjwa ni kweli unaathiri mapafu na kupelekea vifo au kuna haja ya utafiti zaidi kufanyika kujua athari zaidi, changamoto na utatuzi wake? Izingatiwe kumekua na ongezeko la vifo vya ghafla vikihusishwa na huu ugonjwa.

Ikiwa Ventilator moja inaenda kwa wastani wa bei ya TZS 116 M, nchi kama Marekani au Italia ni ya kuwa na uhaba wa hivyo vifaa kwa hali ya hatari ilivyo kama tunavyoaminishwa? Kwanini wameamua kuidhinisha mabilioni ya pesa yaende kusaidia watu wakati wa hili janga badala ya kujikita kuongeza hizo Ventilator kama unavyoshauri?

Huu msaada anaoutoa ni yeye ameona ndio eneo anaweza kuwagusa watu wa tabaka flani kwa hili janga. Bado kuna wengine watafanya yaliyosalia.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
9,362
2,000
Mawazo ya ajabu mara Chibu, CHADEMA, Mbunge achangie vifaa tiba.

Sisi waTanzania kwanini kwanza tusiibane serikali itumie kodi zetu kwa kununua vifaa tiba vya kutosha kuanzia X-Rays, CT Scanners, ventilators n.k

Kabla ya kufikiria kubana wafanyabiashara, wasanii au kuitisha harambee.

Lazima waTanzania tujenge utaratibu wa kudai kodi zetu zinazokusanywa na serikali kutumika katika maeneo ya Maendeleo ya Afya za watu badala ya kukazania tu Maendeleo ya Vitu SGR, Ndege Atcl n.k
 

grand millenial

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
1,335
2,000
Covid 19 ikipita ndiposa tutakaponunua hizo ventileta pamoja na hizo "sawasandaita" .

《Caprichar o teu sorriso》
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,824
2,000
Kanungila Karim,

Akitoa ventilator Mariah Sarungi atadai mtoto wa kike mwenye mimba kukosa masomo ni tatizo kubwa, msaada wake ungeheshimika kama angewasomesha watoto wa kike.

Mwisho wa siku nsni yuko sahihi? MWENYE PESA YAKE!! Wacha sisi wengine tubaki na hekima zetu zilizojaa kwenye "wongi wa maneno matupu." By the way, umeshachangia kampeni ya kutokomeza COVID 19?

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
7,790
2,000
Sioni tatizo kwa alichofanya Diamond, hata kama angenunua hizo ventiletors si ajabu kwa aina ya watu anaowalenda Diamond wasingenufaika nazo..trust me kuna watu wangepewa kipaumbele..kwenye kuzika wahanga tunaona ubaguzi..

sembuse kwenge kupata huduma! Tusimpangie mtu na hela zake..kwa hali ilivyo ya uchumi watu kodi za nyumba zinawashinda..ni bora awasaidie kidogo na waendelee kujifukiza.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,167
2,000
Waafrika bana ni shida, yaani majungu kwa pesa ya mtu mwingine hayaishi, mpaka bajeti tunampangia doo!!.

Mtoa mada akili finyu sana, domo katoa pesa ya mfukoni kusaidia na hao wa marekani wamechangisha, haikuwa pesa iliyokaa bank, tofauti kubwa hapo.
 

keypass

Member
Dec 2, 2017
54
125
Pesa Ni ya kwake kafanya jambo jema tu,Makazi Ni kitu Cha msingi pia Diamond kalipa kodi wengine watasaidia vingine,ungekuwa unaujua uchungu wa kulala nje kisa kukosa kodi usingeandika hii post.At least mwisho ungempongeza japo kidogo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ludist

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
375
500
Alichofanya diamond ni sawa kabisa kutokana na mapenz yake yalipo, anunue ventilators ili wakatumie tu mawaziri wakat yy anataka kuwagusa watu wa chini?? Mwachen apange matumiz ya pesa zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom