Njooni Tujadili Hii Kauli "Kanye West Anaweza Kutengeneza CLB, Lakini Drake Hawezi Kutengeneza Donda"

Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
2,049
2,249
Wasaalam wakubwa..I hope mko poa..Here we go,,Kama wiki hivi imepita Kuna albums kubwa mbili zimetoka duniani, Nazungumzia Donda ya Kanye West iliyotoka August 29/2021 pamoja na Certified Lover Boy (CLB) ya Drake iliyotoka September 3/2021...

Albums zote mbili nishamalizana nazo kuziskiliza na zote ziko fire sana..Kwenye CLB ngoma zilizozidi ukali kwangu ni In the Bible akiwa na Lil Durk, Fountains aliyomshirikisha M'nigeria Tems,Too sexy akiwapa shavu Future na Young Thug, Fair trade aliyomweka Travis Scott na Girls want girls akiwa na Lil Baby.. Kwa upande wa Donda nimezielewa zaidi Believe what I say na Hurricane na zingine...

Sasa katika pitapita zangu kwenye mitandao mbalimbali nikakutana na tweet Kuna Chalii anasema "Kanye Anaweza Kutengeneza CLB ila Drake hawezi Kutengeneza Donda" Kwa upande wangu hayupo sahihi Lakini yupo sahihi pia it depends kamaanisha katika contexts/Mazingira yapi..Kwanini??..Nianze na Usahihi wake, Kanye mwaka 2004 alikua maarufu tayari sio kwa kuimba bali kwa kuprodyuza ngoma, Kanye ni Rapper, Producer,Songwriter, Singer Lakini pia ni Mvumbuzi wa Rap sung/sing ,,Ukiiskiliza CLB ni genre ya Rap sung/sing ambayo Kanye ni Mvumbuzi wake na Utayarishaji wa CLB kama walivofanya kina Metro Boomin' Anaweza kuufanya pia..

Lakini kusema Drake hawezi kufanya Donda kwa mantiki ya Donda ni kubwa mnoo kuzidi CLB nakataa asee..Dreeze anauwezo mkubwa sana wa Kutengeneza album Kali kuliko msanii yeyote duniani kwa sasa,,Ntatoa mfano,Mwaka 2018 alitoa album yake ya Scorpion, Records nyingi alizoziweka kwenye album ile amekuja kuzivunja yeye mwenyewe kwenye CLB, Records hizo ni siku ya kwanza tu Scorpion ilipata streams zaidi ya Million 132 kwenye Spotify,, Lakini Kanye baada ya kutoa album yake amekua msanii wapili,sio kaivunja record ya Drake ila ni wapili pamoja na kufanyiwa listening party sehemu tatu tofauti na promotion nyingi Mara afute verses za wakali kama DaBaby,Chris Brown nk. Lakini hajaifikia Scorpion, Lakini Drake katoa CLB kaivunja record yake mwenyewe ya kuskilizwa zaidi ndani ya siku moja kwenye streams services, Na kaivunja hiyo record ndani ya masaa10 tu...

Kwahiyo huyu chalii wa Twitter yuko sahihi na yuko wrong pia ni kutokana tu na yeye atajitetea vipi au atasimamia upande upi??..Tuache tabia ya kumchukulia poa The Champaignpapi huyu katoka sayari nyingine...

Karibuni Tujadili hili Wadau

@NgarenaroBoy
View attachment 1931950
 
Sijaelewa chochote baba. Nialiachanaga na ngoma za majuu baada ya kizazi cha kina Dre, Snoopy, Buster, Coolio Nas, Big Pac n alike.

Kwa sasa nasikilozaga ngoma zao tu. Na zile za kibongo za jazz band kama mlimani park, nginde. Msondo, kamanyola, pambo mto, mdekule, super bomboka ya marijani.

Kule zaire ya Mobutu seseseko. Kina Verkisy, Mpongo love, Veve, Lipualipua na kina Roucherou, Lwambo. Hizo ndio ngoma zangu za kusikiliza kwa sasa.
 
Binafsi "7am On Bridle Path" ndiyo track pekee niliyoikubali kwenye album ya Drake.

Kanye album yake ni bora zaidi: "Hurricane", "Ok,Ok" na "Junya" ndiyo best tracks kwangu.
 
Binafsi "7am On Bridle Path" ndiyo track pekee niliyoikubali kwenye album ya Drake.

Kanye album yake ni bora zaidi: "Hurricane", "Ok,Ok" na "Junya" ndiyo best tracks kwangu.
Fafanua bro,,Criteria zipi zinaifanya Donda iwe Kali kuliko CLB?
 
Sijaelewa chochote baba. Nialiachanaga na ngoma za majuu baada ya kizazi cha kina Dre, Snoopy, Buster, Coolio Nas, Big Pac n alike.

Kwa sasa nasikilozaga ngoma zao tu. Na zile za kibongo za jazz band kama mlimani park, nginde. Msondo, kamanyola, pambo mto, mdekule, super bomboka ya marijani.

Kule zaire ya Mobutu seseseko. Kina Verkisy, Mpongo love, Veve, Lipualipua na kina Roucherou, Lwambo. Hizo ndio ngoma zangu za kusikiliza kwa sasa.
Hahah sawa Mzee,,Shikamoo
 
Huyo jamaa ni chizi, kuna interview aliongea kwamba yeye ndio the one and only master. He's going to buy the entire Earth and be the King. Halafu anaongea yupo very serious hata apepesi macho.
 
