NMB IFAKARA Branch ichukuliwe hatua za haraka kunusuru afya za wateja na wafanyakazi

rjohannes

Member
Nov 11, 2011
11
14
Kwa yeyote mwenye access na mamlaka zinazohusika na kusimamia mazingira na afya makazini, ninaomba asaidie kufikisha taarifa hii. Ni miezi mitatu sasa tangu Viyoyozi (Air Conditioners) katika tawi hili (NMB Ifakara Branch) viharibike na hakuna hatua za makusudi zimefanyika kurekebisha hali hii. Ukiingia ndani ya tawi hili kuna hewa nzito na joto la ajabu ambalo linatokana na msongamano wa wateja pamoja na wafanyakazi. Watu wanavuja jasho na harufu zisizovumilika. Pamoja na hali hiyo, bado mlango wa mbele ambao ungefunguliwa kunusuru na kusaidia hewa kuingia, umekua ukifungwa.

Wateja wamekua wakipiga kelele lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Hili limekua ni eneo hatarishi kwa afya za wateja pamoja na wafanyakazi wa bank hii. Katika tawi zima, ni ofisi ya Manager wa tawi pekee yenye kiyoyozi na hii imechangia kwa yeye kutochukua hatua zozote kurekebisha hali hii. Endapo ikitokea mtu mwenye magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya hewa, ni dhahiri hali itakua mbaya sana.

Naomba mamlaka ziweze kuchukua hatua ili kunusuru afya za watu wanaoingia pale.

Wakuu naomba wenye access muweze kufikisha ujumbe huu mahali panapohusika

Asante
 
Back
Top Bottom