Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Ukweli ni kwamba kwa dunia ya sasa ili kufanikiwa , inatakiwa kutumia akili na ushawishi mwingi huku ukitumia nguvu kidogo sana au usitumie nguvu kabisa. Ukifanya kinyume chake yaani kutumia nguvu za tembo na ushawishi sungura huwezi kuwa na mafanikio ya maana sana.
Angalau moja ya mambo ya kutia moyo, sasa tunahama tena kutoka siasa za msuli na kwenda kwenye siasa za kutumia akili na kujenga ushawishi.
Kutoka 'wewe balozi nakupa mwezi, ole wako nisione watalii' kana kwamba wanafungwa na kamba na kuletwa kibabe, hadi kwenye 'kushirikiana kwa pamoja kuwashawishi watalii kwa nini waje kwetu'.
Kutoka kuwatisha wenye mawazo tofauti hadi kukaribisha mijadala.(Japo taratibu taratibu kwa sababu 'too rapid transformations may lead to cracks')
Kutoka kuumizana sababu ya mitizamo hadi 'Njooni tuzungumze'
Kutoka 'forced economy' hadi 'Influenced economy' n.k
Maswali yanayoulizwa sana:
1. Kwa nini suala la katiba mpya halishughulikiwi kwa haraka? hili ni suala ni sensitive na linalohitaji timing na kutuliza vichwa na sio emotions na kukurupuka. Hivyo pamoja na umuhimu wake, Halihitaji kushughulikiwa kwa kukurupuka kwani uwezekano wa kukwamia njiani unakuwa ni mkubwa kama ilivyotokea hapo awali.
2. Ushirikiano mkubwa na nchi zilizoendelea (ni mabeberu?). Kwanza kuwaita wenzako mabeberu ni jambo lisilofaa, kama mwenzako beberu wewe ni nini? Hakuna namna nchi zenye uchumi mdogo zinaweza kuendelea bila kushirikiana vyema na waliofanikiwa. Matajiri sio maadui zetu bali ni development partners, hivyo tunaenda vizuri na kwenye muelekeo sahihi.Hata mtaani kwako usichukie matajiri bali shirikiana nao nawe utajirike. Kuwachukia ni roho ya uchawi ambayo nawe haikusaidii.
3. Nchi tajiri hazitupendi: Hii ni atitude ya ovyo kweli. Haya, hawatupendi sisi tunawapenda? ni kiashiria gani kinachoonesha kuwa wao hawatupendi ila sisi tunawapenda? ok wanatupa vitu kibao,sisi tunawapa nini? hatujui kuwa uhusiano ni kunufaishana na kama humnufaishi rafiki yako wewe rafiki mzigo? (na ni bora uwe unamnufaisha rafiki kuliko wewe kusubiria kunufaishwa tu, huo nao ni aina flani ya uhuni) so ni suala tu la kuangalia tunasaidiana vipi lakini hawa ni marafiki 'development partners'. Dhana ya ubeberu ilikuwa ni hila na tuliikataa toka mwanzo.
Kwa kuhitimisha, tunaenda kwenye muelekeo mzuri, siasa inayofanyika sasa ndio siasa ambayo watu wenye busara, uungwana na akili timamu wamekuwa wakiitamani wakati wote, siasa ya kuongea, kubadilishana mawazo, kufanya kazi pamoja, kushawishiana na sio siasa za msuli na kuumizana.
Hivyo kuna mema mengi yanakuja kwenye nchi hii. Tuendeleeni kuwa positive.