Habari zenu wadau, kuna rafiki yangu wa karibu ameniomba ushauri wa jinsi gani atagundua kama mchumba wake anatumia mtandao wa 0713.. kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba anatarajia kufunga ndoa na huyo mchumba hivi karibuni lakini kuna wapambe ambao wamemuuma sikio kwamba kabla ya kuwa na mahusiano na huyo mchumba hapo mwanzo huyo binti alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bwana mwingine ambaye anasifika kwa mchezo huo mchafu wa kuruka geti. Sasa rafiki yangu yuko njia panda kwani hana uhakika kama ni kweli mchumba alikuwa akifanyiwa hivyo au la, na pia ana hofu akiingia ktk ndoa atashindwa kumridhisha kwani yeye sio muumini wa hiyo kitu, karibu tumshauri kama kuna namna ya kumtambua mtu anayetoa ndogo kwani kwa kumuuliza tu kwa maneno anajua huyo mchumba hawezi kukubali