Njombe: Yanayojiri kwenye Mkutano wa hadhara wa CHADEMA

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,788
218,420
Wakuu, Natanguliza Salamu na baada ya hapo naingia moja kwa moja kwenye hoja .

Kama tulivyosema awali, mchana huu ni zamu ya Njombe Mjini ambako Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mwamba mwenyewe Freeman Mbowe, Mtemi Isike, Laingwanan ama Ustaadh Aboubakar watahutubia.

Haya yalikuwa maandalizi ya eneo la mkutano mida ya saa 2 asubuhi.

FB_IMG_1677501328896.jpg
FB_IMG_1677501321061.jpg

Kwa Muhtasari tu ni kwamba , Unyama waliofanyiwa viongozi wa Chadema Njombe na ile serikali ya kinyama ya awamu ya 5 , hauelezeki , mpaka nina andika haya wanachama na viongozi kadhaa wa Chadema wako jela kwa makosa ya uongo , akiwemo diwani wa zamani wa eneo hilo Kijana George Sanga na wenzake , ambao wamebambikwa kesi ya uongo ya mauaji , hawa wako jela kwa zaidi ya miaka miwili

Just Imagine , Mtu anasingiziwa kesi nzito kama hii kwa sababu ya Udiwani tu , tena udiwani wenyewe wa maparachichi ya Njombe , Angalieni ukatili huu , hivi unawezaje kuwasamehe au kuwaombea watu waliofanya haya ?

Rose Mayemba mara kadhaa amenusurika kuuawa kwa kosa la kuwa kiongozi wa Chadema , leo kama kweli mbinguni kuna moto basi nina hakika kuna mtu kabaki majivu matupu .

Ninawaomba Viongozi wa Chadema kabla ya Mkutano watenge japo dk 5 za ukimya kuomboleza waliouawa , kuteswa , kutekwa na kufungwa jela kwa kesi za uongo

Basi kama kawaida yule mwandishi wenu Erythrocyte atawaletea kila kinachojiri

Usiondoke JF

===========
UPDATES :

Hatimaye Msafara wa Chadema umeingia Mjini Njombe na kulakiwa na Umati wa watu kwa maelfu .

Freeman Mbowe apewa heshima ya Uchifu na Wazee.
 
ma waliofanyiwa viongozi wa Chadema Njombe na ile serikali ya kinyama ya awamu ya 5 , hauelezeki , mpaka nina andika haya wanachama na viongozi kadhaa wa Chadema wako jela kwa makosa ya uongo , akiwemo diwani wa zamani wa eneo hilo Kijana George Sanga na wenzake , ambao wamebambikwa kesi ya uongo ya mauaji , hawa wako jela lwa zaidi ya miaka miwili
Kibatala umeyasikia haya ya Wana CHADEMA?

Haya maridhiano ni kweli ya Gredi?

Hatuwezi kuwa wachagizaji wa sheria na haki wakati huo huo tunapendekeza kiaina sheria zipumbwazwe, kupuuzwa na kukandamizwa.

Watolewe jela moja
 
Amen
 
Mjitahidigi kuwalipa waendesha bajaji na bodaboda mnaowakodi maana wanawalaani Sana kwa utapeli wenu maana wamesema kuwa mtakuja Tena na watawaonyesha kazi ,ili mjuwe kuwa utapele mwisho ufipa mnakotafunia Ruzuku za chama kwa miaka mingi
 
Propaganda ya kijinga sana
 
Hotuba za viongozi wa CHADEMA hapo Njombe ni miongoni mwa Hotuba bora zaidi. Tangu nimeanza kufuatilia hii Mikutano ya CHADEMA, kwakweli jamaa wamefanya improvement kubwa sana. Halafu nilikuwa sijawahi kumsikia huyo ndugu anaitwa Masonga aliyekuwa mgombea Ubunge Njombe, kumbe jamaa nae mzima sana kwenye Jukwaa. CHADEMA imekomaa sasa ipewe tu Dola kama Dr. Slaa alivyothibitisha huko Karatu. Wale MACHAWA msinipige mawe, haya ni maoni tu!
 
Masonga wamejaribu mara kadhaa kumuua lakini ikashindikana , alifungwa jela pamoja na Sugu , ndiye organiser mkuu wa kanda ya Nyasa , alikuwa Katibu wa Kanda hiyo kabla ya kuhamishwa
 
Mjitahidigi kuwalipa waendesha bajaji na bodaboda mnaowakodi maana wanawalaani Sana kwa utapeli wenu maana wamesema kuwa mtakuja Tena na watawaonyesha kazi ,ili mjuwe kuwa utapele mwisho ufipa mnakotafunia Ruzuku za chama kwa miaka mingi
Muulize Aeshi na maigizo aliyofanya Sumbawanga na hao madereva Bajaj. Au huna namba yake nikutumie?
 
Masonga wamejaribu mara kadhaa kumuua lakini ikashindikana , alifungwa jela pamoja na Sugu , ndiye organiser mkuu wa kanda ya Nyasa , alikuwa Katibu wa Kanda hiyo kabla ya kuhamishwa
Jamaa yupo vizuri sana. Si kwenye uongeaji tu hadi kichwani yupo vizuri. Nilikuwa sijawahi kabisa kumsikia akiongea japo jina siyo geni. CHADEMA ina vijana wengi wazuri sana kwenye SIASA.

Kule Mbarali nako naona Liberatus hatanii. Kasafiri toka Marekani anakoishi kuja tu kwenye mkutano wa Jimbo lake. Huu si utani..
 
Chadema ina vijana wazuri mno ! Sasa mimi ndio balaa zaidi , hivi karibuni nimepangiwa kuzungumza Jukwaani , sasa ndio watu watajua hatutanii
 
Upo vizuri Mkuu, hata uandishi wako unaonesha. Japokuwa kuna wakati huwa unatupiga kamba za hapa na pale kwa kuongezea chumvi kunogesha taarifa zako ila upo smart.

Kigezo kimojawapo cha wewe kuwa smart ni pale unapoendelea kuwa mpole hasa wapinzani wako wanapoweka comments za kuudhi kwenye taarifa zako. Na sidhani kama ulishawahi pigwa ban humu japokuwa upo active sana hapa.

Inaonesha umeelimika na una exposure pia.!

Swali la kizushi, Je utahutubia mkutano upi na lini? Japo tunatumia anonymous ID humu ila ukitaja mahali na siku naweza kufatilia mkutano mwanzo mwisho huenda nikakufahamu. Ha ha Haa!
 
Ni kanda ya Pwani , ila sijui ni lini , na ni Dar es Salaam , kuhusu ban nimewahi kupigwa ban 2 za uonevu , lakini si kwa kumtukana mtu bali niliambiwa picha ya nembo ya ccm niliyoiweka ilikiuka sheria za jf , na kwa vile jf hakuna kujitetea nikaishia kuumizwa
 
Back
Top Bottom