Njoo tuwekeze kwenye biashara ya mkaa kijana mwenzenu sina mtaji

Dah, ni biashara nzuri tatizo niko mbali yanj Zenji..mpaka nivuke maji...sasa hata nikiingia ubia na wewe mara moja kunitia changa la macho😅
Ni kweli ndugu mwenyew nitapenda mtu tutakayekuwa jiran zaidi ili aweze kuona na changamoto zake ili lawama zisitokee Kama ukiwa uko fresh karbu siku moja Kama nikianza nitakujulisha uje ujifunze zaidi
 
Habari za kazi wakubwa

Biashara ya mkaa Ni biashara ambayo inawez kukutoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ,hivo kwa fursa hyo napenda yeyote ambaye atakuwa 💯
Hiyo miti anakuuzia nani halafu huko polini maliasili hawaji?
 
Kuna mtu anauza mkaa
Anafata mkoani huko Kwa malori
Gunia 700 au kwake kitu kidogo sana

Cha kushangaza kila siku ana shida
Kila siku anauza nyumba anayoishi..
Anaenda Jenga ingine kabla haijaisha kapata tena shida anauza...


Niliwahi sikia biashara ya mkaa kuna aina ya miti kama inaku laani hivi...unapata shida zisizo isha..unaposhiriki kukata na kuchoma hiyo miti...

Siamini but then again....

Mkuu ukiona kuna biashara muhindi haifanyi, basi usifanye..

Hakuna muhundi anauza mkaa hata umpe msitu bure avune na achome mkaa..

Biashar ya mkaa itakupa hela, pia itakufilisi na nimeona wengi sana
 
Mkuu ukiona kuna biashara muhindi haifanyi, basi usifanye..

hakuna muhundi anauza mkaa hata umpe msitu bure avune na achome mkaa..

biashar ya mkaa itakupa hela, pia itakufilisi na nimeona wengi sana
Kivipi yani...fafanua! Halafu hao wahindi ndo nani mpaka wawe ndi kigezo chako katika biashara au ujasiriamali?
 
ukifika nchi, mkoa ama eneo ambapo hamna wahindi wanafanya biashra, tambua hilo eneo au nchi halifai wewe kufanya biashra
Sawa, ila wahindi sio watu wa biashara za jasho sana kama hizi za makaa..wao biashara zao ni kwenye maduka ya bidhaa sana sana.
 
Mkuu ukiona kuna biashara muhindi haifanyi, basi usifanye..

hakuna muhundi anauza mkaa hata umpe msitu bure avune na achome mkaa..

biashar ya mkaa itakupa hela, pia itakufilisi na nimeona wengi sana
Umenchekesha Sana. Kuna rafk yangu mtu mzima kidogo nilimfata ushari nataka nihamie kampuni flani. Akaniambia hiyo kampuni nnayotaka kuhamia imejaa wahindi kibao sasa nnachosubiri kuhamia ni nini. Akanshauri Acha ujinga nenda huko.
🤣🤣🤣🤣 yaani kigezo wwahindi.
 
Umenchekesha Sana. Kuna rafk yangu mtu mzima kidogo nilimfata ushari nataka nihamie kampuni flani. Akaniambia hiyo kampuni nnayotaka kuhamia imejaa wahindi kibao sasa nnachosubiri kuhamia ni nini. Akanshauri Acha ujinga nenda huko.
🤣🤣🤣🤣 yaani kigezo wwahindi.
wapo kama nzi wale wakijani, wakihisi harufu ya hela lazma wajazane..
uzuri wao, huambiana wao kwa wao tofauti na sisi rangi ya mkaa
 
Habari za kazi wakubwa

Biashara ya mkaa Ni biashara ambayo inawez kukutoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ,hivo kwa fursa hyo napenda yeyote ambaye atakuwa vizuri tuwekeze pamoja katika mchanganuo huu lakin kwa upande wangu nitawekeza nguvu zaidi (yaani Sina mtaji).

Update..
💢Biashara yetu hii haitahitaji kibali chochote kwa sababu hatutauzia mijini wateja wetu wote wanafwat polin tunapochomea, na wateja wa huku wanakuja na mifuko ya kujazia wao wenyewe..



Kwanza tujue Nini kinahitajika ili kupata matokeo mazuri..mkaa tutakao choma hapa sio mti Poli yan ule mgumu tutachoma wa kawaida,
💢kununua miti kwa wastan miti wanaanza kuuza tsh laki mbili eneo linakuwa kubwa la miti.
💢Gharama za ukataji miti hyo kwa ajili ya kupanga zinagharimu elfu hamsin.
💢Gharama za upangaji tanuli hlo la mkaa tutatumia watu wawili ambao nitasaidiana nao na kwa siku tutawalipa tsh elfu sita maana inaweza tumia siku mbili sawa na elfu ishirini na nne.
💢💢Kwa ujumla Gharama zitakazo maliza maandalizi Ni tsh laki mbili na elfu Sabin na nne ,hivo inabidi tufanye makadilio kwa sababu tupo Poli iwe laki tatu kamili...

Matokeo baada ya kupanga tanuli na kuchoma
💢 Kwa miti tutakayoipata hyo la laki mbili yaweza kutoa tanuli tatu za uhakika tanuli moja ambalo hupangwa na kutoa gunia hamsini hivo kwa tanuli tatu tutakuw na gunia 150. Na gunia moja huku huku polin linauzwa tsh elfu kumi hyo bei anakuja kuchukua anayejumua hvo huja pamoja na mifuko yake hapo sisi hatutahusika kwa Gharama yeyote.
💢💢 Hivo baada ya kuwekez tsh laki tatu .matokeo yake baada ya uendeshaji tunapata tsh million na laki tano

💢💢 na kazi za uchomaji hutumia siku Saba kwa tanuli la gunia hamsini
💢💢💢💢💢
Kama upo tayali ndugu karibu tuwekeze Mimi nitatoa nguvu zangu(Sina mtaji) nawe mwenzangu Kama upo vizuri kifedha wekeza

💢💢💢
Nipo mkoani Njombe hivo kazi hizo tutazifanyia Sana huko maan itakuwa rahisi kwa upatikanaji wa miti
💢💢💢 Karibu pm tuyajenge

Maoni ya Wachangiaji💯
Utafanyia mkoa gani?
 
Ni kweli ndugu mwenyew nitapenda mtu tutakayekuwa jiran zaidi ili aweze kuona na changamoto zake ili lawama zisitokee Kama ukiwa uko fresh karbu siku moja Kama nikianza nitakujulisha uje ujifunze zaidi
Binafsi ninakuunga mkono Mimi nipo mafinga nitakutafuta tufanye mapatano
 
Back
Top Bottom