kuna sehemu nimewahi kusoma historia ya vita ya drc wanasema laurent kabila aliwashirikisha rwanda na uganda katika vita ya kumpindua mabutu kwa ahadi ya kuwagawia mkoa wa kivu kuwa ni makazi ya wanyarwanda(kusini) na waganda-kaskazini. Baada ya jamaa kufanikiwa hakutekeleza hiyo ahadi. Jamaa wakaingiza majeshi yao kwa lazima kwa kisingizio cha kuwalinda wanyarwanda. Lengo lilikuwa kuteka ile miji iwe chini yao waendelee kuchimba madini. Baada ya kufanikisha zoezi la kumuua kabila inaonekana aliyepokea kijiti naye akawa mbishi. Inaonekana baadaye walifanikiwa kumshawishi jose kwamba yeye ni mtutsi hivyo anatakiwa kulinda maslahi ya wanyarwanda. Wakakubaliana kusitisha hujuma kwa kuudanganya umma kwamba nkunda amekamatwa na anashikiliwa na serikali ya rwanda. Kagame ni noma.