Huyo jamaa ni chizi, kuna interview aliongea kwamba yeye ndio the one and only master. He's going to buy the entire Earth and be the King. Halafu anaongea yupo very serious hata apepesi macho.
Hahah jamaa sometimes umeme waga mdogo
 
Japokuwa sielewi kama kuna ukribu wa kivile kati ya Kanye na Drake ila najua hizi album zimesetiwa kimkakati kabisa kwa lengo la kuwa na mauzo mazuri sokoni kwa pande zote mbili, kwanza kabisa wasambazaji wakuu wa hizi album kama kawaida ni Universal Music Group chini ya makampuni yao mawili ambapo Republic Records inasambaza CLB wakati Def Jam Recordings Inc,LLC inasambaza DONDA..Kwanini nasema hizi album zimesetiwa kimkakati hapo ni kwamba mikakati yenyewe ni kuhakikisha kwamba hizi album zinacreate attention duniani ndio maana unaweza kuona zimepishana kidogo releasing date,na kingine kuna matukio yanatokea unajua kabisa haya yamepangwa mfano Kim Kardashian mke wa zamani wa Kanye aliscreeshot na kuweka insta story akisikiliza album ya Donda ikiwa muted while muda huohuo anasikiliza CLB in full voice kingine nilichoona hizi album zipo kimkakati zaidi na si kiushindani ni pale ambapo Drake alinunua BILLBOARDS(Mabango ya matangazo) hili kupromote album yake katika miji mingi kama Atlanta,New York,Chicago,Memphis,New Orleans ambapo sehemu hizohizo zilizowekwa mabango ya Drake Kanye akaja kuweka matangazo yake ya DONDA...
 
Kanye ni exceptional, kitu anachofanya hakuna mtu anaweza kufukiria kufanya.

Rock Ross hajataka kumumunya maneno amesema 'YE ni genius' wa hicho anachokifanya.

Rosie yeye anataka uweke pesa mezani tu, anaweza kusema au kumtungua mtu wowote kwa lyrics vile unavyotaka wewe. Sikiliza Intanglement aliivyoongea kuhusu Jada na Will. Ndio maana hata Diamond alivyompa pesa tu ngoma ilikaa sawa. Believe me,Kanye is crazy. Na utajiri wake wote lakini bado haaminiwi kuwa na watoto wake peke yake
 
Huyo jamaa ni chizi, kuna interview aliongea kwamba yeye ndio the one and only master. He's going to buy the entire Earth and be the King. Halafu anaongea yupo very serious hata apepesi macho.
What do you, espect...homie with the KARDASHIAN...Its a curse, ukiyadeti hayo mademu ni kama laana, lamar nusu awe chizi he became a crack head, tyga ndio alipotea kwenye mziki kbsaa alishazama.....
 
Rosie yeye anataka uweke pesa mezani tu, anaweza kusema au kumtungua mtu wowote kwa lyrics vile unavyotaka wewe. Sikiliza Intanglement aliivyoongea kuhusu Jada na Will. Ndio maana hata Diamond alivyompa pesa tu ngoma ilikaa sawa. Believe me,Kanye is crazy. Na utajiri wake wote lakini bado haaminiwi kuwa na watoto wake peke yake
Kanye ni genius wa hicho anachokifanya. Hakuna anayeweza kufikiria kuwa anaweza kufanya anachofanya Kanye na ku-make a lots of money as he do.

Maswala ya ukichaa wake na sijui maswala ya kukaa na watoto ni mjadala mwingine huko ambao hauna mahusiano yoyote na kazi zake tunazojadili hapa.
 
What do you, espect...homie with the KARDASHIAN...Its a curse, ukiyadeti hayo mademu ni kama laana, lamar nusu awe chizi he became a crack head, tyga ndio alipotea kwenye mziki kbsaa alishazama.....
Ben Simmons wakati yuko rookie year NBA alikuwa moto wa kuotea mbali .

Leo anatukanwa Sana na anaonekana garasa watu hawampendi tena Kama zamani (alipita na Kendall Jenner)

Kim alipita na Reggie bush(kabaki jina) Ray J(Sijui yuko wapi, khris humphiries ( aliishia wapi sijui)
Christiano. Ronaldo sijui alioga maji ya bahari gani angechonga mzinga kwa kim angabaki historia

Tristan Thompson kaisha kabisa kabaki kutembelea nyota ya ubingwa wa NBA akiwa CAVs(alipita na khole)

Devin booker nasikia anahit **** ya Kendall so unajua alivyokuwa Moto msimu huu ulioisha Sasa sikilizia msimu ujao lazima aflop mbaya na majeruhi juu.

Inaonekaana Kyle hana kimavi mbona Travis scotie yuko poa tu
 
Hio familia kwa kimavi noma, yan Simmons hata statistics zake saivi haziko poa, Tristan Thompson kabaki na ubishoo tu...mganga wa CR7 ni nux...hata Drizzy alipiga kim akasepa nae bahati yake...
 
Hio familia kwa kimavi noma, yan Simmons hata statistics zake saivi haziko poa, Tristan Thompson kabaki na ubishoo tu...mganga wa CR7 ni nux...hata Drizzy alipiga kim akasepa nae bahati yake...
CR7 ni nyoko.. ye mwenyewe ni nuksi tosha
 
CLB sijaisikiliza.

Donda nimeisikiliza, nimeipenda kwa sababu ngoma karibia zote zinamtukuza Mungu.
 
Back
Top Bottom