Njia zinazoweza kukusaidia kuishi bila mkazo (stress)

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Kuacha kazi na mambo ya ofisi ofisini. Ikiwa utakuwa nyumbani ni vyema kushiriki na familia kazi za nyumbani & michezo. Kulingana na @CDCgov kati ya 26% hadi 40% ya wafanyakazi wanadai kazi ndio kitu kinachowapa mkazo.

Kusinzia/kulala masaa yasiyopungua nane. Shirikia la Saikolojia la Marekani @APA linadai mtu asiposinzia vya kutosha anakuwa mwepesi wa hasira hivyo kuongeza mkazo (stress).

Kuwa nje ya nyumba na kutembelea mazingira mazuri ni njia ya haraka ya kupunguza mkazo (stress) na kumfanya mtu kuhisi vizuri. Watafiti wanadai njia hii inaweza kuwasaidia wagonjwa wa moyo na saratani kuishi umri mrefu zaidi.

Fanya mazoezi kwa ukawaida. Watafiti kutoka @karolinskainst wamebaini mazoezi hufanya mabadiliko kwenye misuli ya mifupa na kusaidia mwili kuondoa mkazo (stress) unaoweza kuathiri ubongo/akili.

Tenga dakika chache angalau 25 za kutafakari (medidate) kila siku ili kuwa na amani ya moyo na akili kitu kinachopunguza viwango vya homoni ya mkazo (cortisol).



Chanzo; Tiba Fasta
 
Hivyo tunajua mkuu,tatizo mazingira tunayoishi siyo rafiki sana. Naomba unishauri jinsi ya
1:kufanya meditation wakati naishi kwa mtogole. Ngoma usiku kucha,msuto daily,nk.
2:Hapa nikitoka nikatembeetembee naona vibanda,watu,bodaboda,kelele nyingi.
3:Kulala naingia mapema tu,ila usingizi ni fadhila ya jirani,asipolewa nalala,akilewa nakesha.
 
Back
Top Bottom