NMB Idara ya mikopo Rushwa imekithiri

Unaweza kujiona Unajua kumbe hujui, vitu vingine bora kukaa kimya kuficha utupu wako.
 
NMB Tunduma kama unataka mkopo jua ya kwao ni ten percent hiyo haina mjadala tena hapo wewe ndio unawabembeleza na kuwapigia magoti.!
 
Nakushauri kama ifuatavyo:
1. Chanzo cha yote hayo ni wewe mwenyewe kukubali kutoa Rushwa ili upate huduma,sheria ya kupambana na rushwa
inakutia hatiani.
2. Benki zote Tanzania zinagombania wateja,kama umetimiza masharti mkopo utapata,
3. Tafadhali wasiliana na ofisi ya kupambana na Rushwa pindi unapodaiwa rushwa kwenye huduma unayostahili
kuipata
 
Nmb karibia wote, mimi niliwahi omba laki tano bado wakaomba chochote, na wana kawaida ya kugomea, kuchelewa kutoa mkopo hadi uwape chochote. Wapo wanaoshirikiana na meneja wao, na pia meneja wengi wana kawaida ya kuficha uchafu unaofanywa na hawa vijana kuogopa kuchafua jina la benki. Ushahidi ninao, jina la meneja ninalo, jiba la loan ofiicer ninalo, jina la teller mwizi ninalo, jina la anayetangaza salio la wateja baa ninalo ila sina pa kulisemea, wote ni ndugu moja. Jirekebisheni, ushindani upo. Haiwezekani mimi naenda bar naambuwa na baameid salio langu halisi. Vijana wa siku hizi sijui tunaenda wapi.
 
Wewe ni muongo hakuna benki inatoa mkopo wa laki tano mpkaka milioni moja, tena eti umeweka hati a nyumba unajua gharama za kusajili hati ya nyumba ili ichukuliwe na bank we ni punga, utakuwa ulienda saccos ya wanyiha wenzio huko mbozi,
Lini mkopo wa laki 5 umefutwa huko NMB? Mkopo wa laki 5 upo achilia mbali hiyo 1m na marejesho yake ni miezi sita na endapo kumbukumbu zangu zipo sawa, marejsho ni sh. elfu themanini na tisa na hela fulani hapo juu!
 
Nenda Ofisi za PCCB hapo jirani, we umekalia chimpumu tu na ikyinde! Na usiwaambie kama ulishatoaga rushwa hapo awali wanaeza kukudaka manake nao sukihizi wananjaa kama polisi!

Ni walewale hakuna tofauti na Polisi au Mahakama.
 
Siwezi kumlaumu sana mdau kwa kulipa hiyo sh. 15,000/-( hela ya mafuta). Kwa mtu asiye ndani ya benki ni vigumu kufahamu kwamba Loan Officers wana fungu la kutembelea wateja. Loan Officers wengi huwa wanawatwishwa wateja mzigo wa kutembelea wakati kwa NMB kuna account inaitwa Business Travelling ambayo ndio inatoa fungu la usafiri kwa Loan Officers. Sasa wanachofanya, watamambia mteja agharamie usafiri lakini wakirudi ofisni wanaandika vocha ya Business Travelling na pesa wanaweka mfukoni!
 
Kama una ushahidi fikisha NMB House/HQ... trust me, baada ya hapo tulia wiki moja au mbili kisha fuatilia kuhusu hao jamaa kama hujaambiwa wamehama kumbe ndo washachinjiwa baharini! Tatizo letu ni kwamba huwa tunalalamika bila kuwa na tangible evidence... lakini pale ilipo, habaki mtu hapo lakini usitoe malalamiko kwa Branch Manager... hakuna kitakachofanyika... si kwamba hao mameneja wanapenda huo uchafu but trust me, kuchukua maamuzi ambayo unajua huyu mtu atafukuzwa kazi si jambo dogo... inahitaji ujasiri na moyo wa chuma hasa ukizingatia kwamba hawa watu wanaishi na kula pamoja!!!
Lakini ukipeleka malalamiko HQ, they don't care coz' huko hawawafahamu personally hao watu (staffs) kwahiyo inakuwa ni kama kumkoma nyani gladi!
 
Unaweza kujiona Unajua kumbe hujui, vitu vingine bora kukaa kimya kuficha utupu wako.
Watu wengine si wa kuwajibu... binafsi nilitaka kumjibu huyo mbwiga lakini nilijua ningemtolea maneno machafu kwahiyo nikaamua kuachana nae na kumpuuza manake anakera zaidi kiwango cha kukera kinachokubalika! Mijitu kama hiyo ni ile mipuuzi iliyopata vikazi vyenye kamshahara nafuu juzi juzi kwahiyo ndo basi tena wanajiona wameshapatia maisha.
 

heri yako wewe ulienazo. Lakini chunhanga ulimi.
 

Hapa ndio mahali pake weka mtandao wote hapa washawishi na wengine.
 
Lini mkopo wa laki 5 umefutwa huko NMB? Mkopo wa laki 5 upo achilia mbali hiyo 1m na marejesho yake ni miezi sita na endapo kumbukumbu zangu zipo sawa, marejsho ni sh. elfu themanini na tisa na hela fulani hapo juu!

katika hiyo lakini tano...elfu hamsini lazima umwachie afisa mikopo, bila hivyo hupati. That is NMB woking value.
 
We pwapwasa acha kuchafua majina ya watu kidwanzi!hiyo 25000 hukuombwa na ndio mana umeshindwa sema sababu ulizokuwa unapewa hadi ukafikiria unazungushwa sana na kwamba wote ni walewale wanaotaka rushwa.
Pili,mikopo ya biashara na ya watumishi inashughulikiwa na maafisa mikopo tofauti,onesha alice ANAHUSIKAJE kwenye kuombwa rushwa mkeo ambae ni mtumishi na wewe ni mfanyabiashara.
Tatu,wewe ni mnafiki sana!wasema TRA uliwatengea kabisa pesa ya rushwa,sasa hapa umekuja kufanya nini wakati ndio 'michezo' yako?
Usivyo na haya unadiriki kutaja hata jina la mtu eti alikuomba unachokiita rushwa ya 15000 ya mafuta,mwaka mmoja na nusu uliopita!!unajielewa wewe kweli?
Jitazame sana wewe pwapwasa!
 
nmb kote hawachekani tawi la kigoma alikuwepo anaitwa oliva mwanaume nami ni mtumishi niliomba m4 alchukua laki 2 urasimu huo upo na bado unaendelea kwani mara nyngne huhusisha hadi branch manager sijui tukimbilie wap jamaani
 

Ungesoma kwa umakini ungejiona wewe ndio pwapwasa.
 
tusifichane idara za mikopo karibu mabenk yote na branches zake zinanuka rushwa shida ya staffs wa NMB wanaomba rushwa hata kwa wasiokuwa na uwezo wa kutoa rushwa
 

Hopeless.
 
nmb kote hawachekani tawi la kigoma alikuwepo anaitwa oliva mwanaume nami ni mtumishi niliomba m4 alchukua laki 2 urasimu huo upo na bado unaendelea kwani mara nyngne huhusisha hadi branch manager sijui tukimbilie wap jamaani

kama mimi sikupi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…