Njombe: Mwalimu Mkuu ahukumiwa kwa kumjeruhi mwanafunzi kwa fimbo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
d4d52031cd5a444e9193e97c9c411fe3

Na Amiri kilagalila, Njombe

Mahakama ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imemhukumu mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Iwale Mwl.Steven Mahenge kulipa faini ya shilingi Laki 5 au kwenda jela miezi minne kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi mwanafunzi wake anayesoma darasa la 7 mwenye umri wa miaka 13 ambaye jina linahifadhiwa.

Pia Mahakama hiyo imetoa amri ya mshtakiwa kulipa fidia ya shilingi Laki 1 kwa mlalamikaji kutokana na kosa alilomtendea lililopelekea kudhurika mwili wake.

Hakimu mkazi wa mfawidhi wa mahakama hiyo John Mpitanjia amesema shitaka hilo ni rufaa iliyokatwa na mlalamikaji kutoka mahakama ya Mwanzo Matamba baada ya kuona kwamba hakuridhika na hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo ya mwanzo.

Amesema katika shauri hilo baada ya mahakama kupitia mwenendo wa kesi iliyosikilizwa na mahakama ya Mwanzo Matamba, imebainika alishtakiwa chini ya kifungu ambacho hakikuwa sahihi kwa mujibu wa kifungu cha 241 cha sheria ya kanuni ya adhabu 16 kama kilivyofanyiwa marejeo 2002, mshtakiwa akikutwa na hatia alitakiwa kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 5 jela.

Hakimu Mpitanjia amesema kwa mujibu wa kifungu cha 21B cha Sheria ya Mahakama ya Mahakimu, amebatilisha adhabu iliyotolewa na mahakama ya mwanzo Matamba kumhukumu Mwalimu huyo kulipa faini ya shilingi laki 1 ama kwenda jela miezi miwili pamoja na kumlipa mlalamikaji fidia ya shilingi 87,000.

Akijitetea mbele ya Mahakama hiyo kabla ya hukumu kutolewa, Mshtakiwa huyo Mwl. Staven Mahenge amesema kwa kuwa ni kosa lake la kwanza anaomba mahakama hiyo imsamehe na kumuachia huru kwa kuwa anafamilia inayomtegemea na wanafanya kazi kwenye mazingira magumu.

Mpitanjia ametoa hukumu hiyo kwa mshtakiwa na kusema rufaa iko wazi kwa upande wowote ambao haujaridhika na hukumu hiyo aliyoitoa na wanatakiwa kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia leo.

Hata hivyo Baba Mzazi wa Mtoto huyo Majaliwa Chawe nje ya mahakama amesema hajaridhika na hukumu hiyo huku akieleza kukata rufaa upya kutoka na udogo wa adhabu hiyo huku yeye akiwa ametumia ghalama kubwa kuanzia nauli na matibabu ya mgonjwa.

Februari 18, 2020 majira ya saa tatu asubuhi katika shule ya msingi Iwale wilayani Makete mkoani Njombe mshtakiwa alimpiga kwa fimbo na mateke mwanafunzi wake (jina linahifadhiwa) na kupelekea kumjeruhi kwa kumvunja mkono wake.
 
Daa hatari mwalimu kajeruhi akiwa kazini adhabu ndo hiyo Kuna idara ZINGINE zinaua komplitili na hawafanywi chochote
 
Ila walimu na nyie sijui mnavutaga bangi sometimes?

Hivi ukiachana na litoto la watu likawa jinga utapungukiwa nini?

Mwenzenu alikula kifungo cha maisha hivi hivi ila bado mnaleta bangi tu eti?
 
hv ukiachana na litoto la watu likawa jinga utapungukiwa nini ?

Siungi mkono adhabu Kali.

ila jua uyo mtoto akiachwa pia atalaumiwa mwalimu...sasa unaposema atapungukiwa nini sijui unamaanisha nini ??
 
Ila walimu na nyie sijui mnavutaga bangi sometimes?

Hivi ukiachana na litoto la watu likawa jinga utapungukiwa nini?

Mwenzenu alikula kifungo cha maisha hivi hivi ila bado mnaleta bangi tu eti?
Ajali kazini aisee, hutokea bila kukusudia
 
Back
Top Bottom