Njoo tuwekeze kwenye biashara ya mkaa kijana mwenzenu sina mtaji

Biashara ya kwenye daftali tumewekeza 300000 tumepata 1,500000 tuendelee kuijadili hii faida tuifanyie nn huku huku ktk daftali lkn ukichukua hiyo pesa cash ukaenda kufanya hiyo biashara usitegemee kupata faida hiyo kamwe.
Naheshimu mawazo yako sikupingi lakini ww Kama kijana inabidi uonyeshe uthubutu ,utakuja kuhtajik zaid iwe kweny familia au jamii pia
 
Hasara ya biashara hii ya mkaa inatokana na:
  • Ushuru mkubwa toka maliasili kwa kila gunia la mkaa,
  • Gharama ya usafirishaji toka mkoa ulipochoma kwenda mji utakaouza,
  • Gharama ya usafirishaji toka porini ulipochoma mpaka eneo ambalo gari litaweza kufika kupakia mzigo ( hapa utatumia pikipiki au trekta),
  • Gharama ya Uchomaji huo mkaa na upakiaji kwa kila gunia,
  • Gharama ya Magunia yenyewe
  • Gharama ya kuzuia kukwamishana, viongoz wa vijiji, mageti ya maliasili nk.
Mwisho wa siku unapata faida kiduchu au hupati kabisa kitu...
 
yupo dada mmoja nae pia aliacha akahamia kwenye nguo amekuwa maarufu maarufu
ila anasema hawezi kurudia tena biashara ya mkaa
sijui kuna nini humo
 
Mkuu unachosema mi naamini cause kuna ndugu yangu alishafanya Sana iyo biashara akafikia adi kununua Scania yake.Hadi mda huu tunaongea Hana hata mia,na ashukuru alijenga.Inasadikika ni biashara kama ya madini yaani imekaa kudhurumiana Sana kuanzia mkulima ,mfanya biashara hadi dalali.Mi nahisi labda Kwa sababu miti mingi wanayokata ni makazi ya mizimu
 
Mkuu ukiona kuna biashara muhindi haifanyi, basi usifanye..

hakuna muhundi anauza mkaa hata umpe msitu bure avune na achome mkaa..

biashar ya mkaa itakupa hela, pia itakufilisi na nimeona wengi sana
Sumri anafanya hii biashara Chunya huko. Usitishe watu. Au Sumri ni mmang'ati?
 
Sumri anafanya hii biashara Chunya huko. Usitishe watu. Au Sumri ni mmang'ati?
kwny baadhi ya principles kunakuwaga na exceptionals pia, 0.001% ya waliofanikiwa katika hiyo biashara ni sawa na sefuri tu.

Btw, Sumry anaendeleaje now? Yale mabasi yake siyaoni tena Dar, nini shida?
 
Aliacha nadhani watoto wawili. Sasa msimamizi mkuu amefungua shamba la mahindi Songwe ndo huko anatoa mkaa balaa
Anatafuta mtaji hapo, pesa atapeleka kwenye mabasi akirudi kuwa tajiri kuliko baba yake mtasema ni mkaa, kumbe target ni mkaa kuboost mtaji wa biashara yao ya asili ya mabasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…